Kutoka Vijibweni: Rais Magufuli azindua daraja la Kigamboni (Nyerere Bridge)

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,229
5,285

Rais anawasili eneo la tukio na anasalimiana na viongozi mbali mbali. Daraja hili ndo refu kuliko yote Afrika mashariki

Wimbo wa taifa unapigwa na baada ya hapo Makonda anatambulisha viongozi mbali mbali.

Meya wa Dar es Salaam anasimama ns kusalimia. Anasema baada ya uchaguzi sasa siasa zimeisha. Anawataka wananchi kulipa kodi. Anasema Magufuli hela za kuleta maendeleo hatazitoa mbinguni.

Meya wa Temeke anasema Dar ina mameya wanne na wote wamekubalina kuwaheshimu viongozi wa serikali kwani wanategemea ruzuku toka kwa serikali.

Makonda anasoma salamu za mkoa, anazungumzia stend ya Ubungo. Anawashitaki watumishi waliosaini mikataba na kusema kuna upotevu wa milioni zaidi ya 500 kila mwaka.

===================

Ufunguzi wa daraja la kigamboni jijini Dar es salaam lenye urefu wa mita 680 na daraja hilo limegharimu billion 214.6 na lina jumla ya barabara sita za vyombo vya moto na moja ya waenda kwa miguu kila upande, Mh Rais John Pombe Magufuli awasili kwa ajili ya ufunguzi. Rais ameambatana na mama Janeth Magufuli, Naibu Waziri wa Ujenzi Edwini ngonyani, Anthony Mavunde, na Wabunge.

daraja.jpg

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda anaanza kutoa salamu za kutambua meza kuu, Mkuu wa Makonda anasema anaoba kutumia nafasi hiyo kutoa utambulisho anaanza na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndugu Madabida, Wajumbe wa Kamati ya Usalama wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ya Ilala na Temeke. Pia anapongeza juhudi za rais katika kupunga msongamano jijini Dar es Salaam pia daraja litakuza uwekezaji kwa upande wa Kigamboni.

Anaendelea kumtambulisha Katibu wa CCM Mkoa na wabunge mbalimbali Kinondoni, Kigamboni.

Mbunge wa Kigamboni Mh Dr. Ndugulile anakaribishwa na anasema kazi ya muda mrefu imekamilika takribali watu elfu 50 walikuwa wanataabika kufika mjini leo wamepata nafuu na anamshukuru mheshimiwa Rais.

Mbunge Dr. Ndugulile anasema wametenga hekari 1000 kwa ajili ya viwanda, na Kigamboni wanawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza na baada ya kusema machache anamaliza.

Mkuu wa mkoa anamkaribisha meya wa jiji anasalimia kisha anamkaribisha meya wa Temeke. Meya wa Temeke anasema daraja litawaaunganisha wananchi na anaongeza, Dar es Salaam anasema mkoa jiji lina mamaeya wanne ana wamekubaliana kusisitiza nidhamu katika almashauri. Na wamekubaliana kuwaheshimu viongozi wa serikali kuu.

Mkuu wa mkoa anaelezea namna ubadhilifu wa fedha kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo na mikataba ya parking maeneo ya jiji.

=====================
Rais anakaribiswa kwajili ya kutoa hotuba ya ufunguzi, Mh Rais anasema kabla hajazungumza chochote anaomba amkaribishe mtu aliyetoa mchango mkubwa kwenye ujenzi Dr Ramadhan Dau, naye Dr Dau anasema anamshukuru rais kwa fulsa aliyopewa kwasababu hakupangwa kuwa mmja ya wazungumzaji na anaongeza kuwa mpango ulianza mwaka 2002 Mkuranga akiwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa. Na daraja hili litasaidia kukuza uchumi na kurahisisha usafirishaji.

Ujenzi wake ulifanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group. Daraja hilo ndilo la kwanza la kubeba uzito wa barabara kwa kutumia nyaya Afrika Mashariki na la tatu Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara bila kuhesabu Afrika Kusini. Linamilikiwa na serikali ya Tanzania na Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kwa 40% na 60% mtawalia na litachukua nafasi ya feri ya MV Magogoni.

