Kutokwa damu kwenye meno.

Nyanda lunduma

Senior Member
Apr 10, 2015
187
68
Habari za jioni ndugu zangu wana JF.yapata miezi miwili mpaka sasa nasumbuliwa na tatizo la kutokwa na damu kwenye meno hili tatizo linanipata kila siku ukiamka tu asubuhi ukitema mate inatoka damu kwenye meno,pia hata ukiwa unapiga mswaki asubuhi damu inanitoka kwenye meno
Nawaombeni sana msaada ndugu zangu wana jf nitumie nn hasa niweze kupona.
 
Pole sana. Utapata maelezo mengi sana, lakini kimsingi unashauriwa umpeleke hospitali yoyote akaonwe na dentist.

Kwetu Afrika hatukimbilii sana kufikiria upungufu wa vitamin C mwilini, kwa sababu tunapata vitamin hizo kwa namna nyingi sana. Umeshasema akila tunda la apple anaacha damu, ina maana huyo anao uwezo wa kupata hata matunda aghali hivyo. Machungwa na mapera pia ni mfano mzuri wa chanzo cha vitamin C. Kwa hiyo ni bora kuondoa wazo hilo kabisa kwa sasa.

Hakuna kitu "KURTU" kwenye meno, kwani kutu ni zao la chuma (iron) kushambuliana na oxygen. Hakuna chuma cha namna hiyo kwenye meno. Kinachotolewa ni mwamba unaotokana (tartar au calculus) na mtu kutopiga mswaki meno yake ilivyo sawasawa na kuacha wadudu wazaliane juu ya masalia ya chakula katika aina ya utando kufunika meno, ambapo protein aina ya pellicle hufanya kazi kama cement au gundi kushikilia uchafu huo. Wadudu wanapenda kutumia masalia (au tabaka la) ya chakula kama raw material na kuzalisha tindikali ambayo hutelemsha tindikali ya mdomoni (pH) hata kusababisha meno kutoboka, lakini pia toxin ya harakati ya bacteria hao huumiza fizi taratibu. Ukichelewa utakuta hata mfupa unaoshikilia meno unayeyushwa na meno kuanza kulegea kwa kukosa mahali pa kujishikiza. Palipo na calculus wadudu huwa attracted zaidi kukaa kwa sababu habitat yake huwafaa sana. Miamba hiyo ni ishara tosha kwamba hujapitisha mswaki eneo hilo kwa zaidi ya siku saba hata kama unapiga mswaki kila siku, maana yake hupigi ilivyo sawasawa kila eneo la jino. Daktari analazimika kukusafisha kwa kutumia vyombo maalum kwa sababu miamba hiyo haiondoki kwa kupiga mswaki wa kawaida. Huitwa SCALING.

Fizi zilizoathirika kwa kutopiga mswaki ilivyo sawasawa huwa na dalili nyingi, mojawapo ni kutoka damu hovyo hata kama zimeguswa kidogo tu, na utagundua unapopiga mswaki kikawaida unapotoka damu, ujue kuna eneo ndio kwanza limepata mwaki siku hiyo na fizi zinatoka damu. Hali hiyo huisha yenyewe kwa kuongeza bidii ya kupiga mswaki sawasawa kuzungukia meno yote mdomo mzima. Dawa ya kusukutua anayokupatia sio badala ya kupiga mswaki, maana dawa hiyo haiondoi uchafu bali inafanya kazi ya kuwatibua bacteria wasitawale kwa kuzaliana baada ya wewe kufanyiwa usafi na daktari, kwani wadudu hupunguzwa kasi ya kuzaliana na hivyo kupunguza madhara kwa fizi.

Niseme kwa ufupi tu kwamba mpeleke mgonjwa kwa daktari aone hali halisi ilivyo na kuamua hatua bora ya kumsaidia mgonjwa wako. Inashauriwa mtu amwone daktari wa meno angalau kila miezi 6 kwa check up ya kawaida ili kushughulikia matatizo yoyote yanayojitokeza mapema kwenye fizi au meno. Upigaji mzuri wa meno ni kila siku angalau mara mbili - BAADA ya kifungua kinywa asubuhi na kiwe ndio kitu cha mwisho kabla hujalala usiku kitandani ili kuhakikisha unadhibiti mioto ya bacteria. Sasa kupiga mswaki kabla ya kifungua kinywa ni hiari yako na sio vibaya, lakini sio sahihi kitaalam kwa lengo la kudhibiti wadudu kwa kuondoa masalia ya chakula. Ukiweza piga hata mchana. Hakikisha kila jino limepigwa mswaki sehemu zote. Huwezi kufanya hivyo kwa dakika tatu.
 
Kama unatoka damu baada ya kupiga mswaki... Jaribu kubadili aina ya miswaki unayotumia, acha kutumia miswaki inayokuja na dawa ya meno. Tumia miswaki kama wisdom na inayofanana nayo.
 
Rekebisha mkuu..damu haitoki kwenye meno...ni fizi ndizo zinazotoa damu....swaki vizuri at least twice kwa siku..tatizo litaisha
 
Pole sana. Utapata maelezo mengi sana, lakini kimsingi unashauriwa umpeleke hospitali yoyote akaonwe na dentist.

Kwetu Afrika hatukimbilii sana kufikiria upungufu wa vitamin C mwilini, kwa sababu tunapata vitamin hizo kwa namna nyingi sana. Umeshasema akila tunda la apple anaacha damu, ina maana huyo anao uwezo wa kupata hata matunda aghali hivyo. Machungwa na mapera pia ni mfano mzuri wa chanzo cha vitamin C. Kwa hiyo ni bora kuondoa wazo hilo kabisa kwa sasa.

Hakuna kitu "KURTU" kwenye meno, kwani kutu ni zao la chuma (iron) kushambuliana na oxygen. Hakuna chuma cha namna hiyo kwenye meno. Kinachotolewa ni mwamba unaotokana (tartar au calculus) na mtu kutopiga mswaki meno yake ilivyo sawasawa na kuacha wadudu wazaliane juu ya masalia ya chakula katika aina ya utando kufunika meno, ambapo protein aina ya pellicle hufanya kazi kama cement au gundi kushikilia uchafu huo. Wadudu wanapenda kutumia masalia (au tabaka la) ya chakula kama raw material na kuzalisha tindikali ambayo hutelemsha tindikali ya mdomoni (pH) hata kusababisha meno kutoboka, lakini pia toxin ya harakati ya bacteria hao huumiza fizi taratibu. Ukichelewa utakuta hata mfupa unaoshikilia meno unayeyushwa na meno kuanza kulegea kwa kukosa mahali pa kujishikiza. Palipo na calculus wadudu huwa attracted zaidi kukaa kwa sababu habitat yake huwafaa sana. Miamba hiyo ni ishara tosha kwamba hujapitisha mswaki eneo hilo kwa zaidi ya siku saba hata kama unapiga mswaki kila siku, maana yake hupigi ilivyo sawasawa kila eneo la jino. Daktari analazimika kukusafisha kwa kutumia vyombo maalum kwa sababu miamba hiyo haiondoki kwa kupiga mswaki wa kawaida. Huitwa SCALING.

Fizi zilizoathirika kwa kutopiga mswaki ilivyo sawasawa huwa na dalili nyingi, mojawapo ni kutoka damu hovyo hata kama zimeguswa kidogo tu, na utagundua unapopiga mswaki kikawaida unapotoka damu, ujue kuna eneo ndio kwanza limepata mwaki siku hiyo na fizi zinatoka damu. Hali hiyo huisha yenyewe kwa kuongeza bidii ya kupiga mswaki sawasawa kuzungukia meno yote mdomo mzima. Dawa ya kusukutua anayokupatia sio badala ya kupiga mswaki, maana dawa hiyo haiondoi uchafu bali inafanya kazi ya kuwatibua bacteria wasitawale kwa kuzaliana baada ya wewe kufanyiwa usafi na daktari, kwani wadudu hupunguzwa kasi ya kuzaliana na hivyo kupunguza madhara kwa fizi.

Niseme kwa ufupi tu kwamba mpeleke mgonjwa kwa daktari aone hali halisi ilivyo na kuamua hatua bora ya kumsaidia mgonjwa wako. Inashauriwa mtu amwone daktari wa meno angalau kila miezi 6 kwa check up ya kawaida ili kushughulikia matatizo yoyote yanayojitokeza mapema kwenye fizi au meno. Upigaji mzuri wa meno ni kila siku angalau mara mbili - BAADA ya kifungua kinywa asubuhi na kiwe ndio kitu cha mwisho kabla hujalala usiku kitandani ili kuhakikisha unadhibiti mioto ya bacteria. Sasa kupiga mswaki kabla ya kifungua kinywa ni hiari yako na sio vibaya, lakini sio sahihi kitaalam kwa lengo la kudhibiti wadudu kwa kuondoa masalia ya chakula. Ukiweza piga hata mchana. Hakikisha kila jino limepigwa mswaki sehemu zote. Huwezi kufanya hivyo kwa dakika tatu.
 
Hilo nlkuwa nalo tena kwa miaka kadhaa, ila kwa sasa limeisha kabisa baada ya kutumia juisi za matunda kama vile embe, ukwaju, pesheni na ulaji wa apples niliweka ratba kila siku nilikuwa nakula apple moja(nlkula kama siku kumi hivi). Now napiga mswaki kwa amani, nikila nyama au chochote ambacho kitaacha mabaki kwa meno natumia toothpick bila wasiwasi wowote.
Try it 'n see mkuu, I believe the prob' will over
 
Back
Top Bottom