Robert edo
Member
- Mar 9, 2015
- 44
- 5
Takribani imepita miezi mi nne tangu awamu ya tano kuingia madarakani na mjadala mkuu inayotikisa kwa sasa ni kile kinachoitwa "kutumbua majibu" wananchi wanashangilia na kuchekelea sana utumbuaji huko, hoja ni kwamba kumng'oa mtu na kumuweka mwingine kwenye taasisi ileile yenye udhaifu mkubwa haitasaidia kuleta mabadiliko.
Mabadiko ya kweli yataletwa na kubadilisha katiba tulionayo kwa kurejea pale ile rasimu ya Warioba hali kadhalika lazima sheria kandamizi zibadilishwe kwani ndizo huchangia vitendo vya ufisadi, mikataba kandamizi, pamoja kuminywa kwa haki za binadamu pamoja na utawala bora.
Tuepuke kuchekelea majibu na badala yake tudai kwa nguvu katiba mpya na kufutwa kwa sheria kandamizi kwa manufaa ya kizazi cha Leo na cha miaka 100 ijayo.