Kutembelea nyota ya mtu mwingine!

Kutembelea nyota ya mtu mwingine!

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
KUTEMBELEA NYOTA YA MTU MWINGINE!

Fuatana nami

Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️

Je, umewahi kusikia watu fulani fulani huko wakisema "fulani anatembelea nyota ya fulani?"

Na je, nini ulikuwa mtazamo wako kuhusiana na kauli hiyo au kauli kama hiyo?

Tumefundisha kwa miaka mingi kuhusiana na elimu ya Nyota na angalau watu wengi sana waliotupinga kwa nguvu zote miaka hiyo, hususani miaka ya 2019 kuja 2020 na 21, wengi wao ni wadau wakuu wa elimu hii siku hizi. Huo ni ushindi kwa waalimu wote wa ELIMU YA NYOTA kwa Afrika Mashariki na Kati; kwa hiyo hapa sitaanza kwa kuelezea maana ya nyota, acha niende moja kwa moja kwenye hoja.

Unaposikia watu wanasema kwamba mtu fulani anatumia nyota ya mtu mwingine au nyota za watu wengine, ni ukweli usiopingika kabisa.
Kuna uwezekano mkubwa endapo mtu akiamua kutumia nyota yako au ya mtu mwingine, kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa sababu kila mtu ana aina ya nyota inayosapoti mambo fulani tofauti na wenzake.
Aidha, kuna Nyota ambazo zenyewe kwa asili yake zinasapoti nyota zingine hususani Nyota ya Simba na Nyota ya Ng'ombe.

Mtu akianza kutumia nyota yako kwa maslahi yake, ni wazi kwamba wewe unakuwa unamfanyia kazi yeye kwa kujua au bila kujua, unakuwa unamnufaisha yeye.

Kuna njia nyingi za kutumia nyota ya mtu kufanikisha mambo yako, nitataja njia kadhaa:

1. Tendo la ndoa
Hili tendo ambalo wazungu huliita SEX ni tendo ambalo mtu mke na mtu mme wakikutana kimwili, wanabadilishana nishati zao; huyu anabeba za huyu na yule anabeba za mwenzake. Ndio maana ya neno S.E.X ambalo kirefu chake ni Sacred Energy Xchange!
Kila unapokutana kimwili (kingono) na mtu awaye yote, awe mkeo/ mumeo au la, mnachofanya kiroho mnabadilishana nguvu, unampa zako anakupa zake.
Sasa watu wengi wana nguvu au nishati (au roho) chafu ambazo zinaharibu mambo, sasa wakilala na wewe, wanakuachia zao chafu wanabeba za kwako safi, mkitoka hapo wewe unaharibikiwa wao wanasonga mbele (wametumia nyota yako kujisafishia au kuoshea nyota yako)

2. Huduma za jamii
Kama nyota yako ni safi na inang'aa alafu mtu 'akaiona' na akaitaka, anaweza kuanza kujitolea kukusaidia au kukuhudumia mahitaji yako yote bila kuhitaji chochote kutoka kwako.
Kikawaida utamuona ana roho nzuri (ni sawa), lakini kiuhalisia (kiroho) unakuwa unampa uhuru wa kuitumia nyota yako kufanikisha mambo yake.

3. Kugawa fedha na zawadi kama nguo, viatu, saa nk.
Kama mtu 'akiona' nyota yako inang'aa sana, lakini hujitambui, basi anaweza kuichukua 'kwa kuinunua'
Atafanya hivyo kwa kuchukua pesa na kuinuizia manuizo (spells) fulani fulani, kisha atakupatia kwa mkono wa kushoto na atajitahidi kuhakikisha na wewe unapokea kwa mkono huo. Tendo hilo linakuwa ni alama au Ishara ya mauziano, anakuwa amenunua nyota yako.
Asipotumia fedha anaweza kutumia nguo, saa, viatu, soksi au chochote kinachotoka kwenye mwili wake.

ZIPO MBINU AU NJIA NYINGI ZA KUPEANA NYOTA, ACHA NITAJE HIZO TATU TU.

Watu walio kwenye hatari kubwa ya 'kuibiwa' Nyota zao wengi ni wale wa Nyota za Simba na Ng'ombe, wachukue taadhari.
Kuna namna nyingi za kufanya ili kuilinda nyota yako isichezewe.

Nyota yako ikiwa chafu au imechezewa, fanya ufanyavyo, huwezi kutoboa!

Somo litaendelea......
Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

By Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom