Kutapika safarini

bakundande jr

JF-Expert Member
Oct 22, 2021
507
670
Habari za mda tena ...
Hili swala la mtu kutapika akiwa safarini huwa linatokana na nini??? ...
Ni ushamba wa Safari au ni ugonjwa na mtu mwenye shida Kama hii anawezaje kuondokana nayo,,,,
Kwa anaejua tafadhali

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni kawaida kama hujazoea safari za masafa marefu au mchafuko wa hali ya hewa kwa mfano ukienda zanzibar ule mtikisiko wake kama hujazoea lazima utapike maana tumbo linajaa gas kingine ni tabia ya kula kula kila aina ya vyakula likipita indi dirishani unakula biscuit unakula gari ikisimama unanua chips, soda,mikate, sambusa, vitumbua kama unaenda safari ya siku mbili unavyofakamka vyakula hapo lazima tumbo litengeneze gas likijaa gas shughuli imeisha hapo kinachofuata ni msiba.
 
Siku moja kabla ya safari epuka kula hovyo.

Siku ya safari epuka kula au ikibidi kula kula vyakula vikavu kama vile clips za viazi au mihogo, biscuits, cakes n.k

Epuka kunywa vimininika.

Hayo machache.
 
Habari za mda tena ...
Hili swala la mtu kutapika akiwa safarini huwa linatokana na nini??? ...
Ni ushamba wa Safari au ni ugonjwa na mtu mwenye shida Kama hii anawezaje kuondokana nayo,,,,
Kwa anaejua tafadhali

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Iliwahi nitokea those days nikaambiwa niwe nanunua gazeti alafu nalikalia niwapo safarini, hakika sikuwahi tapika tena kila nifanyapo hivyo.

NB.Sijui kuna mechanism gani na pia bado nafanyaga hivyo.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom