God'sBeliever
JF-Expert Member
- Sep 1, 2015
- 5,786
- 3,068
Kuna sehemu inafikia maishani matatizo yanakua yamekuzunguka chungu mzima. Ukifanya hiki shida, ukigeuka shida, ukitafakari yanazuka mapya ila naamini bado ipo sehemu ya maisha iliyo bakia.
Mpini wa jembe unaweza vunjika katikati lakini ukatumia hiyo nusu iliyobaki kuendelea na kilimo na maisha nayo ni hivo hivo. Sio mwisho pia.
Wapo watakaofurahia mateso yako, wapo watakaochekelea gizani ilimradi waonekane wako na wewe kumbe wanafiki tuu. Wapo watakaojitokeza waziwazi kukukebehi pengine kushangilia na kupiga vigelegele masumbuko yako, ila yote ni maisha hakuna jipya dunian mengi marudio.
Wapo watakao kusaka au kukutengenisha na jamaa zako kusudi kuchochea ugomvi kusudi kupata tuu sababu ya kukumaliza na kama haitoshi watu hao hao watatokeza mbele na kujinadi eti ni wema wewe ndio uliekua mbaya hivyo umepata thawabu yako. Ila yupo Mungu mkuu mno uweza wake sii kama binadamu. Yeye ndie mtetezi wa wanyonge, waskini na waliokata tamaa wamtegemea yeye.
Wenye nguvu ndio wao kila wanalofanya ni jema hata kuhukumu uhai wa mtu wao ni wema ila mnyonge ajitokeza atete jambo jema kwa maslahi ya wote huyo atakua kikwazo na muuaji/mpenda damu... kwa kweli hii dunia hakuna haki bora mtu ujikalie kimya tuu maana kwa wema wako utajeuka chungu na kuweka jeraha ndani ya moyo wako lisilofutika milele.
Naungana na waliokata tamaa, kunyanyasika, kudharaulika, kudhulumiwa, kusemwa vibaya, kudhalilishwa na hata kutishwa usalama wa maisha yao kwa kile wanachokisimamia. Daima Mwenyezi-Mungu awe faraja kwenu maana binadamu si kitu hata umtumainie bali Mwenyezi-Mungu, Usitarajie malipo kwa kila jema utendalo bali tenda kwa upendo.
Zaburi 5:7-12