Mlangaja
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 579
- 218
Leo tena mitihani ya veta imevuja. Hivi utamaduni wa kuvuja kwa mitihani hapa Tanzania utakwisha lini? Miaka nenda rudi tatizo lipo pale pale. Hivi wahusika wa mitihani huwa wanawajibishwa? Hawa ni watu walioaminiwa na kupewa ofisi na serikali ya Tanzania wasimamie. Hivi wanaposababisha hasara kama hii wanajisikiaje?
Kweli Tanzania ina namna nyingi za ufisadi. Kwangu ufisadi huu wa kuvujisha mitihani ni mbaya mno. Kama taifa lazima tutafute mwarobaini wa tatizo hili. Na kwa kweli wahusika ingefaa wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa vizazi vijavyo.