Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
"Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani hata masaa 48 wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa".
Rais John Magufuli wakati wa Kiapo cha Wakuu Wa Mikoa
15/03/2016.
Hii kauli mbaya sana inayochochea ukandamizaji wa haki za binadamu imetolewa na kuongeza kasi ya udikteta imetolewa na anayeitwa kiongozi mkuu wa nchi akiruhusu ukiukwaji wa sheria na unyanyasaji wa wanyonge......huyu ni rais Magufuli Joseph.
Huu ni uovu mwingine CCM inaupalilia kutesa na kunyanyasa Watanzania katika taifa lao kuishi utumwani kwa shinikizo la uongozi wa kidikteta unaoratibu masilahi ya makada mafisadi wa ccm.
Kama huyu mtu anania ya kupambana na mafisadi, na kuondoa umasikini Tz mbona toka aingie madarakani;
Hajakamata wahujumu uchumi katika awamu ya pili, tatu na nne?
Mbona hajahoji mikataba ya kifisadi katika awamu ya pili, tatu na nne?
Mbona hajaongelea kukubali maoni ya wananchi ya rasimu ya katiba ya Tume iliyoongozwa na Warioba?
Mbona hajaonesha nia ya kuhoji utajili wa viongozi wa ccm na wafanyabiashara makada wa ccm?
Mbona hahoji na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wafanyabiashara wa mihadarati na kujulisha umma?
Mbona uchumi unazidi kuyumba....Benki Kuu inadorora na hakuna hatua yoyote inayochukuluwa?.....shilingi inaporomoka kila kukicha na hadi sasa hakuna utaratibu unaofanyika kulinda na kukuza uchumi wa Tanzania?
Mbona hajachukua hatua dhidi ya "dolarization" shilingi haitumiki bali dola na euro ndizo pesa zinazotumika nchini?
Haya yote yanayofanyika kuwa kuna kasi ya utendaji ni sarakasi zisizo na mpagilio zilizojaa fujo na uparaganyishaji wa idara mbalimbali bila kubadilisha chochote maana mifumo ni mibovu sana hivyo hakuna jipya linalotarajiwa wala hakuna kitakachofanyika kumpa raia wa chini unafuu wa maisha.
Wananchi wengi hawana ardhi, mitaji hakuna, benki za kigeni zinafyonza uchumi wa nchi yetu na riba ziko juu sana.
Wananchi wengi ni watazamaji ktk uchumi wa nchi yetu ila wamiliki wa biashara na viwanda asilimia kubwa ni wageni....hili halijaguswa na haligusiwi na hawa waimba kasi ilihali ni speed za mbayuwayu zisizo na mwelekeo maalumu na hazijabeba lolote la maana linalomgusa mwananchi wa kawaida.
Hapa tunategemea:
Umasikini unaendelea kutesa watanzania na kuendeleza gap la wasionacho na walionacho kuwa kubwa maana hakuna jipya kati ya awamu ya nne na ya tano.....uozo ule ule, timu mbovu ile ile ndiyo imepangwa kucheza mpira na katika uwanja ule ule.....hili ni janga kwa wananchi makabwela wasio na kimbilio.
Majanga ya kijamii kama wizi, ukahaba na utupaji wa watoto yataongezeka kwasababu watu wanaendelea kukosa mwelekeo kwa kulishwa maneno na vitisho utadhani tuko utumwani/kwenye koloni la CCM.
WAKUU WAPYA WA MIKOA.
Niliwahi kusema haya kuwa kamwe haitatokea CCM kufanya mabadiLiko yenye tija kwa wananchi wanyonge.
Ni zaidi ni ukosefu wa ufahamu kutegemea zimwi CCM lililozoea kula vya kunyonga na kubaka demokrasia kuratibu mabadiliko ya kumnufaisha mwananchi mnyonge.
UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA....NI JIPU
Mkumbuke kwa utaratibu wa CCM Rais anatakiwa kuwa M/kiti wa CCM.
Hivyo Mkuu wa nchi wa vikosi vya ulinzi na usalama anakuwa M/kiti wa CCM....hilo ni kosa na huondoa uwezekano wa uwepo wa utawala bora.
Ndio maana Magu anateua makada wa CCM kushika nafasi za kiserikali na kuagiza vyombo vifanye kazi ya kuilinda CCM kwa kisingizio cha kutuliza gasia.
Katika ilani ya UKAWA ilianisha wazi kupunguza ukubwa wa serikali. Mojawapo ya mbinu za kupunguza ukubwa wa serikali ni kuondoa nafasi za uongozi zisizo na tija.
Mathalani....mfumo wa uongozi wa mkoa utakuta viongozi wafuatao:
-Mkuu wa Mkoa
-Katibu Tawala Mkoa
-RPC
-Mayor wa Jiji baadhi ya mikoa
Hawa wote ni viongozi wakuu wa mkoa na wanalipwa mishahara, marupurupu, usafiri, makazi, bima kwao na familia zao, fedha za uhamisho n.k
Huu ni mzigo mkubwa sana unaobebeshwa wananchi wanyonge walipa kodi wanaoteswa kwa umasikini ilihali serikali ya ccm inatengeneza nafasi za viongozi wasio na kazi ya wananchi bali wanawekwa kulinda masirahi ya CCM na mafisadi waliojaa chama hicho.
UDHAIFU WA UTEUZI.
Katika uteuzi huo mbali na kuwa hauungwi mkono na wanamabadiliko mbaya zaidi unamadhaifu mengi sana.
1. Uteuzi wa wazee wastaafu.
Asilimia kubwa ya wateule wa ukuu ni wastaafu waliokwishatumika kwanini wasipewe vijana wenye fikra mpya, ubunifu wa kisasa na mbinu mpya za kupambana na umasikini?
2. CV zao zinatia shaka
Hawa wakuu wa mikoa huteuliwa kwa misingi ya ukada wa CCM na uswahiba kati ya mteua na mteuliwa.
Kuna wanajeshi na makada wastaafu wanaopewa ukuu wa mkoa ilihali hata elimu ya kidato cha sita hawana.
Mara nyingi unakuta hawana elimu ya uongozi na menejimenti kabisa.
Hawa wanaperekwa kuwa maboss wa wataalamu wote ktk mkoa....hili ni tatizo kubwa sana.
3. Ukuu wa mkoa ni ufalme wa kumalizia maisha
Hii haipingiki maana mkuu wa mkoa hana majukumu bali ni mtoa matamko na kuzindua matamasha na kuwakirisha ccm ktk serikali. Hii ni hujuma kwa wananchi masikini na vyama vya upinzani.
4. Uteuzi wa waliokosa ubunge
Hii ni dharau kwa wananchi na kukanyaga demokrasia.
Mtu amethibitishwa na wananchi kuwa hafai kuwa kiongozi ila rais anamteuwa kuwa mkuu wa mkoa.
Mtu ameshindwa kudeliver na wananchi wakaona ni mzigo rais anaubeba huo mzigo na kuutwisha wananchi. Wajinga wanashangilia tu lakini nchi yetu itaendelea kuwa masikini kuendelea kuwa na viongozi hovyo.
5. Mfumo hovyo wa uwajibishaji wa Mkuu wa Mkoa
Hawa huishi kama wafalme katika mkoa na hakuna wa wakuwajibisha, hakuna wa kuwapangia kazi, hakuna wanaporipoti na hakuna anayewakagua.
Hawa huishi peponi tu kufuja mali na kuvuna utajili, kulipwa kwa historia ya ukada na fadhila kwa aliyemteua.
6. Uteuzi wa Viongozi wa Kijeshi kuwa viongozi wa kisiasa.
Hii ni hatari kubwa dhidi ya ustawi wa demokrasia.
Viongozi wa polisi na JWTZ hushawishika kujipendekeza viongozi wa ccm ili wakiistafu wapewe fadhila ya ulaji ktk ukuu wa mkoa.
Hii ni mbaya maana hawezi kutenda haki dhidi ya vyama vya siasa vinavyotetea masirahi ya umma kupata viongozi bora.
Kwa utaratibu huu kikundi kidogo kinaungana kuratibu ulaji wa wachache na kuweka rehani maendeleo ya wananchi ilimradi wakuu wa ccm na wanamtandao wameridhishwa kuendelea kuiweka ccm madarakani.
7. Ni viongozi wa ccm na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa utaratibu huu Wakuu wa Mikoa hulinda masirahi ya ccm kwa nguvu na mbinu zote kandamizi.
Jambo hili huunganisha serikali na ccm na vyombo vya ulinzi na usama kuwa kitu kimoja sawa na timu ya Simba. Hili ndilo chimbuko la uongozi mbovu na umasikini nchi yetu.
Takukuru na polisi hupewa amri na makada wa polisi kwa sababu bosi wao ni kiongozi wa CCM na hujikuta wako katika shinikizo la kutumika kisiasa kulinda ajira zao.
Hapa ndipo fedha za umma hutumika kwa masilahi ya CCM, mishahara na posho wakidai wanalinda usalama wa umma kumbe ni usalama wa ccm.
Hivyo basi tusitegemee kupata mabadiliko kupitia CCM. CCM na viongozi wake wapo kutetea kikundi cha watu wachache.
Huyu Magufuli hawezi kufuta mwenge, wakuu wa wilaya na vyeo vingine vyenye masilahi ya CCM ila mzigo kwa wananchi kwasababu huwezi kutenganisha kiwiliwili na kichwa....CCM imesuka mfumo wa kutawala sio kuongoza...tena kutawala kidikteta.
Nchi inakuwa na kundi kubwa la viongozi wanaofuja fedha za umma ila hakuna jipya lolote wafanyalo kukwamua umasikini wa Watanzania.
Ni CCM na viongozi wake wote ni majipu maana ndio wameasisi huu mfumo mbovu uliokwamisha maendeleo ya nchi yetu.
Huyu Magufuli ameweka hapo kulinda huo mfumo uliomweka hapo. Hivyo kutegemea CCM kuondoa umasikini ni ndoto za alinacha.
Na;
Solomon M. Kambarangwe
15/03/2016

- Kuendelea kuona vifo vingi vya akina mama na watoto,
- Ukosefu wa elimu bora na ujinga kuongezeka,
- Ukosefu wa ajira kuendelea kuwa mkubwa sana.
- Utapiamulo (malnutrition) kuendelea kuwa janga na kudumaza akili na afya za Watanzania.