Kutegemea Mabadiliko Kupitia CCM, Ni Sawa na kutegemea Kukamua Kuku Maziwa

Hakika nawaambieni,Magufuli atamaliza miaka mitano hajafanya lolote.sikutegemea mtu mwenye elimu kubwa (Phd) azifagilie sifa za kinafki za mtu kama makonda...hakika tuna safar ndefu.yangu macho tu....nadiriki kusema,bora ya JK...
 
CHADEMA wanaopenda kutambulika kama chama mbadala wa CCM, bado hakijaweza kujipambanua na yote ambayo wao wanaona ni mabaya ya CCM. Utawala bora ungeanzia ndani ya CDM, Mbowe angeachia uongozi mwaka 2014 na sio kujiongezea muda kwa sababu ya ushawishi wake ndani ya chama. Unataka vijana waendelee kubakia mitaani wakicheza pool na kuvuta ganja kuanzia saa mbili asubuhi, kwa hasara ya nani kama sio taifa kwa ujumla?. Unaridhika sana unapowaona vijana wenye nguvu za kufanya kazi wakishinda wanazunguka maeneo ya vituo vya mabasi, huku wakitazama mabinti legelege ili wawaibie pochi na simu zao halafu wakimbilie vichochoroni.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuongea kama mwanaharakati fulani, na kuongea kama mtu ambaye anayo majukumu makubwa ya kuleta maisha mazuri kwa nchi yake. Unafika wakati ambapo hatuwezi kuendelea kusikiliza ngonjera nyingi za wanaharakati, ambazo zina faida kwao kwa maana ya ongezeko la pato mifukoni lakini halina faida kwa wengi waliobakia njia panda kutokana na ugumu wa maisha.

JK alipendwa kwa sababu aliwapa uhuru wengi kiasi cha kujikuta akivumilia mpaka matusi na kejeli kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, huyu mwenyeji wa chato simuoni akifuga ujinga, hata kidogo. Nchi ilijisahau, watu wakajisahau. Na kujisahau kubaya zaidi ni kule ambako watu wanataka waendelee kuishi maisha yale yale ya malumbano, wakati maendeleo ya kweli yanaweza kupatikana ndani ya uwezo wetu. Kuna fedha nyingi inaliwa kwa maana ya mishahara hewa, watu wanabuni njia mbalimbali za kupiga fedha ya serikali, this time around imekula kwao, wahesabu maumivu makali.
Ninyi ndio raia mizigo, mnatetea maovu na kujipendekeza mfumo wa mafisadi mkisahau kuwa kuna wanyonge 90% wa nchi hii wanateswa na mafascist wa serikali ya CCM. Unajitia upofu kutokuelewa hoja iliyotolewa kwasababu akili huna imeshikiliwa na walio Lumumba, ufahamu uko tumboni.

Haya yanayotokea zbar wajinga na waovu walio ccm ndio wanayashangilia, lakini aibu ni kuwa wanaenda misikitini na makanisani kumnajisi Mungu. Nenda kawambie huko Lumumba kuwa moto wa jehanamu unawangoja na utawafanya mkaa mbali na ubinafsi na anasa za uongozi wanazowafanyia Watanzania masikini.
 
"Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani hata masaa 48 wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa".

Rais John Magufuli wakati wa Kiapo cha Wakuu Wa Mikoa
15/03/2016.

Hii kauli mbaya sana inayochochea ukandamizaji wa haki za binadamu imetolewa na kuongeza kasi ya udikteta imetolewa na anayeitwa kiongozi mkuu wa nchi akiruhusu ukiukwaji wa sheria na unyanyasaji wa wanyonge......huyu ni rais Magufuli Joseph.

Huu ni uovu mwingine CCM inaupalilia kutesa na kunyanyasa Watanzania katika taifa lao kuishi utumwani kwa shinikizo la uongozi wa kidikteta unaoratibu masilahi ya makada mafisadi wa ccm.

Kama huyu mtu anania ya kupambana na mafisadi, na kuondoa umasikini Tz mbona toka aingie madarakani;

Hajakamata wahujumu uchumi katika awamu ya pili, tatu na nne?

Mbona hajahoji mikataba ya kifisadi katika awamu ya pili, tatu na nne?

Mbona hajaongelea kukubali maoni ya wananchi ya rasimu ya katiba ya Tume iliyoongozwa na Warioba?

