kutukanwa itukanwe CCM tu na siyo CHADEMA kwanini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kutukanwa itukanwe CCM tu na siyo CHADEMA kwanini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkali wa Leo, Apr 4, 2012.

 1. M

  Mkali wa Leo Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwanza niipongeze CCM kwa uzalendo na ukomavu katika Demokrasia sina shaka hii inatokana na kushiriki chaguzi nyingi kidemokrasia...Naipongeza CCM kwasababu imekubali kushindwa kwenye Uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru na kuwaheshimu wananchi waliomchagua Mhe Joshua Nasari kwa ushindi.Rafu nyingi sana zimetendeka kwenye uchaguzi wa Arumeru na matukio mengi ya kikatili yamefanyika...LAKINI TUJIULIZE JE TUITAENDA NA STYLE HII YA VITA KWENYE UCHAGUZI HADI LINI?JE TUNAJENGA?..pili nimrudie mbunge mteule wa MTERA Mhe.Livingstone Lusinde alichokifanya kwenye uchaguzi ni sehemu ya siasa maana siasa ina kejeli na hizi pande mbili zote zimekuwa kama watani wa jadi iweje leo hii lusinde awe gumzo tene baada hata ya uchaguzi..NIWAOMBE TUSHAURI NA TUFANYE MAMBO YENYE KUJENGA PALE UCHAGUZI UNAPOPISHA AMA SIVYO WAAFRIKA HATUTOPIGA HATUA KAMWE MAANA KUMBUKENI WAKATI NYIE WAPAMBE MNAPIGANA KULE NASARI NA LUSINDE WANACHEKA NA KUSHAURIANA BUNGENI..HEBU TUACHE USHABIKI TUJENGE
   
 2. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kama sio lusinde mwenyewe basi ephrem kibonde kaandika hii thread,kwa sababu ndio yalikuwa majibu ya lusinde wakati anaomba msamaha akisaidiwa na kibonde e.clouds fm kwenye jahazi!
   
 3. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Acha upuuzi, mwuungwana akitambua kakosea huomba msamaha. Iweje Lusinde atukane matusi yasiyoandikika asifiwe? Kiukweli Lusinde kwa sababu ya elimu ndogo alonayo au akapimwe akili ana dalili zote kuwa ni mgongwa, yapaswa aombewe.
   
 4. s

  sverige JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  sasa ikiwa kaandika yeye ama mwingine yoyote kipi cha ajabu tuache ushabiki tujenge nnchi
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Huyu ni LUSINDE MWENYEWE KABISA
   
 6. l

  liverpool2012 Senior Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  clouds ni tawi la ccm
   
 7. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huyu ni kibonde,kajipange upya
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  ningetoa wazo hapa, ila sasa bani!!!!
   
 9. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160

  Hata tuliokuwa hatupo Arumeru tulifanikiwa kuyaona matusi ya Lusinde kama unao ushahidi wowote wa cdm kutusi ccm na watu wake uweke hapa wote tuuone
  Kumbuka hatuwezi kuijenga nchi kwa kutukanana na kuvunjiana heshima kwa staili ya Lusinde kwa hili Lusinde amejishushia hadhi yake na chama chake hasa viongozi aliokuwa nao jukwaani.
   
 10. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  aliye andika hapa ni Lusinde au kibonde.
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako unasubili hadi upewe ban ndio ufunguwe ID nyingine, maveteran kama mimi huwa hatuogopi ban wala hatufagilii mtu hapa JF. Nina modem 3 na ID za kutosha.
   
 12. B

  Benaire JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ya Lusinde ni zaidi ya matusi na utani...huwezi kusema Lema ali......." huko gerezani,hii sio siasa hata kidogo.
  Ili jambo sio la kulifumbia macho kama unavyotaka kutuaminisha...kwa kufuata ushauri wako hapa nadhani Tanzania yenye neema tutaishia kuisikia.
  Mawazo yako ni mazuri lakini hayatakiwi kufanyiwa kazi!
   
 13. M

  Mkali wa Leo Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mawazo mazuri siku zote hufanyiwa kazi....
   
 14. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hivi matusi ni sehemu ya ukomavu wa kidemokrasia kumbe? duuuuuuuuuuuuh nilikuwa sijui, wapi mwalimu wa civics?
   
