Kusoma Masters Open University of Tanzania

Rusumo one

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,078
3,607
Wandugu habarini za leo?

Naomba kwa mwenye ideas na Masters of Project Management toka Chuo Kikuu Huria Tanzania, nahitaji kujua upatikanaji wa materials, lecturers na changamoto zilizopo pia nataka nisome through distance learning.

===
Maoni kutoka kwa wadau:
Mkuu stable, nimependa ulivyoeleza kwa mapana kuhusu OUT. Nami pia 2019/20 nataka nianze undergraduate ya BA in Socialogy (BASO), kuna watu wanasema kama ukikomaa na kujicommit unaweza ukasoma kwa miaka 2 tu, na ukawa umepata degree yako. Je, ni kweli?

Pia ningependa unifafanulie kuhusu malipo na gharama mbalimbali hasa wanapotumia neno UNIT katika mgawanyo wa ada maana nimejaribu kupitia Prospectus yao hawajadadavua kiundani. Na vipi kuhusu utaratibu wa field?

Asante kwa kufuatilia mjadala.

Mimi ninasoma Masters, hivyo nadhani kuna utofauti wa katika ada pamoja na mambo mengine, lakini bado nina nafasi ya kukuelezea yale ninayo yafahamu.

1. Ada - Chuo Kikuu Huria tunalipa ada kwa Unit, ninaposema unit maana yake ni Structure/Composition/Uzito wa course husika, Uzito wa course ndio huonyesha unit za ulipaji, mfano kama course ina unit moja na ada yake unit ni tsh 180,000 maana yake ni kuwa somo lenye unit 2 ada yake itakuwa 180,000x2 = 360,000.

Hivyo huku tunalipa ada kwa course unazochukua kwa kipindi husika cha masomo, na kwa uzoefu wangu mara nyingi course za undergraduate huwa zina mchanganyiko wa unit kuna ambazo zina units 1 na ambazo zina units 2, na mara nyingi course zenye unit 2 zinakuwaga ngumu na hubeba dhamana kubwa katika matokeo yako. hivyo ni vyema unaposoma uwe mwangalifu wa course zenye unit 2.

2. Kuhusu muda wa kumaliza degree - Mkuu nadhani hili nashindwa kulijibia kwakuwa mimi ninasoma Masters, lakini kwa ufahamu wangu ni kuwa kiwango cha chini kabisa kilichowekwa na mamlaka ya elimu tanzania kuhusu kupata degree ni miaka 3, hivyo sidhani kama kuna uwezekano wa kupata Degree chini ya miaka mitatu.

Nami pia nilikuwa ninadhani kama hii, ya kufanya Masters ndani ya mwaka mmoja, lakini imeshindikana sabab chuo kina sisitiza kila course lazima isomwe kwa miezi isiyopungua mitatu. so hata ufanyeje ni lazima uwe ndani ya kipindi kilichowekwa na chuo ili kukidhi ile dhana ya muda uliyowekwa kwa ajili ya Degree au Masters au Phd.

Lakini pia kumbuka huwezi kusoma tu kisha ugraduate, ndio mana kuna mitihani ambayo hupangwa kwa muda husika, hivyo sio speed yako ya usomaji itakufanya kuwa na nafasi ya komba mtihani muda wowote unapojiona uko tayari kwa ajili ya mtihani, waalimu wanahitaji kujipanga kisha kuandaa mitihani kwa muda/semista husika.

Pia hata kama umepata nafasi ya kumemaliza course work ndani ya miaka miwili, utalazimika kusubiri miaka miatatu ipite ndio ugraduate, maana yake utakaa pending mwaka mmoja kusubiri miaka mitatu itimie

3.Utaratibu wa Field - Kama nilivyosema,awali, mimi ninasoma masters, lakini bado ninatambua kuwa Chuo kina muhula kama ilivyo kwa vyuo vingine, hivyo utaratibu wa mafunzo kwa vitendo upo kama kawaida na wanafunzi huomba katika taasisi mbali mbali ili kufanya mazoezi kwa vitendo, hii pia inategemea na course unayosomea, kuna wengine hufanya mazoezi wakiwa mwaka wa kwanza, wengine mwaka wa pili na wengine hufanya mwaka wa tatu. na mazoezi haya ya vitendo unaweza fanya katika ofisi unayofanyia kazi au sehemu yoyote ambapo unaona itafaa kwa ajili ya kutimiza matakwa ya mazoezi ya vitendo na kupata recommendation toka kwa supervisor wako.

