kamanda wa mara
Member
- Oct 9, 2017
- 23
- 48
Vitu 12 kila mmoja anapaswa kuvifanya mwaka 2018
1. Taka kutimiliza kitu. Usiende Siku zote 365 bila kuwa na kitu akilini unachotaka kukitimiza. Anza kujenga, nunua lile gari, lipa ada, anzisha biashara. Yaani anza tu! Anza kufanya kitu!
2. Tembea na watu wenye busara, akili, na maarifa zaidi ya wewe. Jizingire na watu wanao kuhamasisha, watu watakao kufanya ujiskie unaweza kufanya vizuri, watu watakaokupa changamoto ya kuendelea kujiboresha zaidi.
3. Tazama uvaaji wako na mwonekano wako kiujumla. Usivae tu chochote ilimradi umevaa. Mwonekano wako unaakisi mengi juu ya wewe. Nyoosha vazi lako vizuri, usivae nguo zisizokutosha vizuri kwa kisingizio cha dini. Vaa kwa heshima lakini mavazi yanayokutosha vizuri. Uvaaji wako uwe simpo wenye viwango.
4. Tazama unavyozungumza. Kabla haujafungua kinywa chako, tafakari ni nani unazungumza nae, wapi unazungumza, wakati gani unazungumza, na hakika elewa unapaswa kuwa makini kuitunza heshima yako. Kwa mazingira mengi, penda kuchagua kua kimya kuliko kuzungumza. Unapoamua kuzungumza, ujumbe wako uwe wenye tija.
5. Watembelee wazazi Mara kwa mara. Elewa kwamba wazee kule nyumbani hawahitaji sana fedha zako, na hawahitaji sana kuwepo kwako. Bali, Wanahitaji mtu amabaye wanamuona na hakika wanajivunia kwa mafanikio yake na ambapo ameweza kufika.
6. Kuwa mtu wa kuomba zaidi. Hakika hauwezi ukaishi maisha yako ukiamini vitu vinatokea tu. kuna Mungu anayeruhusu baraka na mema kutokea katika maisha yako. Omba mbele zake.
7. Anza kufikiri na kupanga juu ya kuchumbia au ndoa. Umri wako unakimbia. Anza kununua baadhi ya vitu utakavyo hitaji ukiwa ndani ya ndoa. Jifunze namna ya kuzungumza kwa heshima na hekima. Jiandae vizuri.
8. Kila wakati fikiri chanya huku ukiwa mhalisia pia. Unapoona chui wanamuomba Mungu, usiungane nao. Unaweza ukawa na mtazamo chanya kwamba hawawezi kukudhuru kwasababu wanaomba, lakini hebu kuwa mhalisia pia. Maana baada ya maombi, wataendelea kua chui na hatimaye watakukula tu.
9. Nunua kitu, kifunge vizuri na kisha mzawadie mchungaji wako. Lini ilikuwa Mara ya mwisho kumzawadia mchungaji wako kwa chochote? Ndani ya mwaka 2018 jaribu kufanya kitu kidogo kwaajili yake. Kamwe hauwezi kujua ni nini anapitia katika maisha yake. Muache ajiskie kuwa angalau kuna mtu ndani ya kanisa anamjali.
10. Wekeza zaidi, tumia kidogo. Fedha zako nyingi zielekeze katika kuwekeza. Nunua hisa, anzisha biashara. Hakikisha kwa mwaka huu, una mkondo zaidi ya mmoja wa kipato.
11.Nyerere hayupo tena, lakini Tanzania ipo. Komla Dumor hayupo, BBC bado inaendeshwa vizuri tu, KABA hayupo tena, lakini Multimedia inaendelea vizuri. Jambo la msingi ni kwamba, usiishi maisha yako yote ukitumikia kazi tu. Hakika hautakwenda kaburini na kazi yako. Pata mda wa kutosha wa kupumzika, tembelea familia yako, nenda kwa daktari kupima afya Mara kwa Mara, tembelea bustani, baharini, furahia maisha.
12. Baada ya kusoma ujumbe huu, mshirikishe na mwingine.
Na Peter Msigwa The MP 2018