Mbona hajaonesha nia ya kuhoji utajili wa viongozi wa ccm na wafanyabiashara makada wa ccm?

Mbona hahoji na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wafanyabiashara wa mihadarati na kujulisha umma?

Mbona uchumi unazidi kuyumba....Benki Kuu inadorora na hakuna hatua yoyote inayochukuluwa?.....shilingi inaporomoka kila kukicha na hadi sasa hakuna utaratibu unaofanyika kulinda na kukuza uchumi wa Tanzania?

Mbona hajachukua hatua dhidi ya "dolarization" shilingi haitumiki bali dola na euro ndizo pesa zinazotumika nchini?

Haya yote yanayofanyika kuwa kuna kasi ya utendaji ni sarakasi zisizo na mpagilio zilizojaa fujo na uparaganyishaji wa idara mbalimbali bila kubadilisha chochote maana mifumo ni mibovu sana hivyo hakuna jipya linalotarajiwa wala hakuna kitakachofanyika kumpa raia wa chini unafuu wa maisha.

Wananchi wengi hawana ardhi, mitaji hakuna, benki za kigeni zinafyonza uchumi wa nchi yetu na riba ziko juu sana.

Wananchi wengi ni watazamaji ktk uchumi wa nchi yetu ila wamiliki wa biashara na viwanda asilimia kubwa ni wageni....hili halijaguswa na haligusiwi na hawa waimba kasi ilihali ni speed za mbayuwayu zisizo na mwelekeo maalumu na hazijabeba lolote la maana linalomgusa mwananchi wa kawaida.

Hapa tunategemea:
  • Kuendelea kuona vifo vingi vya akina mama na watoto,
  • Ukosefu wa elimu bora na ujinga kuongezeka,
  • Ukosefu wa ajira kuendelea kuwa mkubwa sana.
  • Utapiamulo (malnutrition) kuendelea kuwa janga na kudumaza akili na afya za Watanzania.

Umasikini unaendelea kutesa watanzania na kuendeleza gap la wasionacho na walionacho kuwa kubwa maana hakuna jipya kati ya awamu ya nne na ya tano.....uozo ule ule, timu mbovu ile ile ndiyo imepangwa kucheza mpira na katika uwanja ule ule.....hili ni janga kwa wananchi makabwela wasio na kimbilio.

Majanga ya kijamii kama wizi, ukahaba na utupaji wa watoto yataongezeka kwasababu watu wanaendelea kukosa mwelekeo kwa kulishwa maneno na vitisho utadhani tuko utumwani/kwenye koloni la CCM.

WAKUU WAPYA WA MIKOA.

Niliwahi kusema haya kuwa kamwe haitatokea CCM kufanya mabadiLiko yenye tija kwa wananchi wanyonge.

Ni zaidi ni ukosefu wa ufahamu kutegemea zimwi CCM lililozoea kula vya kunyonga na kubaka demokrasia kuratibu mabadiliko ya kumnufaisha mwananchi mnyonge.

UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA....NI JIPU

Mkumbuke kwa utaratibu wa CCM Rais anatakiwa kuwa M/kiti wa CCM.

Hivyo Mkuu wa nchi wa vikosi vya ulinzi na usalama anakuwa M/kiti wa CCM....hilo ni kosa na huondoa uwezekano wa uwepo wa utawala bora.

Ndio maana Magu anateua makada wa CCM kushika nafasi za kiserikali na kuagiza vyombo vifanye kazi ya kuilinda CCM kwa kisingizio cha kutuliza gasia.

Katika ilani ya UKAWA ilianisha wazi kupunguza ukubwa wa serikali. Mojawapo ya mbinu za kupunguza ukubwa wa serikali ni kuondoa nafasi za uongozi zisizo na tija.

Mathalani....mfumo wa uongozi wa mkoa utakuta viongozi wafuatao:
-Mkuu wa Mkoa
-Katibu Tawala Mkoa
-RPC
-Mayor wa Jiji baadhi ya mikoa

Hawa wote ni viongozi wakuu wa mkoa na wanalipwa mishahara, marupurupu, usafiri, makazi, bima kwao na familia zao, fedha za uhamisho n.k

Huu ni mzigo mkubwa sana unaobebeshwa wananchi wanyonge walipa kodi wanaoteswa kwa umasikini ilihali serikali ya ccm inatengeneza nafasi za viongozi wasio na kazi ya wananchi bali wanawekwa kulinda masirahi ya CCM na mafisadi waliojaa chama hicho.

