John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 113
- 222
Kutunza na Kufua Nguo na Matendo Yetu
Nguo au vazi linawakilisha “matendo ya mtu”. Maana yake ni kuwa kiroho, mtu mwenye mavazi safi, maana yake matendo yake pia ni safi. Kinyume chake, mwenye mavazi machafu maana yake matendo yake si safi (Ufunuo 19:18).
Kuna uhusiano kati ya mavazi ya mtu na matendo ya mtu
Matendo ya mtu pia yanatunzwa, lakini pia yanafuliwa au kusafishwa, kama vile nguo inavyoweza kutunzwa na kufuliwa.
Kutunza mavazi yetu
Maana ya kutunza mavazi ni kuhakikisha hayaharibiki wala kuwa na kasoro yanapokuwa mwilini. Vazi lililotoboka au kuchanika maana yake limekosa matunzo, mwisho wa siku yule mtu atabaki tupu. Kwa jinsi hiyo hiyo, ni wajibu wetu kuyatunza matendo yetu mema, yasiharibike.
Kutunza matendo yetu
Kwa kujiangalia mazingira tuliyopo na mabo tunayofanya. Hali hiyo inaendana na Kitabu cha Ufunuo 16:15 kinavyosema: "Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake”. Mambo yanayoharibu matendo yetu mazuri au tabia nzuri ni pamoja makundi tuliyo nayo na mazungumzo tunayofanya katika makundi hayo.
Kitabu cha 1Wakorintho 15:33 kinasema: “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”. Hivyo, ni muhimu kuchunguza makundi tuliyonayo na aina ya mazungumzo tunayofanya.
Kufua nguo zetu
Nguo isiyofuliwa inapoteza umaridadi na unadhifu kwa mtu, hata kama haijaharibika au kuchanika. Vivyo hivyo, matendo yasiyofuliwa yanapoteza unadhifu wa mtu kiroho.
Hii ni kama maandiko katika Kitabu cha Ufunuo 22 kinavyosema: 12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri
kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.
Matendo ya mtu yanafuliwaje?
Hii si kwa njia nyingine bali ni kuomba na kusoma Neno la Mungu.
Na je, utajuaje kuwa matendo yako yameanza kuingia dosari? Na hii pia si kwa kusubiri uambiwe na mtu au watu, bali kwa kusoma Neno (biblia). Unaposoma Neno, ndipo utakapojijua kama una kasoro au la. Hii ni kwa sababu Neno la Mungu ni kioo. Ili ujijue kama una uchafu mwilini, husubiri kuambiwa, kwa sababu si wote wenye ujasiri wa kukwambia kasoro zako. Kitu pekee kitakachoweza kuutambulisha uchafu usoni mwako ni kioo. Unaposoma Neno la Mungu, unagundua kasoro mbalimbali ulizo nazo kiroho, ambazo zinahitaji kufuliwa. Ndiyo maana,
usomaji wa Neno ni lazima uambatane na maombi. Kwa jinsi hiyo, maombi ni “maji” na Neno la Mungu ni “sabuni”. Kwa kufanya hivyo, matendo yetu yatakuwa safi daima.
Hivyo, utunzaji na ufuaji wa nguo au mavazi yetu mwilini, yaende sambamba na utunzaji na ufuaji wa matendo au tabia zetu katika maisha ya kila siku. Utunzaji na ufuaji wa matendo au tabia zetu, hufanywa kupitia kusoma Neno la Mungu, kila siku, jambo ambalo huimarisha utakatifu wetu duniani.
Pia, huimarisha uhusiano na urafiki wetu na Yesu Kristo, na hivyo kujiwekea hazina mbinguni.