Kutumbuliwa kwa Lugola: Askari Polisi waandika waraka, washukuru kuondolewa wizarani kwani aliwadharau na kuwabeza hadharani

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MH. KANGI LUGOLA? - NI HATARI SANA KUISAHAU KESHO

Ndugu askari wenzangu, tunakwama wapi ? Kwanini hatubadiliki? Katika kitabu changu cha "Maandalizi bora ya kustaafu kwa askari" katika ukur asa wa 7 niligusia kuwa kama hutakufa leo basi tambua kuwa kesho pia kuna maisha !

Polisi tumekua na utamaduni wa kujengeana chuki, kuchukiana, na kuwekeana visasi, kupikiana majungu, kutamani mwenzio aharibikiwe!

Mimi hili hata siwezi kulishangaa wala sitalaumu kwa nini iko hivo? Ni kwa sababu ya misingi tuliowekewa au tunayowekeana katika mafunzo tunayopitia kuanzia recruit, resfreshers, promotions courses mpaka katika maeneo tunayofanyia kazi.

Najua ni mara nyingi umekua ukisikia hii kauli polisi hatupendani, Mimi ambae nafundisha darasani katika kila kozi lazima kuna session itaibuka issue ya sisi polisi hatupendani!

Hatuwez kupendana kwa sababu mioyo yetu imejaa sumu iliopandikizwa, imejaa nyongo inayotafuta pa kutokea, hii ni hatari sana kama nayo imekua ni sehemu ya maisha ya askari!

Sasa nije kwenye mada yangu, nimetangulia kusema hivyo kwa sababu Mh Kange alikua ni askari polisi tena wa cheo kizuri tu kabla hajatukimbia kwenda kutafuta pe nye malisho mazuri zaidi, nachelea kusema kwamba tabia aliokua nayo Kange ni ule ule muendelezo Wa utamaduni Wa kipolisi, chuki, fituna na majungu kati yetu!

Mh kange kama tulivyo wengi wetu tunasahu kuwa kesho nayo ni siku, tunajisahaulisha kuwa kuna kesho, ni hatari sana kuisahau kesho! kibaya zaidi kadri tupatapo madaraka ya juu ndivyo uhalisia wetu huonekana, kuna msemo unaosema ukitaka kuijua tabia ya MTU ngoja apate pesa au madaraka!

Hakuna askari ambae alikua hamfahamu mh kange kabla ya kuwa waziri, hakuna mbunge aliekua anajua kutetea maslahi ya askari kama Kange, alikua haxhoki kujitanabaisha na kudeclare interest kwamba yeye, mkewe wote ni askari, kila bajeti alitusemea sana kwa uzuri, alivoteuliwa kuwa waziri askari wengi tulijisemea moyoni hakika sasa tumepata mkombozi, yule tulimngojea kwa miaka mingi, anaetambua shida na matatio yetu si kwa kuambiwa bali kwa kuziishi...

Kadri Siku zilivyokwenda ndivyo mambo yalibadilika, siyo yule Lugola tena tuliemtegemea, kabadilika haraka sana, zile tabia halisi za kipolisi zikaanza kujidhihirisha!

Chuki za wazi, majungu ya kutengenezwa kwa askari zikaanza kuwa sehemu ya mada zake katika kila alipoenda kuzungumza, hakuona shida kumfedhehesha OCS, OCD, RPC, na askari yeyote wa cheo chochote ilifika mahali askari akawa kama mtoto asiye na baba.

Tunajua Mh.Rais JPM alikuamini sana kwa sababu ni askari utaongoza wizara hii yenye majeshi ya zimamoto, uhamiaji, magereza na polisi kwa upendo na kwa weledi Wa hali ya juu. Lakini imekua tofauti na matarajio ya Mh.Rais na sisi uliokuwa unatuongoza!

Tatizo lako ni moja tu ulifika mahali ukaisahau kesho! Ukasahau kuwa kama utabaki mzima basi kesho nayo ni siku! Ulimdhalilisha IGP hadharani tukainama kwa aibu, ulimdhalilisha Kamishina Jenerali wa Magereza mbele ya vyombo vya habari kama mtoto mdogo hata raia walijiuliza kulikonii?

Ile kesho ulioisahau ndio leo! Tuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwako kutokusahau kwamba kuna kesho, hakuna aijuae kesho hivyo hatuwezi kuidharau kesho.

Kila mmoja kwa nafasi yake ana wajibu wa kujitathimini kuhusu anachokifanya leo akioanisha na kesho yake..leo umeaminiwa umepewa madaraka hata kama ni constable ulietoka depo juzi au ndie IGP jiulize unatumiaje nafasi yako? Unalewa madaraka kiasi cha kuisahau kesho? Unaongozwa na chuki, unasikiliza majungu, unatengeneza fitina kwa viongozi au kwa unaowaongoza?

