Kuna kiongozi fulani aliyekuwa amezuia fedha za kampeini ya kunawa mikono zisifanye kazi hiyo badala yake zijenge vyoo ktk stend moja wilayani kwake. Nilijaribu kumshauri kwamba fedha hiyo si ya serikali na mara zote wafadhiri hutaka fedha zao zitumike kwa matumizi waliyopanga.
Mkuu huyo wa wilaya hakunielewa akasema "potelea mbali hiki ni kipindi cha uteuzi na ninyi mnanipa sifa. Ntaita TBC hapa nionekane nimetumbua jipu kwa bwana mkubwa"! Tulifungasha virago vyetu na kurudi na wafadhiri wakaamrisha turudishe hela yao.
Lengo langu haikuwa kuwapa kisa hicho bali kuwaonyesha upande wa serikali unavyotumia vibaya vyombo vya habari na hasa chombo cha umma kujitangaza ktk vitu vya 'hovyo' na kuacha maslahi mapana ya nchi. Mbaya zaidi wabunge wa Ccm wako kimya
Hivi ninyi wabunge wa Ccm hamuoni jinsi gani mnaingizwa mkenge na upande wa serikali yenu? Mkuu wa wilaya akitaka kumsimamisha kazi nesi jimboni kwako anawaita TBC anauza sura, we mambo yako uliyofanya jimbo wananchi hawatakiwi kuyaona alafu unagonga meza!