UDHAIFU WA UTEUZI.
Katika uteuzi huo mbali na kuwa hauungwi mkono na wanamabadiliko mbaya zaidi unamadhaifu mengi sana.

1. Uteuzi wa wazee wastaafu.
Asilimia kubwa ya wateule wa ukuu ni wastaafu waliokwishatumika kwanini wasipewe vijana wenye fikra mpya, ubunifu wa kisasa na mbinu mpya za kupambana na umasikini?

2. CV zao zinatia shaka
Hawa wakuu wa mikoa huteuliwa kwa misingi ya ukada wa CCM na uswahiba kati ya mteua na mteuliwa.

Kuna wanajeshi na makada wastaafu wanaopewa ukuu wa mkoa ilihali hata elimu ya kidato cha sita hawana.

Mara nyingi unakuta hawana elimu ya uongozi na menejimenti kabisa.
Hawa wanaperekwa kuwa maboss wa wataalamu wote ktk mkoa....hili ni tatizo kubwa sana.

3. Ukuu wa mkoa ni ufalme wa kumalizia maisha

Hii haipingiki maana mkuu wa mkoa hana majukumu bali ni mtoa matamko na kuzindua matamasha na kuwakirisha ccm ktk serikali. Hii ni hujuma kwa wananchi masikini na vyama vya upinzani.

4. Uteuzi wa waliokosa ubunge

Hii ni dharau kwa wananchi na kukanyaga demokrasia.

Mtu amethibitishwa na wananchi kuwa hafai kuwa kiongozi ila rais anamteuwa kuwa mkuu wa mkoa.

Mtu ameshindwa kudeliver na wananchi wakaona ni mzigo rais anaubeba huo mzigo na kuutwisha wananchi. Wajinga wanashangilia tu lakini nchi yetu itaendelea kuwa masikini kuendelea kuwa na viongozi hovyo.

5. Mfumo hovyo wa uwajibishaji wa Mkuu wa Mkoa

Hawa huishi kama wafalme katika mkoa na hakuna wa wakuwajibisha, hakuna wa kuwapangia kazi, hakuna wanaporipoti na hakuna anayewakagua.

Hawa huishi peponi tu kufuja mali na kuvuna utajili, kulipwa kwa historia ya ukada na fadhila kwa aliyemteua.

6. Uteuzi wa Viongozi wa Kijeshi kuwa viongozi wa kisiasa.

Hii ni hatari kubwa dhidi ya ustawi wa demokrasia.

Viongozi wa polisi na JWTZ hushawishika kujipendekeza viongozi wa ccm ili wakiistafu wapewe fadhila ya ulaji ktk ukuu wa mkoa.

Hii ni mbaya maana hawezi kutenda haki dhidi ya vyama vya siasa vinavyotetea masirahi ya umma kupata viongozi bora.

Kwa utaratibu huu kikundi kidogo kinaungana kuratibu ulaji wa wachache na kuweka rehani maendeleo ya wananchi ilimradi wakuu wa ccm na wanamtandao wameridhishwa kuendelea kuiweka ccm madarakani.

7. Ni viongozi wa ccm na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa utaratibu huu Wakuu wa Mikoa hulinda masirahi ya ccm kwa nguvu na mbinu zote kandamizi.

Jambo hili huunganisha serikali na ccm na vyombo vya ulinzi na usama kuwa kitu kimoja sawa na timu ya Simba. Hili ndilo chimbuko la uongozi mbovu na umasikini nchi yetu.

Takukuru na polisi hupewa amri na makada wa polisi kwa sababu bosi wao ni kiongozi wa CCM na hujikuta wako katika shinikizo la kutumika kisiasa kulinda ajira zao.

Hapa ndipo fedha za umma hutumika kwa masilahi ya CCM, mishahara na posho wakidai wanalinda usalama wa umma kumbe ni usalama wa ccm.

Hivyo basi tusitegemee kupata mabadiliko kupitia CCM. CCM na viongozi wake wapo kutetea kikundi cha watu wachache.

Huyu Magufuli hawezi kufuta mwenge, wakuu wa wilaya na vyeo vingine vyenye masilahi ya CCM ila mzigo kwa wananchi kwasababu huwezi kutenganisha kiwiliwili na kichwa....CCM imesuka mfumo wa kutawala sio kuongoza...tena kutawala kidikteta.