Mwisho. mfumo wanaotumia chuo kikuu huria ni mfumo unaotumika sana katika vyuo vingi vya nje, na jambo linalofurahisha zaidi ni aina ya delivery ya materials inayotumiwa na waalimu wa OUT, kwakweli ina motivate hata mtu kusoma kwa bidii, walimu wanasisitiza mwanafunzi kuelewa na sio kukariri, na ndio mana assignment pamoja na mazoezi mbalimbali huwekwa katika platform inayoitwa MOODLE (Modular Object-Oriented Dynamic Learning Environment), yaani kwa namna yoyote mwalimu lazima atajua kama umecopy na kupaste sababu wana software ambazo zimeshakuwa attached to moodle ambazo zinadetect mambo hayo.

stable, Ahsante kwa majibu ambayo nami yamenisaidia, tafadhali unaweza tujulisha muda wa application wa course hii, na pia gharama zake, maana nilisikia Open ada unalipia per course!

Ni kweli tunalipa kwa Course/Unit:

1. Gharama.

MPM (Masters of Project Management) ina Course 8, ambazo 6 ni Core alafu 2 ni Elective. Na kila course unit kwa mwaka 2017/18 tulilipia Tsh 220,000 lakini sasa hivi wamepunguza gharama hizo na kuwa Tsh 180,000 per unit.

Kwahiyo, gharama ya course moja yenye unit 2 ilikuwa ni Tsh 220,000 x 2 = 440,000 alafu Dissertation ilikuwa na unit 6, ambapo ni 6 x 220,000 =1,320,000. Hivyo jumla ya gharama kwa tuition fees tu ni (440,000 x course 8) + (Dissertation Unit 6 x 220,000) = 3,520,000 +1,320,000 = Total 4,840,000.

Kwa hesabu hiyo, badilisha kwenye 220,000 uweke 180,000 ambayo ndio bei ya sasa. (360,000 x 8) + (6 x 180,000)
2,880,000 + 1,080,000 = Total 3,960,000. Hivyo Tsh 3,960,000 kwa bei ya sasa ndio gharama ya Course work plus Dissertation.

Kuna michango mingine ya chuo ambayo kwa sasa sitaweza ikumbuka, lakini nashauri uende katika Website ya chuo utaikuta imeorodheshwa.

2. Muda wa Application

Mkuu nadhani kama sijakosea, Open University kwa mwaka wana enroll mara 2 (nakubali kusahihishwa) hivyo muda wa application inategemea na wewe ungependa kuapply mwezi gani, maana kuna June, then December. Nikiri kuwa katika sehem hii sina ufahamu mzuri, ila nikushauri utembelee Regional centre yako, au kupitia website yao kuna namba za help desk, unaweza wapigia watakufahamisha mengi juu ya Usajili wa wanafunzi wapya.

Karibu

Mkuu, nadhani wenye negative mind ni kukosa ufahamu wa yale yanayoendelea katika chuo hiki. Kikubwa ni wewe kuelewa nini kumekupeleka hapo, maana masomo ni yale yale, sasa kwa kuwa tuna mazoea ya kufundishwa darasani, mtu anapokuwa anajisomea peke yake or online, ni kama anaonekana hasomi.

Na kwa taarifa tu ni kuwa, unapokuwa na mazoea ya kujisomea vitabu bila kungojea mwalimu kuja kukufundisha, inakujengea uwezo wa kusoma vitabu vingi na hivyo kuwa na uelewa wa masuala kadhaa yanayoendelea katika dunia yetu, maana mambo mengi yapo katika maandishi.

Unavyosikia Watanzania tu wavivu wa kusoma vitabu, elewa moja ya vyanzo vya tatizo hili na mazoea ya kutafuniwa, then unameza tu. Hivyo Open ina ujenga kuwa na uwezo wa kujisomea vitabu vingi kisha kudigest kile ulichokusoma.