LE.jpg

Mheshimiwa Rais anaanza kuhutubia, Rais ananza kwa kumshukuru mwenyezi Mungu, na kuwashukuru viongozi kwa kumualika kwenye sherehe za ufunguzi. Rais anasema wakoloni kutok uingereza walitaka kujenga daraja mwaka 1933, na pia Mwalimu Nyerere pia aliwahi kuwa na ndoto kujenga daraja lakini fedha za kuwezesha mradi hazikupatikana.

Rais anaongeza "Master Plan" ya jiji la Dar es Salaam inaonyesha kituo cha mabasi ya kutoka Kusini (Mtwara na Lindi) kitajengwa Kigamboni. Mh Rais anasema wizara ilipendekeza daraja lipewe jina lake yeye alikataa na kwasababu na kwasababu ni daraja litakalotumiwa na makabila na watu wa ainza zote anapendekeza liitwe daraja la Mwalimu Nyerere.

Pia daraja hilo litakuza uchumi, utalii na ndio maana hata majirani wanalitamani. Daraja hili linabeba zaidi ya tan elfu moja na life span yake ni zaidi ya miaka mia moja. Pia ujenzi wake unagharama kubwa sana na ujenzi wake utamalizwa kwa upande wa barabara ya kilomita moja. Rais anasema itaongezwa fly over moja na Kigamboni utakuwa mji wa kisasa.

Daraja limejekwa kwa utaratibu wa PPP (Public Private Partnership) hivyo serikali imetoa asilimia 40 na 60 imetoka NSSF hivyo kuta kuwa na ulipaji wa vyombo vya usafiri kama baiskeli, guta, pikipiki, na magari. Lakini wananchi waenda kwa miguu wa hawatalipia matumizi ya daraja.

Rais anawaomba waandishi wa habari wawewazalendo na waitangaze Tanzania kwa mambo mazuri.

Anamwita Makonda aseme mkurugenzi wa jiji kafanya nini, anasema mambo mengi yanatikwa kuamriwa hapahapa. Rais Magufuli amsimamisha kazi mkurugenzi Dar Wilson Kabwe anayetuhumiwa kuingia mikataba iliyosababisha hasara ya zaidi ya Sh. 3bn.

===================

MWISHO:
Akiongea muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi daraja linafaa kupewa jina la Mwalimu Julius Nyerere kutokana na mchango wake kwa nchi hiyo. Rais anatoka jukwaani na kuelekea eneo maalum kwa ajili ya kuzindua daraja rasmi na kisha anazindua rasmi daraja la Mwalimu Nyerere.

Daraja la Kigamboni lilianza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 na lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilomita 2.5.

LEO.jpg
 
Ufunguzi wa daraja la kigamboni jijini Dar es salaam lenye urefu wa mita 680 na daraja hilo limegharimu billion 214.6 na lina jumla ya barabara sita za vyombo vya moto na moja ya waenda kwa miguu kila upande, Mh Rais John Pombe Magufuli awasili kwa ajili ya ufunguzi. Rais ameambatana na mama Janeth Magufuli, Naibu Waziri wa Ujenzi Edwini ngonyani, Anthony Mavunde, na Wabunge.

daraja.jpg

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda anaanza kutoa salamu za kutambua meza kuu, Mkuu wa Makonda anasema anaoba kutumia nafasi hiyo kutoa utambulisho anaanza na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndugu Madabida, Wajumbe wa Kamati ya Usalama wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ya Ilala na Temeke. Pia anapongeza juhudi za rais katika kupunga msongamano jijini Dar es Salaam pia daraja litakuza uwekezaji kwa upande wa Kigamboni.

Anaendelea kumtambulisha Katibu wa CCM Mkoa na wabunge mbalimbali Kinondoni, Kigamboni.

Mbunge wa Kigamboni Mh Dr. Ndugulile anakaribishwa na anasema kazi ya muda mrefu imekamilika takribali watu elfu 50 walikuwa wanataabika kufika mjini leo wamepata nafuu na anamshukuru mheshimiwa Rais.

Mbunge Dr. Ndugulile anasema wametenga hekari 1000 kwa ajili ya viwanda, na Kigamboni wanawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza na baada ya kusema machache anamaliza.