 15. M

  Mkali wa Leo Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mhe lusinde bado ataendelea kuwa kiongozi mahili na shupavu ndani ya chama cha mapinduzi na jamii inayomzunguka tukumbuke alisaidia mno kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la igunga..
   
 16. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Wahaya wanasema...'embwa keba etakaile mukila teluga mwijiko'.......meaning 'mbwa kama hajaungua mkia huwa haondoki jikoni'......darling wangu Konnie embu tujimuvuzishe level 8 Kempinski aka mmu.
   
 17. M

  Mwanamutapa JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 499
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Usitake kututia kichefuchefu wapenda haki, maendeleo na amani hayo maneno aliyoyasema Lusinde ni vijembe au matusi? ingekuwa ni Gobless Lema, Mbowe, Lissu, Slaa au Kabwe wameyasema dhidi ya Kikwete bado CCM wangekuja na kusema ni kejeli? kwa sasa wabunge hawa wapendwa si wangekuwa na kesi ya kujibu mahakani kumtukana na kumdhalilidha Rais wa jamhuri ya muungano? Sasa iweje ni kejeli kwa upande mmoja halafu ilwe ni matusi ya kesi ya jinai kwa upande wa pili?

  Napenda kusema CCM ndio chanzo cha vurugu za siasa Tanzania maana wao huwa hawataki kushindwa na wanadhania ndio chama pekee kina haki ya kutawala Tanzania wakati ni wezi, wanyang'anyi, wanaongoza kwa degree fake, hawana ubunifu wa kumuendeleza mtanzania maana wamesababisha mifumuko ya bei, maisha magumu, kukosekana ajira, kupeana madaraka kindugu, mahospitali kukosa huduma, shule kuwa fake na ili kudhihirisha hawapendi kushindwa hawajawahi kushinda uchaguzi Znazibar tangu mfumo wa vyma vingi kuanza maana muda wote wamekuwa wakiwadhulumu CuF
   
 18. N

  Njelemela77 New Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba CCM watoe tamko japo la kulaani tu tabia chafu ya kada na Mbunge wetu Lusinde. Mimi siamini kabisa kama tabia hii aliyoonyesha inatokana na malezi mabovu ya wazazi wake, bali ni uhayawani aliojifunza kwenye vijiwe vya wavuta bangi. Kama anasema hii ndiyo siasa ya upinzani, basi hajui siasa za upinzani ni nini maana hii ni zaidi hata ya ile siasa ya maji taka. Kama Chama kinashindwa kutoa tamko, naomba Wazee wa Mtera wamkalishe kitako wamfunde kwa mara nyingine tena. Hajakua huyu. Mwenyekiti wa CCM na rais wangu, upo? Hivi kweli unaridhika nchi kuchafuliwa nanma hii na kiongozi wa chama? Matusi ya Lusinde yamewafikia watu wote wanaoongea Kiswahili duniani. Mimi ni kijana ninayetaraji kugombea uongozi wa chama katika ngazi mbalimbali kadri nafasi zinakavyotokea, na nimefundishwa nikafundishika kwamba kiongozi ni kioo cha jamii. Kioo gani hiki? Nitajifunza nini kwa Lusinde?
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Nikishafungua multiples, ntakuwa hivi.

   
 20. S

  Sangiwa Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ushauri wa bure: Mwenyekiti wa chama CCM na rais wangu, kwa kuwa Lusinde amesema mwenyewe hakutumwa na chama kutoa yale matusi, na kwa kuwa aliyoyasema yalikuwa ni matusi dhahiri mbele ya hadhara yakiwa ni zaidi ya siasa basi ni vizuri ungechukua hii nafasi kusafisha jina la chama na jina lako. Tumia kamati ya nidhamu ya chama kutoa tamko ili kuonyesha njia. Hii ndiyo itakayodhihirisha ukomavu wa chama bila kujali Lusinde alisaidia nini Igunga. Ukimezea na kuacha mambo yasonge mbele kama wanavyokushauri akina Kibonde utakuwa umepoteza nafasi nzuri ya kutoa funzo. Watanzania wataanza kuzoea matusi makubwa zaidi, na utakuwa umeshachelewa.
   
Loading...