Asante.
 
Karibu.

Pia nami ninasoma course hii, nathubutu kusema ni course nzuri sana, na kuna waalimu wazuri,

1. Kuhusu upatikanaji wa materials lectures
Kuna platform inaitwa moodle. Hii platform inatumika kama interface kati ya wanafunzi na waalimu. Ndani ya moodle kuna mambo mengi sana ikiwemo materials na vitabu mbalimbali (kiufupi hii ni sehemu ambayo) hufanyika mijadala (discussion mbalimbali za masomo pamoja na mambo mengine muhimu yahusuyo course.

Waalimu hutumia sehemu hii kuweka materials mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitabu, video za elimu, majarida, na sources za materials mbalimbali hivyo suala la materials sio tatizo kabisa, kila kitu kipo ni wewe tu ushindwe.

2. Changamoto
Kimsingi unapotaka kusoma Postgraduate kupitia Open university, ni vyema ukajitathmini kwanza uwezo wako (Upstair) lakini pia muda wako (Personal time Management). Course hii ina mambo mengi sana hivyo unahitaji muda mwingi wa kujisomea pamoja na kufanya discussion kama una wenzako.

Pia katika course hii kuna masomo kama Project Finance pamoja na Quantitative Techniques for Project Management yana hesabu (Calculation) hivyo kama hauna background ya finance au hesabu kwa ujumla, masomo haya yatakusumbua japo ukikomaa lazima ufaulu.

Kuhusu muda wa masomo ni kuwa, Open University tunasoma kwa Tri-mester (related to semester) maana yake ni kuwa kwa sisi watu wa project tuna jumla ya course 9, hivyo kila Tri-mester moja unatakiwa kusoma masomo 3 tu, kwahiyo utaona kuwa ndani ya miezi 18, kila tri-mester inakuwa na miezi sita kisha unafanya mtihani wa final wa masomo matatu iliyochagua kusoma kwa tri-mester moja.

Kama una jambo lingine unaweza uliza, nitakusaidia.
 
Nasikia una uhuru wa kuchagua idadi ya masomo na aina ya masomo ya kusoma kwa semester.
 
C
Kweli kwa usomaji huo sidhani kama utamaliza hapo ukiwa competent graduate

Unazungumzia competency? Open University? Competency ya mtu inapimwaje? Tusaidie ili tujaribu kulinganisha mtu anayesoma kwa kujitafutia resources na mtu anayekaririshwa darasani.nPia competency ya mtu mara nyingi hutegemea na mtu mwenyewe awe Open, UDSM au etc
 
Mkuu stable, nimependa ulivyoeleza kwa mapana kuhusu OUT. Nami pia 2019/20 nataka nianze undergraduate ya BA in Socialogy (BASO), kuna watu wanasema kama ukikomaa na kujicommit unaweza ukasoma kwa miaka 2 tu, na ukawa umepata degree yako. Je, ni kweli?

Pia ningependa unifafanulie kuhusu malipo na gharama mbalimbali hasa wanapotumia neno UNIT katika mgawanyo wa ada maana nimejaribu kupitia Prospectus yao hawajadadavua kiundani. Na vipi kuhusu utaratibu wa field?
 
Mkuu stable, nimependa ulivyoeleza kwa mapana kuhusu OUT. Nami pia 2019/20 nataka nianze undergraduate ya BA in Socialogy (BASO), kuna watu wanasema kama ukikomaa na kujicommit unaweza ukasoma kwa miaka 2 tu, na ukawa umepata degree yako. Je, ni kweli?

Pia ningependa unifafanulie kuhusu malipo na gharama mbalimbali hasa wanapotumia neno UNIT katika mgawanyo wa ada maana nimejaribu kupitia Prospectus yao hawajadadavua kiundani. Na vipi kuhusu utaratibu wa field?

Asante kwa kufuatilia mjadala.

Mimi ninasoma Masters, hivyo nadhani kuna utofauti wa katika ada pamoja na mambo mengine, lakini bado nina nafasi ya kukuelezea yale ninayo yafahamu.

