Iruru
JF-Expert Member
- Jan 27, 2014
- 1,470
- 2,864
Haraka sana baada ya kusikia hii habari ya CAG Asad kustaafu, cha kwanza sikushangaa na hii ni kwa sababu ya matukio kadhaa yaliyotokea hapo nyuma kati yake na Bunge/Serikali. Pamoja na mabishano mengi ambayo yamekuwepo ya kisheria miongoni mwa watu juu ya kama Prof. Assad alikuwa na haki ya kuteuliwa kwa kipindi cha pili na hii haki iko kikatiba ama kisheria, mimi likanijia wazo hili: Je, kustaafu uCAG kabla ya umri wake wa kustaafu ni nini implication ya hili kwa Assad binafsi? Je, kuna vimafao kidogo vinataka kuminywa hapa tofauti na kama angestaafu uCAG kwa sababu ya umri? Na je, huku kustaafu kwake, anastaafu uCAG tu au na ile kazi yake ya kufundisha pale Chuo Kikuu?
Kwa tabia za meko, pamoja na kutaka kuendelea kuficha kile ambacho asingependa kifahamike hasa matumizi ya pesa za walipa kodi, anaweza pia kuwa anataka kumuumiza Prof. Assad kama namana ya kulipiza kisasi juu yake.