Kutoka kwa wadau wa facebook... kwa nini CUF hawakutoka bungeni kama CHADEMA? pembuzi

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
786
752
Asaalam, ndugu yangu...

Mimi napenda kutoa mwelekeo halisi wa kisiasa hapa nchini ya wapi tupo na tunakoelekea..Sitaki kujua tulipotoka kwa kuwa chama kimoja ni zama za mawe.. Moja kwanza nitambulike kama mtu mwenye mlengo wa kati na mtu makini mwenye mwendelezo makini na tafakuri halisi isiyopotosha wala kufurahisha bali kuelimisha kwa ajili ya ustawi halisi wa nchi hii..

Japo waliogoma ni CHADEMA tuu lakini malalamiko kuhusu tume hata CUF na vyama vingine makini vimelalamikia hili.. Kama kweli wote tunataka tume huru na katiba mpya na kufutwa kwa sheria kandamizi kama ibara ya 41(7) inakataza matokeo ya uraisi kuchunguzwa katika mahakama yoyote nchini na kwingineko. Mimi hoja yangu nitalenga katika mrengo wa kati kwa manufaa ya nchi hii. Kama CHADEMA wangekubali matokeo haya kama CUF walivyofanya basi haikuwa na maana kwa kuwa Mwenyekiti wa CUF alitoa hoja siku ya matokeo kuwa tume sio huru kwa kuwa inateuliwa na raisi. Lakini imetokea bahati mbaya CUF wamekuwa chama tawala kule Zanzibar na sasa wamefungwa mdomo nafuu ya CCM.

Katika hali ya kushangaza hii sheria ilitungwa mara baada ya vyama vingi mwaka 1992 ikiwa na nia moja tuu kukandamiza vyama vipya. Swala hapa sio kumtambua raisi au kutoka bungeni lakini hoja ya msingi ni vifungu vya katiba kandamizi ya 1977 ya enzi za chama kimoja.. CHADEMA wangesema wanamtambua raisi hata EU na Umoja wa madola wangewashangaa kwa kuwa wenyewe walisema wazi kuwa hapakuwa na uwanja sawa katika kampeni hadi uchaguzi.. Refa(NEC) imeteuliwa na mmoja wa wachezaji(JK).. Kimsingi mimi bado msimamo wangu utakuwa kutoyatambua matokeo yote ya mwaka huu kwa kuwa utata ulianzia vituoni... Lakini kimsingi matokeo ya uraisi yameleta utata zaidi baada ya NEC kutangaza kuwa wakurugenzi hawatatangaza matokeo mpaka yatumwe NEC..Sijajua kwa nini??? Jambo lingine ni idadi ndogo 41% iliyojitokeza kwa kuwa haijawahi kutokeo toka uchaguzi uanze kufanyika miaka ya nyuma kwa watu chini ya asilimia 70.

Nimefarijika hata juzi mtandao wa haki za binadamu nao wametoa msimamo wa kutaka katiba mpya.. Nikimnukuu Jaji mstaafu Manento alisema katiba inadai Tanzania ni nchi ya kijamaa wakati ukweli unajulikana ni nchi yenye mwelekeo wa kibepari na si vinginevyo.. Katiba ya Kizazi kipya ni lazima na si vinginevyo!!!
Bado nafuatilia nitaongeza niliyonayo?? baadae

Summary: Madai ya CHADEMA NI
1. KATIBA MPYA
2. TUME HURU
3. SHERIA KANDAMIZI KUFUTWA ZOTE
 

emma 26

Senior Member
Oct 29, 2010
108
2
walikuwa wapi zamani,kwanini wasidai kabla ya uchaguzi,na walilijua hilo tangu mwanzo
 

werema01

Member
Feb 10, 2010
47
0
walikuwa wapi zamani,kwanini wasidai kabla ya uchaguzi,na walilijua hilo tangu mwanzo

emma, zamani unamaanisha mwaka gani?

Ila ufahamu kila jambo lina wakati muafaka wa kufanya....... Huu ndo wakati wa jambo hilo. Kama una ushauri mbadala toa
 

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
786
752
madai hayajaanza leo toka mwaka 1995 Mwanaharakati na mwanasheria maarufu akiwa na Mrema, Bw. Mabere Marando.... Toka kipindi hicho kama unafuatilia siasa madai haya yalianza haswa kuhusu njama ya kuchomekwa vipengere vya katiba kukandamiza vyama vipya vya upinzani... Kama unajua kirefu cha NCCR(National committee for Constituonal Reform) ambayo walikaa mara ya kwanza kabisa kikao pale Karimjee mwaka 1990 kuanza mchakato wa katiba mpya... Lakini mbio hizi hata CUF walikuwepo...

Mwaka huu CHADEMA wamepata bahati ya kuwa na wanaharakati wengi ndio maana wamelazimika kuwa mwanga kwa wengine ili sasa iwe lazma baaada ya diplomasia kushindwa!!!
 

freethinker

Member
Nov 1, 2010
29
0
urasa hiyo ni excuse jibu hoja. Wewe kuwa JF kwa muda mrefu haimaanishi there are no other Great Thinkers outside there. There are greater that us. Let them come
 

Nsaji Mpoki

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
396
64
Naomba nirejee historia ya viongozi waandamizi wa CUF walivyofukuzwa CCM.Mkumbuke kuwa hawa jamaa Seif Shariff Hamad,Khamisi Mloo.Machano Khamisi na Hamad Rashid walikuwa wajumbe wa CC na NEC ya CCM.Viongozi hawa waliondolewa kwenye Uongozi baada ya kutoelewana wakati wa uteuzi wa mgombea nafasi ya Urais baada ya Mwinyi kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Niliwahi kusimuliwa kuwa kwenye kikao hicho alikuwepo mjumbe wa baraza la mapinduzi Colonel Hamisi Darwesh alishawishi kuwatosa kina Hamad kufuatia maagizo ya Rais wa Kwanza Zanzibar Hayati Karume ambayo aliacha kama wosia.
Hivi mvutano wote wa CUF na CCM ulikuwa ni kuhusu hizi personalities ndiyo maana jambo la msingi kama kurudisha madaraka kwa wananchi wa Zanzibar kupitia kutungwa kwa katiba mpya Zanzibar lilikuwa halitiliwi maanani.Nguvu zote ilielekezwa kwenye kugawana madaraka ambayo waliyang'anywa na Kamati Kuu ya CCM mwaka 1988.Mabadiliko haya mnaoyashuhudia yanatokea baada ya Colonel Darwesh kufariki dunia mwishoni mwa 2007.Mimi kwa upande wangu naona mchango wa mageuzi aliofanikisha Seif ni mkubwa na sasa wengine tuanzie alipoishia,badala ya kumshutumu.
 

Samawati

Member
Oct 6, 2010
90
71
Uyu Emma anaishi pande ipi wajameni?.. ako na mawazo ingine kama aishi sayari ya Zuhura! Ata magazeti usomi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom