Kutengua uhamisho wa TAMISEMI

Statistics

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
3,594
7,586
Habari waungwana,

Mwezi may 2016 nilikamilisha michakato ya uhamisho nikitumaini mapema July kuhama, toka mkoa wa mbeya kurejea mkoa wa mwanza, halmashauri ya misungwi.

Baadae June, mwaka uliopita likatolewa zuio kwa mwezi, ambao umekuwa mwaka sasa.

Kwa sababu jina langu lipo tamisemi na kwa sasa sihitaji kuhama tena,

Je, nini nifanye ili jina langu lisipate kibali?

Au nini nitafanya kama jina likapata kibali na kutakiwa kuhama, kumbuka tunabadilishana na afisa mtendaji mwenzangu wa kata.

Natanguliza shukrani.
 
Zuzu on freak!
 
Hiyo simple sana mkuu maana barua ya uhamisho toka tamisemi haikufungi.
NANUKUU MAELEZO YA BARUA HAYO.

"Unaelekezwa kubaki ktk kituo chako cha awali iwapo hutakuwa tayari kwa sababu yoyote ile kujigharamia uhamisho ulioomba. Hivyo utapaswa kutoa taarifa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Halmashauri uliyokubaliwa kuhamia".

MWISHO WA KUNUKUU MKUU.
Mimi ni miongoni mwa watu waliobahatika kuhama mwaka 2015 JULY.

MAELEZO HAYO NIMENUKUU TOKA KWENYE BARUA TOKA TAMISEMI IKINIRUHUSU KUHAMA KUTOKA X KWENDA Y.
 
Usitoe taarifa popote hata ile barua ya uhamisho uliyoomba ikija ipokee afu tulia uwa kuna siku unazoambiwa ukaripoti kituo kipya uliipoomba zikishaisha ujaripoti uhamisho unajifuta automatically na taarifa zako za kiutumishi zinaendelea kubaki hapo ulipo so haiathiri chochote yupo mtu alifanya hivyo had ssa yupo kituo chake cha awali mwaka wa nne huu hakuna kilichotokea aliahirisha kuhama.
 
Back
Top Bottom