Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 15,654
- 25,826
Habari za muda huu wabunge wenzangu wa bunge tukufu la MMU, ningependa tushirikiane hii kitu hapa......
Wengi wetu tuko katika mahusiano ya kudumu na yasiyo ya kudumu na tumekutana na changamoto nyingi ambazo zingine zimetukatisha tamaa mpaka kusitisha mahusiano zingine tunaendelea kupambana nazo.
Naomba tuiongelee hii changamoto ambayo mara nyingi imekuwa tatizo naomba tu kuuliza swali je kususa/kununa ni suluhisho la tatizo katika mahusiano? na hili lipo sana kwa wanawake japo hata wanaume huwa wanasusa,unaweza ukamkwaza mwenzako kwa kujua ama kutokujua anakununia siku nzima wengine wanaenda mbali hata wiki nzima hawaongei ndani kama ni baba kanuna basi hata pesa ya matumizi atapewa house girl au mtoto ambaye yupo au isitoke kabisa sasa hapo unamkomoa nani? mwanamke hata ile tamu ya baba anashindwa kutoa kwa kuwa amekwazwa na mume au mchumba wake........mifano ipo hata humu humu watu wanaleta matatizo eti mpenzi wangu kaninunia siku ya nne je hapo tunakuwa tunajenga au tunabomoa?
Endapo mwanamke atasusa hata mchezo akashindwa kutoa lazima atasaidiwa na wengine wanaosema mume wa mtu mtamu ila mke wa mtu ni sumu, na wengi wao wakinuna majibu yao yanakuwa ya mkato au anafanya kimya kimya hata bila kuongea,jamani njia nzuri ya kupunguza machungu ni pamoja na kuyasema kwamba bwana kwakweli umenikwaza hapa na hapa ili ajirekebishe au hata kuomba msamaha kununa/kususa si njia nzuri ya kupuguza migogoro bali inaongeza ukubwa wa tatizo,ukinuna na ukabembelezwa basi bembelezeka na useme dukuduku lako na mambo yataenda hii ni njia nzuri ya kupunguza migogoro midogo midogo

*****************************