Mkuu wa mkoa anamkaribisha meya wa jiji anasalimia kisha anamkaribisha meya wa Temeke. Meya wa Temeke anasema daraja litawaaunganisha wananchi na anaongeza, Dar es Salaam anasema mkoa jiji lina mamaeya wanne ana wamekubaliana kusisitiza nidhamu katika almashauri. Na wamekubaliana kuwaheshimu viongozi wa serikali kuu.

Mkuu wa mkoa anaelezea namna ubadhilifu wa fedha kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo na mikataba ya parking maeneo ya jiji.
 
Bwana mkubwa anashangiliwa ila JK na Dau hawaonekani
Unajua ukiwa na tuhuma zimejaa magazetini lazima uwe na hofu kuwa Magufuli anavyopenda sifa anaweza akaamuru ukamatwe, hata kama dhamira hiyo haipo. Wanaita kujishuku
 
Hata tujenge miundombinu mikubwa kiasi gani kama Dar itaendelea kusafishwa na wale wakina mama na mifagio yao ile ya mkono kamwe haitakaa ipendeze, daraja hilo linavutia sasa tuwape mda machinga waje kufanya yao, soon daraja la London lenye zaidi ya miaka mia litaendelea kuvutia na kigamboni itabaki kuwakilisha taswira ya muafrika!
 
Alipoanza kuongea Meya wa jiji tu wakakata TBC alipoanza meya wa Temeke wakawa live tena. Meya wa Temeke kaanza mambo ya CCM. Je anauhakika gani kwamba wanakigamboni ni CCM au wachangia kodi wa Dar wote ni CCM. Am sick hasa TBC kuzima live coverage just because Meya wa ukawa kasimama kuongea????
 
Kwenye kitabu kile cha KULI yule Rashid alikaririrwa akisema "yana mwishowe haya"
 
Hata tujenge miundombinu mikubwa kiasi gani kama Dar itaendelea kusafishwa na wale wakina mama na mifagio yao ile ya mkono kamwe haitakaa ipendeze, daraja hilo linavutia sasa tuwape mda machinga waje kufanya yao, soon daraja la London lenye zaidi ya miaka mia litaendelea kuvutia na kigamboni itabaki kuwakilisha taswira ya muafrika!
Jiji limekabidhiwa Ukawa, tupeni muda utaona tofauti
 
Rais anawasili eneo la tukio na anasalimiana na viongozi mbali mbali. Daraja hili ndo refu kuliko yote Afrika mashariki

Wimbo wa taifa unapigwa na baada ya hapo Makonda anatambulisha viongozi mbali mbali.

Meya wa Dar es Salaam anasimama ns kusalimia. Anasema baada ya uchaguzi sasa siasa zimeisha. Anawataka wananchi kulipa kodi. Anasema Magufuli hela za kuleta maendeleo hatazitoa mbinguni.

Meya wa Temeke anasema Dar ina mameya wanne na wote wamekubalina kuwaheshimu viongozi wa serikali kwani wanategemea ruzuku toka kwa serikali

Mbona husemi TBC inamnyima meya wa jiji kusikika live???
 
Nipo nafuatilia uzinduzi wa daraja la Kigamboni ila nimefurahi kuona yule tuliyeambiwa haruhusiwi kuattend, amehudhuria na ametabulishwa yaani Barozi Dau. Cha kusikitisha, wakati wa utambulisho, Meya wa Jiji kwanza katupwa huko nyuma sana, pili wakati wa utambulisho RC Makonda alikuwa hakumtaja mpaka Rais alipomnong'oneza na alipoanza kusalimia wananchi TBC ikazima mitambo. Alipoanza meya wa Temeke akaanza sera za chama as if daraja limejengwa na chama na siyo wachangiaji wa shirika ambao ni NSSF.

Tunaomba TBC muwe na aibu mjue walipa kodi si wote wana vyama bali ni watanzania period.
 
Uzinduzi WA daraja la kigamboni unaendelea sasa hivi live kwenye to mbalimbali! Serikali inastahili pongezi wa hili hali ilikuwa mbaya sana kwa wakazi wa Kigamboni!
 
Back
Top Bottom