Kutembea na mke / mume wa mtu sio ujanja

madamu bahati

Member
Dec 8, 2019
5
184
KUTEMBEA NA MUME WA MTU/MKE WA MTU SIO UJANJA NI UJINGA...

Ujinga ni pale unatembea na mume wa mtu lakini unakazana kutuma picha za uchi kwa mke wake kwa madai kuwa unamkomoa mke wake;

(1) Mwenzako kaolewa, ana ndoa na likitokea la kutokea anarudi kwa mkewe, yaani unamringisgia kumpata mume wake wakati yeye alishampata kitambo na ndani kawekwa!

(2) Hakuna kipya ambacho unamtumia na yeye hana, kwamba kamaa ni hivyo vifaa vyako unavyotaka avione basi nayeye anavyo, nikujidhalilsiha tu unamtumia uchi wako mwanamke mwenzako akuone ili nini, kwamba atagundua kuwa wakwako una madini labda atajisikia vibaya kuwa wakwako upo mabegani?

(3) Unatuma mnafanya mapenzi na mume wake, sasa kuna kipya kipi, mwenzako kafanya, kashamtumia huyo mwanaume na inawezekana na kuzalishwa kazalishwa, kwamba labda kuna staili mpya umegundua kwamba mkifanya mapenzi huyo mwanaume anakojoa noti ndiyo unataka kumuonyesha ili kumrusha roho!

(4) Mwenzako ndiyo kashafika, katulia, ananyanyaswa lakini haondoki, wewe bado kijana, ukifikisha tu miaka 28 utaanza mara kutafuta mtoto, mara utataka kijana wako, mara utakutana na mtu unaingia kwenye ndoa. Mipicha yote ushampa unategemea yeye akianza kulipa kisasi na kumtumia mume wako au mpenzi wako kuna ndoa hapo. Wanawake wanasamehe ila unafikiri mchumba wako akiona huo uchafu hata ukimuambia nilifanya kabla ya kukutana na wewe atakuelewa, atakuona Malaya tu unajiuza na kukuacha!

(5) Hembu jithamini kidogo, unajua mnajidhalilisha, na hii mitandao aisee, hivi siku ukakutana na mwanamke kichwa maji, unamtumia mapicha yako ya uchi ana mfowardia Baba yako utasema nini? Au kwakua umeficha sura, anascreenshopt na namba yako anamtumia dingi yako anamuambia “Mkanye mwanao” ndiyo utafanya nini?

NB; Nina hasira, nimeandika usiku na kuna mtu yamemkuta, hembu mjifunze basi na kudanga, achene kudanga kipuuzi namna hii ujumbe umewafiki mkitaka kulike mtalike msipotaka kucomment kisa nimesema ukweli poa kazi yangu ni kuwaelekeza

Sent using i phone x
 
Huyo mwanaume aliyeamua kuchepuka kama haitoshi akaona upate na picha sio mume huyo...ni mvulanabaharia
Hakupendi, hakutaki, hakulindi wala hakuthamini

Wahenga tunasema akufukuzae hakuambii toka
 
km ni wewe
1576682589392.png
Bahati pole. duh wamemchukua Mumeo / hawara? halafu wanakutumia mapicha wakidinyana, muite mwambie ni style gani hajaipata mpe atulie, la sivyo anza mbele utaumia dadangu
 
Wadada wa mjini,wadangaji na maslay Queens hawawezi kukuelewa hata kidogo.

Wale wazee wa vitonga ndio kabisa hawataki hata kuuona uzi huu.

Ila kaa ukijua hamna mtu mbaya kama anaye iharibu ndoa ya mwenzie,hasa ile ndoa iliyo toa matunda ya watoto.

Kwani ndoa ikivunjika wanaopata tabu hasa ni watoto ambao ktk makuzi yao watakosa upendo wa mzazi mmoja na baadaye kuna uwezekano wa kutooana umuhimu wa ndoa,mwisho wa siku mnatengeneza kizazi kijichojali familia au kisichojali watoto.
 
Haya yote yatakwisha ikiwa watu wataacha kuchepuka. Tukitibu chanzo cha uchepukaji watoto, watapata malezi ya baba na mama.
Wadada wa mjini,wadangaji na maslay Queens hawawezi kukuelewa hata kidogo.

Wale wazee wa vitonga ndio kabisa hawataki hata kuuona uzi huu.

Ila kaa ukijua hamna mtu mbaya kama anaye iharibu ndoa ya mwenzie,hasa ile ndoa iliyo toa matunda ya watoto.

Kwani ndoa ikivunjika wanaopata tabu hasa ni watoto ambao ktk makuzi yao watakosa upendo wa mzazi mmoja na baadaye kuna uwezekano wa kutooana umuhimu wa ndoa,mwisho wa siku mnatengeneza kizazi kijichojali familia au kisichojali watoto.
 
Maisha ni mchafukoge
Maisha yamejaa vurugu
Maisha yana alama zote
Ndio! Alama za hisabati
Kuna kutoa na kujumlisha
Kuzidisha na kugawanya
Pia kuna skwea ruti nyingi
Aidha usisahau anda bruti
Kuna hesabu ngumu mno
Lakini zingine kama maji
Mradi kuna hesabu anuai
Yanini kujipa taabu bure
Kuwananga wana wa Adam
Wana waso na staha au soni
Kila leo kujadiliana na Shetani
Huwawezi aslani jali yako

Bazazi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njooni kwangu wanawake wote mnaosumbuliwa na waume zenu,maana room na gegedo nitagharamia mimi
 
Back
Top Bottom