chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Mwalimu wa shule ya msingi Busekwa wilaya ya Magu mkoani Mwanza Renatus Mkama anadaiwa kuwabebesha mimba wanafunzi wanne wa shule hiyo kitendo na kuwatelekeza kilichopelekea wanakijiji kutaka kumchomea nyumba mwalimu huyo,
Wanafunzi wa shule hiyo wanadai mwalimu huyo huwaita nyumbani kwake kwenda kumuoshea vyombo kisha ndio huwamalizia hukohuko
Mmoja wa wanafunzi waliobebeshwa mimba na kushindwa kuendelea na masomo licha ya kufaulu darasa la saba ni Mariam Bahati ambaye amezalishwa watoto wawili na kuachwa na anadai hakuwa na maamuzi kipindi hicho
Mwalimu huyo alipohojiwa anadai hizo ni tuhuma tu, Mkuu wa shule hiyo anatuhumiwa kumlinda mwalimu huyo kwa kuondoa majina ya wanafunzi hao katika daftari la mahudhurio kuficha ushahidi na amekiri mwalimu huyo kuwa na tabia hiyo lakini yeye aliidhibiti kwa kumlazimisha kuoa