Habari za leo wana jf nimekuja kwenu tena nikiamini nitapata msaada au njia ya kupata ufumbuzi wa tatizo langu.
Mimi ni binti wa miaka 25 nina tatizo linanisumbua mwaka wa tano sasa kila ninapobeba kitu kizito mfano ndoo ya Lita kumi tu ya maji kwa mwendo hata wa dk 1 huo mkono lazima uvimbe na maumivu. Nikitembea pia miguu itavimba mpaka chini kwenye nyayo na maumivu makali pia kipindi cha baridi joints zote zinavimba na kuuma na maumivu mengi yanazidi jioni mpaka siwezi kutembea au kuchuchumaa.
Nilienda kupima maabara moja hapa Mwanza nikaambiwa nina wingi wa uric acid nikazuiwa kula baadhi ya vyakula na nikaandikiwa dawa masharti niliyafata na nikanywa dozi ya kwanza ikaisha bila nafuu nikaambiwa niirudie lakini pia sikupata nafuu yoyote.
Nikaenda kupima tena kwa hawa madaktari wa kisabato wa tiba lishe nikaambiwa nina cholesterol kwenye damu na matatizo mengine mengi tu nikapewa dawa nyingi sana kwa gharama kubwa iliyonilazimu kusitisha masomo kwa muda ili nifanye kazi. Nikapewa dawa nikatumia zote tatizo likapungua kidogo baadae likarudi tena mpaka sasa sijui nifanye nini maana ugonjwa ndio kama umeamka upya miguu imevimba mpaka kwenye nyayo na magoti na viwiko vya mikono pamoja na maumivu makali sana.
Natamani kwenda Bugando Ila wana gharama kubwa ambazo siwezi kuzikidhi ila maumivu ni makali.
Naamini naweza kupata msaada humu ndani wa nini nifanye au dawa gani nitumie za asili ambazo hazina gharama kubwa angalau nipate unafuu.
Samahani kwa Maelezo marefu sana ila natumai msaada.