Kutaja mali za viongozi, mwisho 31 Disemba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutaja mali za viongozi, mwisho 31 Disemba!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaitaba, Dec 30, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wakati viongozi wa Tanzania (Mawaziri nk) 23% wametaja mali zao na 77% sawa 7,000. wamegoma kutaja, siku zinazidi kuyoyoma na mwisho ni tarehe 31/12/2009

  Swali ni je hawa 7,000 wasipotaja watafukuzwa kazi? na wakifukuzwa serikali inao uwezo wa kuajili idadi kubwa hii?

  Ni kwanini hawajataja wakati sheria inasema ukiajiliwa, unatakiwa kutaja ndani ya siku 30?
   
 2. TingTing

  TingTing Member

  #2
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ni uzembe tu wa uongozi na viongozi husika. Hakuna mtu, idara, shirika wala mahakama yeyote wa kuwauliza mbona wamekiuka sheria hiyo. Wagomaji ujue wamepata mali kwa njia zisizo halali. Pia Serikali ifungie macho tu suala hili kwani kuna watanzania wengi tu ambao wanavyeti vyao na wamekaa nje wanahangaika kutafuta kazi. Ingawaji cheti inaweza kikawa si uwezo wa mtu ila kuwaweka wao kutasaidia hata kubadilisha mambo mengi yakiwemo hata huduma katika idara mbali mbali. Ukweli ni kuwa serikali haiwezi kuwafukuza maana wao wenyewe kuwajibika ZERO.
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280

  Wao ndiyo serikali yenyewe. Sasa watajifukuza wenyewe. Wanajua wanalolifanya usifikiri ni uzembe, ni maksudi!!
   
 4. I

  Irizar JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wamtaje nani wakati woteeeeee wezi watupuu,wezi watupu, wezi watupuuuuuuuu............
  Nani amfunge nani they are all the same sh....i....t..
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hamna kitu hapa. Wataje ili iweje?

  Amandla......
   
 6. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nafikiri kwa janja ya serekali na kuwaogopa hao viongozi wengine watawazidishia (kusogeza mblele)siku za kutaja mali zao ili wamiliki mizengwe ya kubuni jinsi yakutaja.
   
 7. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katika hili serikali haipaswi kutoa tamko kweli?, au tusubili hiyo kesho tuone itakuwaje
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  hawawezi kufukuzwa.............kwa kuwa ni waheshimiwa,hata wakitaja hawataji mijumba na account zao za nje ili kujua theier actual worth.........hivyo hii ni9n danganya toto ili tuone kama kuna utawala bora na utawala wa sheria wakati miaka nenda rudi ni vilevile .......bora ichukuliwe kuwa hata waliotaja hatujui mali zao kwani hawataji mali zote......................kama sivyo kwa kuwa siasa ni uongo na mwanasiasa akisema mambo 10 basi manane sawa na 67% ni uongo basi tuchukue thamani ya mali walizo taja alafu tuzidishe kwa 1.67% ndipo tutakuwa tumecover ule uongo wa kawaida kwas mwanasiasa
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Danganya toto tu na viini macho. Hakuna hatua yoyote ya maana itachukuliwa. Yaani washindwe kuwachukulia hatua mafisadi wenye evidence eti leo hii wanataka watu wa-declare mali hata zile walizoandika majina ya binamus and wapwaaz?? Tanzania usanii ni mwingi.
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  kupotezeana muda tu..........wanajaribu kuficha mada muhimu ili tuone kama viongozi wanataja mali wakati hawajui hata mali za mafisadi................yaani mnataka jk atoke huko akamwambie ROSTAM AU LOWASA atangaze mali zake na asipotangaza atachukuliwa hatua thubutuuuuu................hawa na wengine kama hao wengi wapo juu ya sheria na juu ya kikwete..............
   
 11. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  hivi watanzania mlitegemea hawa watu wataje mali zao na jinsi walivyopata? msahau kabisa! kwa maana kamwe haiwezekani hata siku moja, labda mjerumani arudi walau kwa miaka miwili tu. Kiongozi yupi anayeweza kufuatilia hili, ikiwa 80% ya matamko ya serikali yetu ni uongo. Ina maana kati ya viongozi wetu 80% ni waongo, na kwa kila mmoja kati ya waliobaki, kwa 80% ni mwongo.....

  Lakini hawa viongozi hawana kasoro hata kidogo, bali miongoni mwetu, wengi ndio wajinga, maana wanaingia huko (madarakani) kwa kura zetu.

  Kudanganywa mara ya kwanza sio ujinga, lakini kudanganywa mara ya pili, tatu, nne... ni kielelezo dhabiti cha ujinga.

  Mwaka 1995, 2000, 2005, 2010... bila utekelezaji ni ujinga!
   
 12. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mafisadi tu hawa wanaonyesha usanii tu maana hao wasiotaja mali zao hawatafanywa lolote. UPUUZI MTUPU!
   
 13. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mbona kelele ni nyingi huko Tanganyika, lakini kwenye uchaguzi munachagua chama hicho hicho?Au kuna kipi ambacho sijafahamu, kiongozi kama munaona hamumtaki munaweka utawala mwengine wa upinzani.

  Hawa jamaa ni wizi, na wala sifikirii kama tunaweza kumuuliza mwizi unaiba vipi?Tukategemea ataeleza mbinu zake zote!

  Kelele kibao za ufisadi, lakini CCM inashinda kwa kishindo 80%...kunani?
   
 14. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huu ni usanii mwingine ambao hauna maana yoyote. Hivi kweli katika hali kama hii ambapo ufisadi umeota mizizi nchini kuna maana yoyote ya kutaka viongozi wataje mali zao ambazo wamezipata kwa njia zisizo halali ama kwa kukiuka maadili ya uongozi kwa kutumia vyeo vyao kujipatia hizo mali?
   
 15. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kutaja mali zao: changa la macho na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa!!.

  Akina chenge walitaja, baada ya muda wanatuambia hivyo vijisenti!! Changa changa la macho!
   
Loading...