Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,420
- 2,271
Mkurugenzi wa Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji ameamua kujitosa kupimana ubavu na Bakhresa katika ligi kuu ya Tanzania kwa kuamua kuinunua timu ya Mbagala Market ambayo imepanda ligi kuu.
Baada ya kampuni ya Bakhresa kuibuka na timu ya Azam katika ligi kuu ya Tanzania, mkurugenzi wa Mohamed Enterprises Tanzania LTD, Mohamed Dewji au maarufu kama Mo ambaye pia ni Mbunge wa Singida mjini, amejitambulisha rasmi kuimiliki timu ya African Lyon ambayo awali ilikuwa ikijulikana kwa jina la Mbagala Market.
Utambulisho huo ulifanyika katika Hotel ya Corasseum iliyoko Oysterbay Dar es Salaam.
Utambulisho huo uliambatana na kutunikiwa nishani wachezaji waliofanikiwa kuifikisha timu hiyo ligi kuu.
Mbwana Samaki ambaye ni mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza alizawadiwa kikombe cha ufungaji bora.
Mmiliki huyo mpya aliwataka wachezaji hao kujituma ili kufanikisha timu hiyo inasonga mbele zaidi na kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu ujao.
Kwa upande wake Mo alisema kuwa atahakikisha timu hiyo haitakabiliwa na masuala ya ukata wa fedha au matatizo yoyote yale.
Kwa kuanzia tayari Dewji ameishanunua kiwanja ambacho anategemea kujenga kiwanja cha kisasa cha soka kitakachokuwa na viwanja vya michezo mingine kama vile sehemu ya gym ,maduka na hosteli za kulala wachezaji.
Uwanja huo upo eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam.
Source: Nifahamishe