Kutapeliwa

Hilo ninakubaliana mkuu, kwa wenye tamaa za ovyo ovyo hilo lipo, lakini mwanamke halizwi mara mbili na wana nguvu kubwa kwenye kutafakari kwa kina.

Hakuna kitu naskia Raha Kama mwanaume kuielezea akili ya mwanamke! Hakika watujua vyema!πŸ’ͺπŸ‘πŸ€›πŸ€œπŸ€πŸ‘ŒβœŒοΈ
 
MREJESHO.
Nashukuruni nyote mlonisaidia kwa mawazo na michango, ishu inaelekea kukamilika about 70%.

MPANGO WA KUFATILIA
Ilikua hivi last week tarehe flani nliamua nianze kuifatilia hii ishu, maana kipindi chote iko nlkua sifatilii wala sikuwahi kumpigia tena jamaa.

Sasa hyo tarehe nlienda kituoni nikaandikisha maelezo vizuri tu, wakaniomba nijaribu kuelezea description ya jamaa alivo nikawaambia vyote nnavovikumbuka kuhusu expression yake. Color, urefu, mwili..nk. Maana walinambia cases kama hizo za kutapeliwa kwa dzain hiyo zishafikishwa kama tatu kituoni pale na watuhumiwa hao wa utapeli namba zao wako nazo polisi pale, kwa hiyo mimi nlichotakiwa ni kuleta namba ya yule jamaa nlomkabidhi mashine ili nijaribu kulinganisha ni ipi kati ya namba zile.
Kwa kua siku hiyo sikutoka na namba ya jamaa ilibidi siku ya pili yake niende niwapelekee hyo namba. Bahati mbaya yule anaehusika na hizo namba hakuepo, nikasema sawa.

KUFIKA KITUONI
Sasa juzi jumatatu nikasema ngoja niende niwapelekee namba maana nilikua nishachonga na afande mmoja hivi aakanambia huyo jamaa anaehusika na hizo namba za matapeli leo atakuwepo. Basi nimefika pale nikaambiwa jamaa bado hajafika na atachelewa kuja kwa hiyo cha kufanya ni either niondoke nirudi baadae au nimsubirie. Basi nikajikaza nikasema nitamsubiri.

USO KWA USO NA TAPELI
Ikapita kama nusu saa hivi kuna jamaa alifika pale nlipokuepo ila sikua nimemuona alivoingia, basi me nikawa naendelea kufanya mambo yangu huku nimeangalia upande mwingine maana sikumtilia maanani. Kidogo akanambia kaka vp (alijua ni askari pale) nikamwambia fresh tu, nlvomuangalia hivi sura kumbe ndie yule jamaa aloagizwa kuja kuchukua ule mzigo, basi na yeye akawa amenikumbuka pale pale, akawa anarudi nyuma ili ajiandae kukimbia..amepiga hatua kama tatu hivi nikamshika mkono (maana kwa mwili wake mdogo asingewezea kunichoropoka) basi nikatembea nae hadi kwa afande mmoja pale nikamwambia ishu ilivokua, akabaki anafurahia mwenyewe.

Basi maaskari wakamuhoji pale akakubali kua mashine aliichukua, ila alivoichukua alimpelekea yule mshkaji wake alomtuma aje aichukue (yule ambae alinitafuta tufanye biashara).

Basi chap tukachukua gari hadi jamaa anapokaa (maana tulienda nae uyo tapeli), kufika tukamkuta jamaa. Ila mshkaji akagoma kwamba yule dogo hakumpa mashine. Ikabidi tumchukue pale twende nae kituoni. Wakaendelea kumueka virungu huko ila bado hakukubali. Basi ikabidi wamuweke lock up. Ikawa usiku umeingia nikaondoka.

Leo nimeongea na dada yake(alichukua namba yangu jana) akasema aliweza kuongea nae na akakubali kua mashine aliichukua, ila aliiuza na hamkumbuki aliemuuzia ni nani. Ko akanambia hapo itabidi wapambane wanipe tu hyo hela au waninunulie mashine ingine.

Mimi kama mimi sitaki kesi, ninachohitaji tu ni jamaa anilipe hela yangu au mashine tu basi mambo yaishe. Lakini sitaki apate dhamana, itabidi ndugu zake wapambane mpaka waipate hyo hela...then wakishaipata yote ndo mambo mengine ya kuachiliwa yafuate.

Asanteni sana kwa ushauri wenu na critiques, na matusi (kwa wachache wale). Naamini tutaendelea kua familia. Nakaribisha maswali, maoni na hoja.

"I rest my case"
 
Pole sana mkuu. Ukisimamia hili vizuri utamkamata huyo tapeli. Kwanza kama sio meseji ya nmb itakuwa na namba ya mtu binafsi pale mwisho wa hiyo msg.

Jaribu kuweka hela kwenye hiyo namba iliyokutumia msg. Pata jina la mpokeaji. Nenda polisi umchukulie RB huyo mwenye hiyo namba. Huyo ndiye atakaye kulipa hela yako. Fatilia, nadhani kuna kitengo cha polisi maalum cha wizi wa kupitia simu -sina uhakika- sasa hivi simu zote zimesajiliwa kwa alama ya vidole. Mwenye simu atapatikana. ata kama ametupa laini mtandao unaweza kutoa namba za watu wa karibu waliokuwa wanawasiliana na hiyo namba yake. Hawa wakibanwa watamtaja.
Mwenye kusajili hiyo laini ndiye atakaekulipa hela sababu alimsajilia mwizi laini, kumaanisha anamfahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…