Kutembea ukiwa usingizini

Hapana wanga ni ngumu kuwaona kwa vivid eyes

Jr
Kuna rafiki yangu alinisimulia kila ifikapo saa nane na nusu atake asitake lazima aamke kinachomwamsha hajui,saa kumi na moja anapitiwa na usingizi Ni kila siku hali hi inamtokea yapata miezi mitatu Sasa,na akiamka hua haoni chochote usingizi unakata kabisa,na muda Ni huo huo nane na nusu pengine hii yaweza kua Nini hasa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni tatizo la wengi na imekuwa kama mazoea sasa.. Hata mimi mida hiyo mpaka sasa saa tisa na nusu nakuwaga macho... Labda kwakuwa ndio mida ya wanga na zilaili mtoa roho
Jr
 
Mm juzi nilishtuka ghafra nikaenda sebuleni nikajilaza mweny Kochi mda kama dakika moja nikajiuliza mbona nimekuja sebulini nikajipa jawabu kuwa kitandani Kuna nyoka ,huez amini nilijilaza kwenye Koch takribani dakika 5 ,ndipo nikarudi kitandani nikiwa over confidence ,nikalala kiukweri niliwaza Sana ,nikawasha simu nikaanza kusikiliza kwaya ,nikapitiwa na ucngiz .Sasa hii har ckuelewa Nini maana yake
 
Wanga walikutembelea na wakawa wanakufanyia michezo yao
Jr
 
hii sentensi ina uzito, ila wengi hawajaelewa kilichoandikwa. thanks mshana pia kama utapenda , jaribu kuongelea haya maswala ya fikra. kwamfano, nini kinatokea ukikaa na fikra moja kwa muda mrefu
, hata miaka.. nini ambacho kinajijenga rohoni.

Kwa baadhi ambao hawana tatizo lingine lolote lakini huwa mahiri na waliobobea kwenye fikra za kufikirika hufikia kutengeneza matendo halisi kwenye ufahamu na kujikuta wanayatekeleza usingizini bila utashi wa nafsi
 
Kaka yangu nae kama wewe.anaamka anakimbilia mlango huku anapiga kelele.mshana wanasaidiwaje kwenye hali ya namna hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohammed Saidi Abdullah (MSA), aliizungumzia sana hii dhana ya mtu kutembea akiwa usingizini katika kitabu chake cha "Mzima wa Watu wa Kale". Mojawapo wa mambo aliyokuwa akijiuliza ni kuhusu mwili na roho wa muhusika unakuwa katika hali gani. Pia alieleza uwezekano wa roho kupotea iwapo muhusika atashituliwa kutoka katika hali hiyo na hivyo kusababisha kifo. Kuna visa vimetokea hapa Duniani ambapo muhusika alitenda kosa la kuua na akarejea nyumbani kulala pasipo kujua nini kinaendelea. Katika hali hii kuna utata kuweza kujua kama mauaji yaliyofanyika ni jinai au vinginevyo. Wanasaikolojia wanaweza kuielezea vizuri hali hii.
 
andika kwa lugha ya kiswahili tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True experience mimi kuna siku nimelala ghafla najikuta sebuleni nimejigonga kwenye meza ya kioo mkononi nilikuwa na glass ya maji ikaanguka pembeni puu ile sauti ghafla ikamshtua wife akaamka kwa hofu na mimi hapo ndio nikarudi kwenye ufahamu wa kawaida wife kuniuliza vipi mi nikamjibu hata sielewi nimefikaje sebuleni kuangalia fridge ni kweli lipo wazi akaanza kufoka mipombe yako hiyo angalia umemshtua mtoto analia wakati kipindi hicho nilikuwa sijagusa pombe kama wiki Tatu nikaona tusibishane bora nikae na yangu moyoni
 
Mimi huwa naamka naanza kupiga kelele na hiyo hali inajirudia Sana miaka zaidi ya 10 na huwa sikumbuki bali naambiwa na watu nao lala nao tatizo inaweza kua nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nitafanya hivyo nipe muda
hii sentensi ina uzito, ila wengi hawajaelewa kilichoandikwa. thanks mshana pia kama utapenda , jaribu kuongelea haya maswala ya fikra. kwamfano, nini kinatokea ukikaa na fikra moja kwa muda mrefu
, hata miaka.. nini ambacho kinajijenga rohoni.

Jr
 
Hakuna jinai kwakuwa hakuna utashi wa mtenda.. Yani hana fahamu kamili na kile alichofanya japo cases za namna hii ni chache mno
Jr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…