Kutoruhusiwa kutumia Laptop kwenye Internate Cafe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoruhusiwa kutumia Laptop kwenye Internate Cafe

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by mfianchi, Jan 6, 2010.

 1. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Hapa TZ. Internate cafe nyingi haziruhusu kutumia. Laptops kwenye cafes zao na kama wanarusu basi bei ya muda wa kutumia huwa mara mbili zaidi kulinganisha kama ungetumia PC za cafe sijui tatizo liko wapi,naamini kutokana na mabadiliko ya nyakati ni muhimu watoa huduma au wamiliki wabadilike sioni kwanini kutumia Laptops mtu alipie mara mbili zaidi.
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nafikiri hii imekaa kibiashara sana, kwani wanataka utumie Computer zao ili ulipie kuliko kuiba na kutolipia, Jiulize kama wewe ndo mwenye cafe unawateja wawili wanakuja watu kumi wana laptops zao wanataka kutumia bure utafikiliaje? Je utawakubalia watumie na wakati wewe toka asubuhi una wateja wawili tu?
   
 3. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 4. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35

  Hayo Maswahiba yalishanikuta lakini ninachofikiria mimi wanaogopa kuwa utaupdate laptop yako na hivyo utadownload MB nyingi ambapo itakuwa hasara kwao kwani wao wanalipia kwa MB kutoka kwa ISP.

  Cha muhimu hapa cafe zetu zijipange kukidhi mahitaji ya anaye kuja na laptop yake. It's true anampunguzia mzigo mwenye cafe na inakuwa more advantage.

  Na kama hizo cafe wanalipa kwa MB kutoka kwa ISP wajaribu kuangalia upya mipangilio yao.
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Pale Kijitonyama kuna Cafe inafanya hivyo. Unaenda na Laptop yako wanakuchomekea kwenye outlet yao ya internet ila sina hakika kama wanakuchaji kwa muda ama per MB lakini naona wanapata wateja si haba.
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Hapo kijitonyama nafikiri ni Stambuli Internate cafe ipo jengo la Millenium karibu na mgahawa wa Steers,tatizo siku hizi hapo imekuwa kijiwe cha masuperstar wa bongo flavour wakija ni hadithi tu za nanihii ananibania,sijui produzya fulani kaiba wimbo fulani etc,pia siku hizi Stambuli Cafe si kama zamani net hukatika mara kwa mara na iko slow saana.Ila bigup kwa staff wa hapo cafe kwani wanajali wateja na huduma zao ni za weredi
   
Loading...