papag
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 1,137
- 1,608
Hili la ajira Kombe la Dunia hapa Qatar, litufikirishe sana kama nchi.
Tumejiridhisha pasi na shaka, Afrika Mashariki imetumika sana kama raslimali watu hapa Qatar hasa kwenye maeneo ya security hospitality (Hotel & Bars), madereva na maeneo mengine mitaani na viwanjani.
Naweza kusema kwa uwazi 80% ya maeneo niliyotaja yamechukuliwa na East Africa hasa hasa Kenya na Uganda. Waliobaki (tuseme 20%) ni Wafilipino na West Africa.
Nimeshangazwa na kukuta asilimia ndogo sana ya West Africa kwenye hayo maeneo, nikaambiwa wao wakipata chance ya ulinzi kwa mfano wanatumia muda wa mapumziko kusoma, hivyo wana upgrade position kila mwaka na kwa sasa wengi wao wapo kwenye maeneo ya juu zaidi (management).
Serikali ya Qatar inamiliki train(Metro na Tram), mabasi ya abiria na tax (Karwa). Hili ni eneo lililoajiri hasa. Na usafiri wote huu,umeunganishwa na viwanja vyote vinavyotumika WC.
Swali, kwanini hakuna madereva Watanzania? Kila kituo cha train kina wafanyakazi wengi sana wanaoelekeza watu sehemu ya kwenda. Kwanini hapa hakuna Watanzania?
Kwenye mahoteli, clubs tulizotembelea n.k, walinzi na wahudumu mpaka mameneja, wote ni East Africa, kwanini hakuna Watanzania?
Tumekuja na tafakuri kidogo:
Asilimia kubwa ya watu wanaofanya kazi za namna hiyo ni drop out wa form four au darasa la saba.
University graduate na drop out wa form six watatafuta white collar Job and the like. Je, na huko kuna Watanzania?
Hatujafika huko kwenye hii research, lakini huko naamini bado tunashindana na haohao Wakenya na Waganda, na zaidi wanaongezeka watu wa west Africa.
Kupata kazi huku kwa drop out wetu wa form 4 na std. 7, lazima interview ni Kingereza ili waweze kuhudumia wageni. Form 4 wetu wanaweza kushindana katika interview hizo hapa Qatar au nje ya hapa?
Form Six na graduate wetu hawawezi kuja kuanza kazi za hadhi ya chini, wakitafuta namna ya kujipenyeza juu? Huenda hata hawa tunaowaona wanafanya hivi.
Tuna haja ya kuendelea kushinikiza Kiswahili kifundishwe mpaka ngazi ya chuo kikuu? Tuna uwezo wa kuajiri watu wetu wote ndani ya nchi yetu? Nchi ina haja ya kutuma watu kuja kulitazama hili kwa kina hapa Qatar.
Anyway Jamani, hapa Qatar ikifika saa 11 Jioni inakuwa giza totoro, japo muda unafanana sawa na hapo nyumbani. Na baridi jioni ni kama tuko Arusha. Viwanjani AC kali sana lazima uende na sweta au koti.
Bado tunaendelea kujifunza, tutaendelea kuwajuza.
Imeandikwa na;
Kazimoto,
Kileo,
Amir,
Sam.