Kutibu na kuzuia tatizo la ngozi kavu

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,162
705
TATIZO LA NGOZI KAVU

Somo hili limeletwa kwako na:

S&E BEAUTY SOLUTIONS
WATAALAM NA WASHAURI WA AFYA, NGOZI NA VIPODOZI

0 659 528 724 , 0 784 082 847
Facebook : S&E BEAUTY SOLUTIONS

Ngozi ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu. Inafanya kazi mbalimbali kama vile kuulinda mwili, kusaidia kutoa takamwili, kusaidia kuratibu joto, maji na chumvi ya mwili pamoja na kuhisi vichocheo kama vile joto, baridi, miguso, mkandamizo nk kutoka nje ya mwili. Richa ya hayo, ngozi ni sehemu muhimu sana katika muonekano na uzuri wa mwili. Ngozi ikiwa nzuri na mwili huwa vizuri, ngozi ikiwa vibaya na mwili pia huweza kuwa vibaya.

NGOZI KAVU NI IPI?

Ngozi kavu ni aina ya ngozi yenye upungufu wa mafuta na maji ya kutosha kuweza kuifanya iwe na afya njema, kuifunika na kuiunganisha ili iwe katika hali nzuri. Matokeo yake seli za ngozi hunyauka, huachana na hata kuwa kama magamba na kuweza kubanduka. Ikizidi ngozi kavu huanza kupasuka na kuwa na vidonda na maumivu.

SABABU ZA KUWA NA NGOZI KAVU

Ngozi kavu hutokana na kufeli kwa mfumo wa kuweka sawa kiasi cha maji na mafuta katika ngozi; yaani maji na mafuta yanayozalishwa, yanayoingia, yanayotoka na yanayoondolewa. Hilo husababishwa na

- Mtu kutokunywa maji ya kutosha- Kuunguzwa na jua na joto kali vinavyofanya maji mengi kupotea

- Matumizi ya vipodozi vikali vinavyoharibu ngozi na mfumo wa maisha ya ngozi- Ngozi kuzeeka

- Ukosefu wa mlo kamili (bora)

- Kemikali zinazokausha ngozi kama vile kemikali za kusafishia, sabuni za kufulia na kuoshea vyombo na Kemikali za kuua vijidudu zenye asili ya pombe (Kwa mfano Spiriti)

- Ngozi kutofunikwa na mafuta ya kutosha kuzuia maji yasipotee

MATATIZO YA NGOZI KAVU

Ngozi kavu huzeeka haraka kuliko ngozi ya kawaida. Hii hutokana na kasi ya kufa kwa seli zake kuwa kubwa zaidi na afya ya seli zake kuwa dhoofu.

Pili ngozi kavu ni rahisi zaidi kupata maambukizi, magonjwa na majeraha. Kadiri ukavu wa ngozi unavyozidi ndivyo magonjwa yanavyokuja na kuiharibu zaidi ngozi.

Tatizo jingine la ngozi kavu ni kwamba hunyauka na kusinyaa, na kufanya muonekano wa ngozi usiwe mzuri.

Kuondokana na matatizo hayo ni vyema kutibu ngozi kavu ili irejee kuwa ngozi ya kawaida. Pia kama mtu hauna matatizo hayo ni vyema ukajikinga ili usiwe na ngozi kavu na kuyapata.

JINSI YA KUTIBU NA KUJIKINGA DHIDI YA NGOZI KAVU.

Ngozi kavu huweza kutibiwa na kurejeshwa katika hali yake ya kawaida. Pia mtu anaweza akaitunza ngozi yake na kuikinga isiwe kavu. Hayo huweza kufanikishwa kwa kufanya yafuatayo:

- Kupaka mafuta ya kutosha yenye uwezo wa kuongeza maji (MOISTURIZER) na kutunza kwenye ngozi maji (unyevu) wa kutosha na kuifanya iwe na maji ya kutosha. Vipodozi unavyoweza kutumia hapa ni Losheni zilizoandikwa MOISTURIZER, mafuta yaliyoandikwa PETROLEUM JELLY, au GlycerineKunywa maji ya kutosha kila siku ili yafike na kukaa kwenye ngozi na kuitunza

- Kula lishe bora (mlo kamili) na ya kutosha kila siku ambayo itasaidia kuijenga na kuilinda ngozi vizuri (Vyakula vya wanga, protini, mafuta, nyuzi nyuzi, vitamini, madini na maji ya kuosha )

- Kupaka vipodozi vinavyoendana na ngozi kavu na vilivyotengenezwa mahususi kwa ajili ya ngozi kavu. Kwa mfano tumia mafuta au losheni zilizoandikwa FOR DRY SKIN

- Epuka jua na joto kali. Unaweza kufanya hivi kwa kufunika vizuri mwili wako, kupaka vipodozi vinavyoukinga mwili dhidi ya miale mikali ya jua (SUN BLOCKERS/SCREENS) , kuepuka kushinda au kufanya kazi juani, kuoga mara kwa mara nk

- Epuka vipodozi vikali (na kemikali zingine) vinavyoharibu ngozi na kuikausha. Usiogee sabuni kali, usipake mkorogo, losheni, krimu na mafuta makali kwa ngozi na pia usichubue ngozi.

Yote kwa yote, pata ushauri wa kitaalam kwa kila kitu unachotaka kufanya au kipodozi unachopenda au kutaka kukitumia.

Tumia vipodozi vizuri ili upate matokeo mazuri.

S&E BEAUTY SOLUTIONS INAKUTAKIA AFYA NJEMA……..
 
hii hapa mahsusi kwa ngozi kavu na athari za kuchomwa na jua
piga 0769103506
IMG-20181105-WA0004.jpeg
 
Back
Top Bottom