ukweli na uongo at the same time.
Kuna baadhi ya wanawake wakiingia kwenye familia, inakuwa kama wamaeingia member alfu wa boko haramu. Sijui ni kwa kujua ama kutojua, wanachonganisha familia nzima. Hapa suluhisho huwa ni mume liyemleta boko haramu huyo, kama anajielewa ama anaweza kum-manage mkewe, mambo huwa nafuu. Ila kama ni mume -----, kasheshe, suluhisho la haraka huwa ni kkumtafutia mahali wakaishi na mkewe mbali na nyumbani, kidogo hupunguza mitafaruku. Kuna kaya jirani, waligombanishwa na wakamwana dah! Na hivi watoto wa kiume walikuwa 5, na wakamwana 5, walikuwa wanaishi jirani jirani tu. Sijui ikawaje hadi mama yao akatimuliwa sababu ya mkamwana, mjane yule akaenda kukaa kwa kijana wake mdogo wa kiume wa 6, ambaye hata hajaoa. Ila walikuwa na wifi yao aliyekuwa anaishi jirani, anauwezo wa kusutana na Dar nzima.
Na kuja shem wangu mmoja, mkewe ni kama alshaba, anagombana na mama mkwe wa miaka 80+, sijui hata anagombana naye nini. Kamfanya mumewe haelewani na mtu hata mmoja, ila mume naye ni bu sho ke tu nadhani. Basi unabaki kumhurumia tu lakini yeye anajiona mbabe wa ukoo.
Hapo kuna wanawake, ambao huwa kama baraka na chanzo cha busara kwa mume. Hata pale palipoonekana kuwa na mtafaruku, unakuta mke anafunika weakness za mmewe, labda kwa kuonyesha ushirikiano na nduguze zaidi. Hapa mfano ni wifi yangu, yale mambo ambayo braza hashiriki kabisa, kama ya kusalimia au kuuguza wagonjwa, wifi ndio mstari wa mbele, so ana cover sana hiyo weakness yake. Kiasi kwamba wao wakiwa tunashiriki kwao sababu ya wifi.
Kwa hiyo, kuna baadhi ya wake wanaleta amani, wengine kwa kweli ni hatari tupu.