Nchi inakuwa na kundi kubwa la viongozi wanaofuja fedha za umma ila hakuna jipya lolote wafanyalo kukwamua umasikini wa Watanzania.

Ni CCM na viongozi wake wote ni majipu maana ndio wameasisi huu mfumo mbovu uliokwamisha maendeleo ya nchi yetu.

Huyu Magufuli ameweka hapo kulinda huo mfumo uliomweka hapo. Hivyo kutegemea CCM kuondoa umasikini ni ndoto za alinacha.

Na;

Solomon M. Kambarangwe
15/03/2016

Well done Kambarangwe
 
Ninyi ndio raia mizigo, mnatetea maovu na kujipendekeza mfumo wa mafisadi mkisahau kuwa kuna wanyonge 90% wa nchi hii wanateswa na mafascist wa serikali ya CCM. Unajitia upofu kutokuelewa hoja iliyotolewa kwasababu akili huna imeshikiliwa na walio Lumumba, ufahamu uko tumboni.

Haya yanayotokea zbar wajinga na waovu walio ccm ndio wanayashangilia, lakini aibu ni kuwa wanaenda misikitini na makanisani kumnajisi Mungu. Nenda kawambie huko Lumumba kuwa moto wa jehanamu unawangoja na utawafanya mkaa mbali na ubinafsi na anasa za uongozi wanazowafanyia Watanzania masikini.
Asante sana Kamanda
 
Ha ha ha, povu linakutoka, mishipa ya shingo imekusimama. Mfumo wa mafisadi umemzalisha Lowassa na Sumaye ambao ni mnao huko CHADEMA, kama mfumo mbovu tunaomba muwarudishe CCM hao watu wawili pamoja na mzee Kingunge. Mbowe aliona amepata vifaa vya maana kumbe kazoa makapi. Wewe mwenye ufahamu unaweza vipi kuwa shabiki wa chama ambacho kilipiga sana kelele kuhusu ufisadi wa Lowassa halafu baadae kikampokea kwa mikono miwili. Hayo ya Zanzibar ni upepo na utapita salama. Moto wa jehanam unakungejea hata wewe pia, nani anayeujua upuuzi unaoufanya gizani?. Unafikiri kunywa viroba kunaambatana na akili isiyo na ushawishi wa kutenda dhambi?. Pole sana mkuu.
 
Binafsi nina wasi wasi na uwezo wako wa uelewa au pengine ujambuzi wako ni wa kihistoria na sio wa Kisayansi.

  1. Kwa mtu muelewa; ningetegea ujiulize; Raisi amekaa madarakani kwa muda gani?
  2. Ameweza kuongeza ukusanjaji wa mapato kwa kiasi gani?
  3. Katika kuongeza ukusanyaji wa mapato ni kazi kiasi gani imefanyika?
  4. Changamoto kadhaa za Elimu zimeanza kupatiwa majawabu; ikiwepo Elimu bure shule za msingi na sekondari; Wanafunzi wote wawe wamekaa kwenye madaraka ndani ya miezi sita; Vyuo vikuu vimeanza kukaguliwa ubora na baadhi vimenza kufungwa na vingine kupewa muda.nk
  5. Shule za Serikali zina pitiwa upia zifanyiwe maboresho na kurudisha hadhi yake ya enzi ya mwl Nyerere nk.
  6. KUMBUKA: Nchi haindeshwi kwa kufurahisha watu ..inaendeshwa kwa utaratibu...na hata hao wafanya biashara wakubwa waliokwepa kodi bado tunawahitaji kwani Nchi huwei kuendesha bila wafanya biashara- Japo inahitajika wafuate utaratibu ambao walikuwa hawajauzoea.
  7. Kumbuka wafanyabiashara wasiolipa kodi na baadhi ya mafisadi wameajiri watanzania wengi chini yao. Hivyo ni lazima kuweka mfumo wa kuwa tayari kubeba pale watakapo dhihirika kuwa hawafai kuendelea na shuhuli zao...sio kukurupuka kwa kufurahisha watu wasio na uelewa kama wewe.
  8. wewe ni lile kundi la watu wanao angalia upande mmoja wa kukosoa tena kwa hoja za mtoto wa Nassari??? Ungeandika na upande wa Pili wa yaliyo fanyika kwa siku mia ili tulinganishe (Ingekuwa ni research hapa umepata Zero au basi 5% ya supervisor)
  9. Unaweza kujiuliza tu Rais Obama imemchukua muda gani kufunga lile Gereza la guantanamo bay prison cell???

