Kutoka Bungeni Dodoma: Julai 18, 2011

Tuko pamoja Buchananila haka kamama kababe haka,ngoja tuone michango sasa
 
Sasa ni Hotuba ya Nishati na Madini, Wabunge wameanza kuchangia hoja!
 
Suala la uchimbaji wa Madini ya Uranium Bahi, Mbunge anakusudia kuunga mkono wananchi 6000 wa Bahi kwa kuwasilisha hoja Bungeni kupinga uchimbaji wa Uranium Bahi!
 
Akichangia kwenye mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini leo Jumatatuu, Mbunge wa Bahi amekataza kwa mbunge toka sehemu nyingine Tanzania kuongelea nidhati ya Uranium iliyoko Jimboni kwake Bahi na kusema kuwa yeye ndio mbunge wa eneo hilo.

Je, ni sheria gani inamkataza mbunge kuongelea jambo lililoko kwenye jimbo lingine? Wabunge wana hata miliki ya maeoneo wanayowakilisha? Ina maana hakuna mbunge anaruhusiwa kuongelea sehemu kama wewe si wa eneo hilo i.e madini Bulyanhulu, North Mara, mbuga za wanyama Serengeti, Manyara, Mlima Kilimanjaro etc?

Nini tafsiri ya 'hoja kwa maslahi ya Taifa'?
 
Magamba bwana: eti tunamlaumu bure Mh Ngeleja amepewa fedha kidogo kwenye Bajeti yake! Mbunge wa kwanza kuchangia ndio kaunga hoja mkono ila amedai kuwa mwakani kama tatizo la umeme likiendelea eti "hawatapitisha Bajeti ya Nishati na Madini!"
 
Ni kweli, so far sijaona wachangiaji wa maana aliowasoma!
Hotuba muhimu za bajeti ni mbili tu. Ile ya Bajeti yenyewe inayosomwa na waziri wa fedha na ya ofisi ya Waziri Mkuu. Hizi nyingine ni kwa ajili ya posho kwa Wabunge masikini. Wabunge na mawaziri wengi wako hapa Dar sasa hivi.
 
Kwa wale mlio mbele/mbali, Hembu sikilizeni bunge letu la 10 Lilivyoendelea huko Mjengoni, ni zaidi ya zekomedy, nashauri udownload hii track, ni 1.7MB then usikilize!!

Bungeni Kariakoo!!
 
Madini ni suala la muungano na sio jimbo..........asiige wazanzibari huyo
 
magamba bwana: Eti tunamlaumu bure mh ngeleja amepewa fedha kidogo kwenye bajeti yake! Mbunge wa kwanza kuchangia ndio kaunga hoja mkono ila amedai kuwa mwakani kama tatizo la umeme likiendelea eti "hawatapitisha bajeti ya nishati na madini!"

huyo mbunge ni mpumbavu sana kwa hiyo tuendelee kukaa gizani hadi mwakani.........wakati ni sasa tuchukua hatua, wapi mabunge kama ya india, kenya nk mbunge akiongea pumba unamtwanga kiatu usini.
 
Mdau endelea kutujuza yanayojiri huko bungeni. Hivi hakuna radio inayotangaza mkutano wa bunge LIVE
 
Mbunge wa pili amedai Ngeleja aliwadanganya wananchi wa Wilaya ya Kerwa (huko Kagera) angewapelekea Umeme lakini kwenye vitabu vya Bajeti vya Ngereja mradi huo haujaonyeshwa! Hajaunga mkono hoja ila anasubiri wananchi wake wamweleze aunge mkono hoja au la!
 
Daahhh, hii title yako Bungeni "Kariakoo - Wimbo"??

Hiyo "Kariakoo - Wimbo" umenikumbusha nyumbani kabisaaaaa, kijiwe sio cha kawaida hicho cha enzi hizoooo.
 

Hongera CCM, lakini mnajua takwimu za vifo vitokanvyo na hizo pikipiki? manajua wangapi leo hii hawana miguu?
ugawaji wa pikipiki uende sambamba na uimarishaji wa hospitali za mifupa pamoja na kuongeza maeneo ya makaburi.
Ni ushauri wa bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…