Kesho kofia ya uwaziri, kofia ya ukamanda, kofia ya U-ocd utaiweka pembeni utabaki wewe kama wewe!

Jali unaowaongoza, usiwadharau, waheshimu, usilewe madaraka kumbuka kuna kesho, nayo pia ni siku!

Lotti F.A
Mkufunzi DPA.
 
Attachments

  • AUD-20200125-WA0011.aac
    1.3 MB · Views: 3
Lakini kwa ujumla Polisi wote wa Nchi hii ni washenzi tu..

Mnavyotumwa kwenda kupiga wapinzani na nyie huwa hamuwazi kama kuna kesho??

Kazi ya polisi imekuwa kubambikia raia kesi za uongo..mnatesa raia mpaka wengine wanafia kwenye vituo vyenu..hao matrafiki polisi huko mabarabarani nao ni kama Mungu watu..

Wapi umeona au kusikia wananchi wanashangilia wakiona polisi wao wamepata maafa??..Ni Tanzania tu.

Mna roho mbaya na katili sana polisi wa Tanzania.
 
Tatizo lako ni moja tu ulifika mahali ukaisahau kesho! Ukasahau kuwa kama utabaki mzima basi kesho nayo ni siku! Ulimdhalilisha IGP hadharani tukainama kwa aibu, ulimdhalilisha Kamishina Jenerali wa Magereza mbele ya vyombo vya habari kama mtoto mdogo hata raia walijiuliza kulikonii
Majungu hajayajua vizuri naona, atapigwa majungu hadi atajisahau.
.
Majungu yako majeshini bwana yani kuna majungu hadi hayana majina
 
Nyie Polish acheni ujinga na uzandiki, kwahiyo mlitaka muendelee kukandamiza raia, kubambika kesi, kubania dhamana kisa wkend, kukataza mabasi yasisafiri Usiku mpaka mkatiwe kitu kidogo ndio myaruhusu kwa bahasha, ***** zenu ipo siku mtamkumbuka Ninja na tamaa zenu za kupenda kitonga zitawaponza badilikeni na mtosheke na mishahara yenu.
 
Kangi alisaidia watuhumiwa kufikishwa mahakamani mapema kadri iwezekanavyo kwa mujibu wa sheria!

Alichukizwa sana na mlundikano wa mahabusu kwenye vituo vya polisi kwa muda mrefu kwa kisingizio cha kusubiri uchunguzi!

Actually kulikuwa na value addition kidogo ukilinganisha na kabla yake!

Sasa hayo machache askari hamkuyapenda hadi mumchukie mzee wa ngwasuma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani nyie mapolisi wala msilaumu Lugola.Tabia aliyoonyesha Lugola wengi wenu ndivyo mlivyo.Kwa taarifa yenu raia wa chini,hasa bodaboda,madereva wanamlilia Lugola,mlizoea kubambikizia raia kesi,

Hizo Shangwe zenu hamna lolote,mmefurahia kwa vile aliwabana msionee Raia.Hata wewe uliyeandika hii makala huna lolote.Mzandiki halisi,mwizi,ombaomba,Nyang'anyi.

Unasema Lugola alisahau kesho,nyie Askari kuna hata mmoja wenu huwa anakumbuka kwamba Kuna siku kazi itaisha?.Akili yenu huwa hamkumbuki kwamba utafika muda utastaafu au kuondolewa kazini,ndiyo maana mmekaa kuonea Raia.

Yaani nyie mngejua tunavyowachukia huku uraiani,ni Bora mkistaafu mbaki hukohuko makambini.Lugola kawakomesha kwa kuonyesha uhalisia wenu Askari Polisi,Tunatoa wito kwa Rais,mwambie Simbachawene asimamie yale mazuri aliyoacha Lugola,ikiwepo Askari kutoonea Raia,hasa boda na madereva wa magari.Na nyie Askari Polisi jifunzeni kwa wenzenu wanajeshi,ambao huwezi kusikia analalamikiwa na raia,hata akistaafu,hawana Mambo ya ajabu Kama Askari Polisi.

As long as polis wako nyum ya ris na rais yuko nyuma yao kwa mutual benefit ya october 2020 wacha Lugola afe tu, kanyaga twende lugobola
 
Kangi alisaidia watuhumiwa kufikishwa mahakamani mapema kadri iwezekanavyo kwa mujibu wa sheria!

Alichukizwa sana na mlundikano wa mahabusu kwenye vituo vya polisi kwa muda mrefu kwa kisingizio cha kusubiri uchunguzi!

Actually kulikuwa na value addition kidogo ukilinganisha na kabla yake!

Sasa hayo machache askari hamkuyapenda hadi mumchukie mzee wa ngwasuma?

Sent using Jamii Forums mobile app
Lini kangi aliukuwa mtu mwema namna hii?
 
Back
Top Bottom