Uzuri ni kuwa Nchi zilizo tuzunguka na Mataifa ya Dunia yana anza kutupigia mifano kwa utawala bora unaowajali wananchi... wewe ndio Kipofu usiyeona kazi iliyofanyika kwa siku mia!!
Yaani wewe ni marehemu wa kufikiria na hujitambui kabisa, hiyo namba 7 imenikera kuliko zote na ndiyo maana CCM inatamba mtaji wake ni wajinga kama wewe. umeandaika hivi "Kumbuka wafanyabiashara wasiolipa kodi na baadhi ya mafisadi wameajiri watanzania wengi chini yao". hii compromise ni ya kijinga, kuna watu wamebambikizwa kesi wako magereza ila hawa mafisadi wamepakatwa na ccm, kuna watu waliiba kuku au mahindi wako magereza, mafisadi wakubwa unaleta excuse za kipuuzi. You are a prisoner mentally kwasababu CCM ndio wamekushikia ufahamu na maamuzi.
 
CHADEMA wanaopenda kutambulika kama chama mbadala wa CCM, bado hakijaweza kujipambanua na yote ambayo wao wanaona ni mabaya ya CCM. Utawala bora ungeanzia ndani ya CDM, Mbowe angeachia uongozi mwaka 2014 na sio kujiongezea muda kwa sababu ya ushawishi wake ndani ya chama. Unataka vijana waendelee kubakia mitaani wakicheza pool na kuvuta ganja kuanzia saa mbili asubuhi, kwa hasara ya nani kama sio taifa kwa ujumla?. Unaridhika sana unapowaona vijana wenye nguvu za kufanya kazi wakishinda wanazunguka maeneo ya vituo vya mabasi, huku wakitazama mabinti legelege ili wawaibie pochi na simu zao halafu wakimbilie vichochoroni.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuongea kama mwanaharakati fulani, na kuongea kama mtu ambaye anayo majukumu makubwa ya kuleta maisha mazuri kwa nchi yake. Unafika wakati ambapo hatuwezi kuendelea kusikiliza ngonjera nyingi za wanaharakati, ambazo zina faida kwao kwa maana ya ongezeko la pato mifukoni lakini halina faida kwa wengi waliobakia njia panda kutokana na ugumu wa maisha.

JK alipendwa kwa sababu aliwapa uhuru wengi kiasi cha kujikuta akivumilia mpaka matusi na kejeli kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, huyu mwenyeji wa chato simuoni akifuga ujinga, hata kidogo. Nchi ilijisahau, watu wakajisahau. Na kujisahau kubaya zaidi ni kule ambako watu wanataka waendelee kuishi maisha yale yale ya malumbano, wakati maendeleo ya kweli yanaweza kupatikana ndani ya uwezo wetu. Kuna fedha nyingi inaliwa kwa maana ya mishahara hewa, watu wanabuni njia mbalimbali za kupiga fedha ya serikali, this time around imekula kwao, wahesabu maumivu makali.
Jadili hoja! Mmejipangaje nyinyi Kama watawala kutupa MABADILIKO ya Kweli dhidi ya tuhuma Na hoja za Mwanahabari huru?

Unamzungumzia Mbowe as if yupo Ikulu.
 
Jadili hoja! Mmejipangaje nyinyi Kama watawala kutupa MABADILIKO ya Kweli dhidi ya tuhuma Na hoja za Mwanahabari huru?

Unamzungumzia Mbowe as if yupo Ikulu.
Maisha ya tuhuma na hoja hayawezi kukwepeka hata siku moja. Anatoa hoja zake lakini wanaoongoza nchi wanaitazama kazi wanayoifanya katika mtazamo tofauti na ule wa mwanahabari huru. Sidhani kama rais na wasaidizi wake wanao uwezo wa kufanya kazi kadri ya matakwa ya kila mtanzania. Ni lazima wengine watajiona kama vile wanazo akili nyingi sana kwa sababu maoni yao yanafanyiwa kazi na kuna wengine wanabakia kuwa walalamikaji kwani walichonacho moyo hakijapata bahati ya kuwa ndio wazo au mpango wa serikali.
 
Asante kwa upembuzi yakinifu.
 
Back
Top Bottom