Kutafuta utajiri

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
39,596
Reaction score
61,016
Kila mmoja anapenda kuwa tajiri, na hii inatokana na faida nyingi uzipatazo pale unapokuwa tajiri. Na unapozungumzia utajiri, unazungumzia kumiliki rasilimali fedha, watu, majengo, mashamba, mifugo n.k

Utajiri hupatikana kwa kufanya vitendo na si kwa kuongea tu. Wengi tunaongea ongea tu, ndio maana hatutajiriki.

Utajiri ni matokeo ya ‘kitendo fulani’ kufanyika, hicho kitendo kinaweza kuwa; ubunifu wa bidhaa, ubunifu wa soko, utapeli, rushwa, wizi wa kimazingara, biashara isiyo sahihi (haramu), unafiki, uongo n.k

Ili wewe uwe tajiri inakubidi ufanye ‘kitendo fulani’, na hicho kitendo fulani ndio kitakachokuingizia fedha wewe.

Aya, kazi kwenu matajiri watarajiwa; tafuta hicho ‘kitendo fulani’​
 
Ghafla paa, inatakiwa milioni 100 ukatibiwe India, utafanyaje?

Nina mashamba ya urithi... yapo sehemu potential sana !!! Ni swala la kugusa tu , any way homa huwa zipo tu unaweza kwenda India alafu ukarudi kwenye sehemu ya cargo, upo kwenye lisanduku lilipopigwa tape za kutosha !!!!!!!

Kama siku yako ikifika imefika tu ! Death is a natural thing !!!!

Kina magufuli, mengi, nyerere, mkapa n.k walikuwa na uwezo na walifukiwa chini ya ardhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…