Kutoka Geneva: Prof Mchome atoa msimamo kuhusu mpango wa kujitathmini wa haki za binadamu

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,012
5,571
Tathmini ya pili ya haki za binadamu ulimwenguni inafanyika leo Jumatatu Mei 9, 2016 Muda huu jijini Geneva, Uswisi, imeelezwa kwamba, Tanzania imetekeleza kikamilifu kwa asilimia tisa tu mapendekezo ya awamu ya kwanza,Katika ya mapendekezo 107 iliyoyakubali kutoka mapendekezo 166, Tanzania imetekeleza kwa asilimia 62 sehemu ya mapendekezo hayo wakati haikuyatekeleza kabisa mengine kwa asilimia 29.

Taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) ilieleza kwamba, tathmini ya kwanza ilifanyika Oktoba 3, 2011 ambapo mataifa 48 yalitoa jumla ya mapendekezo 166, lakini Tanzania ikayakubali 107
Ch_1xtXWUAE4pos.jpg

Kutoka Geneva, Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome, anatoa msimamo wa serikali ya Tanzania juu ya mapendekezo 107 kuhusu uboreashwaji wa haki za binadamu. Kikao hiki kipo live online hivyo mtu yoyote anaweza kufuatilia.

Ratiba ipo kama ifuatavyo;

09:00–12:30 Review of United Republic of Tanzania

13:00–14:00 Adoptions of Samoa and Greece

14:30–18:00 Review of UPR of Antigua and Barbuda.

Kufuatilia Mkutano huu fungua hapa=>25th Session of Universal Periodic Review
 
Tanzania bado hatujafikia hatua nzuri, tunahitaji kuongeza bidii katika hili!
 
Back
Top Bottom