Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 28,423
- 39,501
Habarini Wadau,
Hapo jana kulikuwa na uwasilishwaji wa ripoti ya pili ya WIZI wa mali ya Umma. Hili limeumiza wengi sana hususan watanzania masikini na wenye shida mbalimbali wakati nchi yao imejaa rasilimali. Wengi waliisikiliza ripoti ile.
Lakini, binafsi nikikumbuka yale maneno makali yaliyojaa hasira yaliyotolewa na Mh. Rais Magufuli, inanifanya nijiulize je Andrew Chenge (aliyekuwa mwanasheria mkuu wa muda mrefu zaidi kutoka Harvad University) ana ujasiri gani wa kuendelea kukaa katika madaraka?
Nazir Karamagi hata akihojiwa atajitetea nini mbele ya watanzania kwa wizi na utumiaji wa mali zao?
Ni kwanini Mkuu wa nchi alitoa fursa ya wao kuhojiwa badala ya kushitakiwa moja kwa moja?
Hawa wahujumu uchumi na Mafisadi wa mali za watanzania masikini ni kwanini wanapata viburi na ujasiri wa kuendelea kuenjoy uongozi na maisha hapa nchini?
Je Mh. Rais atawachukulia hatua kali kweli hawa?
Nawasilisha.