Kutwa Mara Tatu (..... x 3) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutwa Mara Tatu (..... x 3)

Discussion in 'JF Doctor' started by IshaLubuva, Sep 9, 2010.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nyingi ya dawa tunazotumia baada ya kupata ushauri wa Tabibu huwa inaelekezwa kuzimeza mara tatu kwa siku kadhaa. Katika kumbukumbu zangu za kupakea maelekezo ya kutumia dawa kutoka kwa Wataalamu wa Afya na hata kwenye matangazo ya dawa yanayotolewa na Redio (za Tanzania na Kenya) neno "Kutwa mara Tatu (au Asubuhi, mchana na jioni)" limekuwa likitumika sana kuwaelekeza wagonjwa namna ya kutumia dawa za kutibu magojwa yanayowasumbua.

  Kuna wakati nilijiuliza maana hasa ya kutwa mara tatu ni nini baada ya kukutana na dozi ya aina fulani ya dawa ambapo nilitakiwa kumeza vidonge kadhaa kila baada ya masaa mnane (8). Hapo nikaanza kuhisi suala la kuchanganya lugha kama hivi:

  Kwa kiingereza tukisema "day" inaweza kuwa inamaanisha mchana (ambapo kwa kiswahili kingine ni kutwa) au siku nzima ya masaa 24 kwa maana ya mchana na usiku (Kutwa kucha).

  Ningependa Wataalamu wa Tiba wanijulishe nini hasa maana ya Kutwa mara tatu; je ni asubuhi mchana na jioni au la?
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kutwa Mara tatu = 8hourly

  That is it!
   
 3. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa maana hiyo wale wanaotuambia Asubuhi, mchana na Jioni wanatuelekeza kumeza kwa interval ya masaa isiyo sahihi siyo? Kiswahili fasaha ingekuwa Kutwakucha mara tatu basi.
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kuna makosa makubwa kwa watoa dawa kuwaelekeza wateja wao kwakutafsiri kiingereza kama kilivyo. Kiusahihi zaidi hakuna kitu kutwa mara tatu, bali mara tatu kwa siku. Ukisema kutwa mara tatu maana yake masaa 12 yenye jua, ambapo ukiyagawamasaa 12 unalazimika kunywa kila baada ya masaa manne. Ina maana kwamba kuna kipindi mwili hubaki na dawa pungufu sana mwilini kuweza kudhibiti ali kama inavyokusudiwa na wagunduzi wa dawa hiyo. Half life ya dawa ndiyo inayokutaka unywe dawa kwa tofauti ya masaa mangapi. Ama sivyo mtu angeweza kunywa saamoja, saa mbili na saa tatu akafunga siku, au aknywa kila baada ya nusu saa lakini mara tatu.

  Dawa inagawanywa mara tatu katika masaa 24 ili concentration ya dawa hiyo kwenye plasma iwe stable kudhibiti hali. Dawa unayoambiwa kutwa mara tatu kwa mfano, half life yake - yaani uwezo wa dawa hiyo kupungua kwa 50% katika damu (kwa lugha nyepesi) ni masaa manane. Ili kuimarisha kiwango kilekile chenye nguvu chanya ya kuleta mabadiliko yanayokusudiwa mwilini, dawa uliyokunywa sa 1 asubuhi itakuwa imeshuka kwa kiwango cha 50% kufikia saa 8 mchana. Kwa hiyo kama unataka dawa ifanye kazi sawasawa, unapaswa kunywa tena kiasi fulani cha dawa saa nane mchana. Kwakuwa ukimeza dawa mara nyingi unachukuwa nusu saa ili ifike kwenye damu, basi kiwango kwenye damu kitapanda kufikia wakati huo, utakinyenyua tena baada ya masaa manane baadaye. Ukifuata hayo ndipo utajua kama dawa imekufaa au la.

  TFDA wasijisahau, wawaambie wauza dawa kwamba wateja waambiwe ni mara tatu kwa siku nzima wakiwasisitizia na masaa yanayotakiwa. Hata mimi zamani nilijua kutwa mara tatu ndio sahihi. Hiyo ndi asili mojawapo ya kufeli kwa chloroquine hasa wapenda sindano. Akichoma mara mbili mchana analala tu usiku, resistance inazaliwa. Habari ndio hiyo kwa maneno mepesi.
   
 5. A

  Adm Senior Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kutwa mara tatu ni sawa na kumpa ama kumlazimisha mgonjwa anywe dozi ya masaa 24 ndani ya masaa 12 tu. Kitu ambacho ni hatari sana
   
Loading...