Kutofautiana katika siasa

Mamzalendo

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,670
558
Habari zenu ndugu wanajf!
Mimi leo nina mawili matatu ninayofikiri ni muhimu

1.Kuwa vyama tofauti haimaanishi uadui na kwamba kila anachosema mpinzani wako ni upuuzi, ujinga na kukuonea. Ni vizuri tukijenga misingi ya kutofautiana katika points muhimu. Mfano wapo watu humu jf wamezungumzia elimu ya mheshimiwa mbunge wetu lema, kwa kweli sijaona kwa nini chadema wanakuwa so defensive nilidhani ni kitu rahisi tu kisichohitaji kutukanana kwamba tungejibishana tu kwamba litaangaliwa basi. Kwa sababu soon or late it may have an effect to him as a politician. One of th 48 laws of power is learn to use your enemies, so take note of what your opposer is saying

2.Jambo lingine kuwa katika chama fulani haimaanishi kuwa ukubaliane na kila kitu ndani ya hicho chama whether ujinga au jambo la hekima nafikiri unaweza kutokubali na ukawa na misingi sahihi ya kutokubali na ukaitoa na unaweza kwa kutokubali kwako ukawafungua wenzio macho kwenye jambo ambalo wao hawajaliona. Kwa hiyo tusiwe watu wa ndio katika kila kitu bali tureason for the benefit of all the Tanzanians.

3.Jambo la mwisho jamani watanzania wenzangu naomba niweke msisitizo katika hili no research no right to speak. Kama jambo hulijui vizuri usiwe mwepesi wa kuchangia whether linakugusa au la! Maneno ya ajabu ajabu yapo mengi sana humu mi sidhani kama ni sahihi. Nasisitiza kuheshimiana katika mawazo hata kama unaona anatofautiana na wewe badala ya kumtukana au kumpa neno la kashfa muelimishe kwa utaratibu kwa nini wazo lake ni bovu na la kwako ni zuri hivyo tutakuza siasa zetu katika critical and useful arguments.

NAWATAKIA PASAKA NJEMA WOTE!
 
Back
Top Bottom