eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Asaalam, ndugu yangu...
Mimi napenda kutoa mwelekeo halisi wa kisiasa hapa nchini ya wapi tupo na tunakoelekea..Sitaki kujua tulipotoka kwa kuwa chama kimoja ni zama za mawe.. Moja kwanza nitambulike kama mtu mwenye mlengo wa kati na mtu makini mwenye mwendelezo makini na tafakuri halisi isiyopotosha wala kufurahisha bali kuelimisha kwa ajili ya ustawi halisi wa nchi hii..
Japo waliogoma ni CHADEMA tuu lakini malalamiko kuhusu tume hata CUF na vyama vingine makini vimelalamikia hili.. Kama kweli wote tunataka tume huru na katiba mpya na kufutwa kwa sheria kandamizi kama ibara ya 41(7) inakataza matokeo ya uraisi kuchunguzwa katika mahakama yoyote nchini na kwingineko. Mimi hoja yangu nitalenga katika mrengo wa kati kwa manufaa ya nchi hii. Kama CHADEMA wangekubali matokeo haya kama CUF walivyofanya basi haikuwa na maana kwa kuwa Mwenyekiti wa CUF alitoa hoja siku ya matokeo kuwa tume sio huru kwa kuwa inateuliwa na raisi. Lakini imetokea bahati mbaya CUF wamekuwa chama tawala kule Zanzibar na sasa wamefungwa mdomo nafuu ya CCM.
Katika hali ya kushangaza hii sheria ilitungwa mara baada ya vyama vingi mwaka 1992 ikiwa na nia moja tuu kukandamiza vyama vipya. Swala hapa sio kumtambua raisi au kutoka bungeni lakini hoja ya msingi ni vifungu vya katiba kandamizi ya 1977 ya enzi za chama kimoja.. CHADEMA wangesema wanamtambua raisi hata EU na Umoja wa madola wangewashangaa kwa kuwa wenyewe walisema wazi kuwa hapakuwa na uwanja sawa katika kampeni hadi uchaguzi.. Refa(NEC) imeteuliwa na mmoja wa wachezaji(JK).. Kimsingi mimi bado msimamo wangu utakuwa kutoyatambua matokeo yote ya mwaka huu kwa kuwa utata ulianzia vituoni... Lakini kimsingi matokeo ya uraisi yameleta utata zaidi baada ya NEC kutangaza kuwa wakurugenzi hawatatangaza matokeo mpaka yatumwe NEC..Sijajua kwa nini??? Jambo lingine ni idadi ndogo 41% iliyojitokeza kwa kuwa haijawahi kutokeo toka uchaguzi uanze kufanyika miaka ya nyuma kwa watu chini ya asilimia 70.
Nimefarijika hata juzi mtandao wa haki za binadamu nao wametoa msimamo wa kutaka katiba mpya.. Nikimnukuu Jaji mstaafu Manento alisema katiba inadai Tanzania ni nchi ya kijamaa wakati ukweli unajulikana ni nchi yenye mwelekeo wa kibepari na si vinginevyo.. Katiba ya Kizazi kipya ni lazima na si vinginevyo!!!
Bado nafuatilia nitaongeza niliyonayo?? baadae
Summary: Madai ya CHADEMA NI
1. KATIBA MPYA
2. TUME HURU
3. SHERIA KANDAMIZI KUFUTWA ZOTE