Kutembea Kwenye Utelezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutembea Kwenye Utelezi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichuguu, Nov 29, 2008.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Nov 29, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Baada ya kusoma maoni mbalimbali kuhusu swali na Elektron, naomba kuweka swali jingine la challenge kama hilo. Sote tunajua kuwa kutembea kwa viumbe wengi ardhini kunategemea kuwapo kwa msuguano (friction) kati ya kiumbe hicho na ardhi.

  Je kuna sababu kwa nini lazima kutembea kufanyike kwenye uso (surface) wenye friction tu? Kwa nini viumbe visitembee kwenye uso wenye utelezi bila matatizo? Je kuna kiumbe chochote kinachoweza kutembea kwenye utelezi bila tatizo lolote? Ni kiumbe gani hicho na kinatembeaje?
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unazungumzia Amoeba hapo ,huyo ndo pekee anaeweza kutembea katika anga hizo wengine ni fungus ambao wao sio kutembea tu wao wanajenga kabisa na kuishi hapo na kuzidisha utelezi .ila sijakufahamu unazungumzia utelezi gani maana hata nimewahi kusikia kuwa jamaa alipanda mlima akateleza mwengine alipanda mkarafuu akateleza mwengine alivuka mto akateleza na kuburuzwa na maji..........kiswahili kikubwa !
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Labda ktk kuchangia kidogo nilichonacho, wakti tunafuta ujinga huko skuli tuliambiwa kwamba msuguano baina ya mtembeaji na ardhi sio chanzo cha; mwendo,kubadili uelekeo, au kusimama kutoka ktk hali ya mwendo, bali husaidia tu hayo mambo anuai. Kanuni ya 3 ya Newton ikizingatiwa, nguvu ya msuguano si kisababishi bali nguvu itokanayo na nguvu anzishi/kisababishi.

  Hivyo basi si sahihi kusema kuwa bila msuguano hakuna mwendo, kubadili uelekeo au kusimama. Ili mambo haya yatokee inabidi nguvu sababishi na ambukizi ziwe ktk uwiano.

  Kukosekana kwa msuguano kutaweza kusababisha mwendo au kusimama kutoka ktk hali ya mwendo kuwa ngumu kutokana na kukosekana kwa msuguano na kusababisha utelezi. Hali hii itasababisha mwendo, kubadili uelekeo au kusimama kutoka ktk hali ya mwendo kuwa shaghalabaghala na hivyo mambo mengi ktk shughuli za kila siku za mwanadamu kuwa shakani.

  Was'alam
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Nov 29, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Ninazungumzia kiumbe mwenye miguu anayeweza kutembea kwenye uso tambarare wenye utelezi kama vile tope laini au oil.

  Ulilosema ni kweli,

  Siyo kila mwendo unahitaji msuguano; kwa mfano, mwendo wa ndege angani hauhitaji msuguano kabisa. Ila inapotokea mwendo baina ya vitu viwili sambamba, kwa mfano mtu au gari linapotembea kwenye uso wa ardhi basi msuguano unahitajika ili kuwezesha mwendo huo, ingawa siyo unaosababisha mwendo.

  Je kuna kiumbe chochote chenye miguu kinachoweza kutembea kwenye uso wenye utelezi bila matatizo yoyote?
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama kiumbe atakuwa shetani hakuna mwengine ,halafu umesema ana miguu ndio kabisa maana mashetani wanatembea hata kwenye moto na kwenye ukuta hukatiza tu au chura.
   
Loading...