Christiba
Member
- May 27, 2020
- 24
- 32
SAFARI YA MAISHA NA LENGO LA MIILI YETU.
Safari ya maisha yako imejengwa kwenye sehemu kuu mbili; maisha ya kiroho yasionekana kwa macho na maisha ya kimwili ambayo uhisiwa na milango ya fahamu. Maisha ya kiroho ni safari ya yakuutambua utu wako halisi na kutambua wewe ni nani hasa( true self/ being).Maisha ya kimwili ni safari ya matarajio ya kuwa na hadhi, nafasi au nguvu fulani katika jamii inayokuzunguka(future).
Maisha ya kiroho ambayo ndio ya utu wetu halisi hujengwa nje ya misingi ya muda na nafasi (Time and space) ila maisha yetu ya kimwili hujengwa ndani ya misingi muda na nafasi, ndio maana miili yetu huathiriwa na wakati ( huzeeka) na vilevile huchukua nafasi fulani kwa kudhihilika katika mazingira. Safari hizi mbili zipo ndani ya maisha ya binadamu mmoja hivyo binadamu hutakiwa kuishi katika umoja wa safari hizo bila kuwekeza kwenye safari moja tu. kuufikia utu wako halisi wa kiroho huleta amani ya ndani vilevile na hutusaidia kufikia matarajio yako ya kimwili, kuishi maisha ya matarajio tu bila kuufikia utu wako halisi huleta maangaiko, shida na kutokuridhika.
Malengo ya kuufikia utu wako wa ndani au utu wako halisi( your being) ni kufikia kiwango cha juu kabisa cha utimilifu wako na kuwa na umoja kamili na utu ambao hauathiriwi na muda wala nafasi. Malengo ya maisha ya matarajio tu ni kuuridhisha mwili ambao huathiriwa kirahisi na muda na mazingira husika. Kuishi maisha ya kiroho hutoa uhuru kwa mtu kuishi maisha ya kimwili akiwa anatambua ni sehemu ndogo tu ya maisha yake halisi kwahiyo umuacha mtu na amani, furaha na utimilifu. Kinyume na kuishi maisha ya kimwili ambayo humpa mtu mitihani ya mataraijio ambayo humfunga mtu asijue maisha yake halisi ambayo ndio kusudi kubwa la maisha yake
Kwakuwa maisha ya kiroho yamejengwa nje ya misingi ya wakati wa kifikra ambao sio halisi( wakati uliopita na ujao). Kuishi kwa kuipokea kila hali inayoipitia sasa hivi, katika misingi ya wakati uliopo bila kusumbuka na yaliyopita na yajayo ambayo si maisha kiuhalisia kutakufanya moja kwa moja uishi maisha ya kiroho na kwakuwa hausumbuki na yaliyopita wala yajayo basi kwako kutakuwa na msamaha, upendo na amani, hautopitia kufeli wala msongo wa mawazo ila AMANI. Kuishi katika kupokea hali kama ilivyo kwa muda huo uliopo(being) kuna muunganiko wa moja kwa moja na matarajio ya kimwili, ila ukiishi katika misingi ya kimwili(fikra) inatufanya kujihusisha sana na mambo yaliyopita na yajayo hivyo hufanya tusahau utu wetu halisi ambao tunaupata katika kusudi la maisha halisi ya wakati uliopo(being)
Kuishi kwenye kusudi au kwenye utu hutufanya tusipitie mikanganyiko baina ya safari zetu mbili za kiroho (being/now) na kimwili (past and future). Ila ufanya utu wetu halisi na matarajio yetu ya nje kuwa kitu kimoja, kwa upande mwengine kuwekeza katika maisha ya matarajio pekee hututenga na kusudi letu la maisha halisi ya ndani, maisha ya kiroho kwa kutufanya tuweke mawazo yetu kwenye wakati ujao( nitakuwa nani, nahitaji nini na nitafanya nini) na uliopita ( nilikosea nini n.k).
Ulimwengu umeundwa na nguvu ya uwepo wa uelewa (being) ambao hauonekani, uwepo huo wa uelewa uliingia wenyewe kwenye vitu (maumbo ya kifiziki au linaloshikika/ miili) na lengo la mageuzi ya kuingia kwenye vitu (miili) ni kujidhihilisha( kuweza kuonekana) wenyewe kwenye maumbo ya vitu mbalimbali yanayoonekana. Ili uwepo wa uelewa ujidhihilishe ( uonekane) kutoka kwenye utumwa wa kutoonekana, uelewa huo ukaingia kwenye maumbo na kutengeneza mifumo wa maisha kwenye maumbo hayo(miili). Hivyo ni jukumu la miili kuishi katika kudhihilisha uwepo wa uelewa (roho) katika maisha yanayoonekana.
Kwahiyo lengo la safari yetu ya miili kwenye dunia hii ya kifizikia ni kuboresha uhusiano wa maisha yasionekana (utu/roho) na yanayoonekana (dunia ya nje) kwa lengo la kuyafanya maisha yanayoonekana yadhihilishe utu wetu wa ndani/ roho isiyoonekana. Utu wa ndani ni juu ya fikra zetu zilizoundwa katika misingi ya kuhukumu mema na mabaya, ni juu ya shida na raha za kidunia, ila ni umoja kamili, upendo kamili na amani kamili. Hivyo miili yetu inapaswa kudhilisha tabia hizi za utu wa ndani katika matendo yanayoonekana katika jamii.
🙏🏾🙏🏾🙏🏾