1. Ada - Chuo Kikuu Huria tunalipa ada kwa Unit, ninaposema unit maana yake ni Structure/Composition/Uzito wa course husika, Uzito wa course ndio huonyesha unit za ulipaji, mfano kama course ina unit moja na ada yake unit ni tsh 180,000 maana yake ni kuwa somo lenye unit 2 ada yake itakuwa 180,000x2 = 360,000.

Hivyo huku tunalipa ada kwa course unazochukua kwa kipindi husika cha masomo, na kwa uzoefu wangu mara nyingi course za undergraduate huwa zina mchanganyiko wa unit kuna ambazo zina units 1 na ambazo zina units 2, na mara nyingi course zenye unit 2 zinakuwaga ngumu na hubeba dhamana kubwa katika matokeo yako. hivyo ni vyema unaposoma uwe mwangalifu wa course zenye unit 2.

2. Kuhusu muda wa kumaliza degree - Mkuu nadhani hili nashindwa kulijibia kwakuwa mimi ninasoma Masters, lakini kwa ufahamu wangu ni kuwa kiwango cha chini kabisa kilichowekwa na mamlaka ya elimu tanzania kuhusu kupata degree ni miaka 3, hivyo sidhani kama kuna uwezekano wa kupata Degree chini ya miaka mitatu.

Nami pia nilikuwa ninadhani kama hii, ya kufanya Masters ndani ya mwaka mmoja, lakini imeshindikana sabab chuo kina sisitiza kila course lazima isomwe kwa miezi isiyopungua mitatu. so hata ufanyeje ni lazima uwe ndani ya kipindi kilichowekwa na chuo ili kukidhi ile dhana ya muda uliyowekwa kwa ajili ya Degree au Masters au Phd.

Lakini pia kumbuka huwezi kusoma tu kisha ugraduate, ndio mana kuna mitihani ambayo hupangwa kwa muda husika, hivyo sio speed yako ya usomaji itakufanya kuwa na nafasi ya komba mtihani muda wowote unapojiona uko tayari kwa ajili ya mtihani, waalimu wanahitaji kujipanga kisha kuandaa mitihani kwa muda/semista husika.

Pia hata kama umepata nafasi ya kumemaliza course work ndani ya miaka miwili, utalazimika kusubiri miaka miatatu ipite ndio ugraduate, maana yake utakaa pending mwaka mmoja kusubiri miaka mitatu itimie

3.Utaratibu wa Field - Kama nilivyosema,awali, mimi ninasoma masters, lakini bado ninatambua kuwa Chuo kina muhula kama ilivyo kwa vyuo vingine, hivyo utaratibu wa mafunzo kwa vitendo upo kama kawaida na wanafunzi huomba katika taasisi mbali mbali ili kufanya mazoezi kwa vitendo, hii pia inategemea na course unayosomea, kuna wengine hufanya mazoezi wakiwa mwaka wa kwanza, wengine mwaka wa pili na wengine hufanya mwaka wa tatu. na mazoezi haya ya vitendo unaweza fanya katika ofisi unayofanyia kazi au sehemu yoyote ambapo unaona itafaa kwa ajili ya kutimiza matakwa ya mazoezi ya vitendo na kupata recommendation toka kwa supervisor wako.

Mwisho. mfumo wanaotumia chuo kikuu huria ni mfumo unaotumika sana katika vyuo vingi vya nje, na jambo linalofurahisha zaidi ni aina ya delivery ya materials inayotumiwa na waalimu wa OUT, kwakweli ina motivate hata mtu kusoma kwa bidii, walimu wanasisitiza mwanafunzi kuelewa na sio kukariri, na ndio mana assignment pamoja na mazoezi mbalimbali huwekwa katika platform inayoitwa MOODLE (Modular Object-Oriented Dynamic Learning Environment), yaani kwa namna yoyote mwalimu lazima atajua kama umecopy na kupaste sababu wana software ambazo zimeshakuwa attached to moodle ambazo zinadetect mambo hayo.

stable, Ahsante kwa majibu ambayo nami yamenisaidia, tafadhali unaweza tujulisha muda wa application wa course hii, na pia gharama zake, maana nilisikia Open ada unalipia per course!
 
Ahsante kwa majibu ambayo nami yamenisaidia, tafadhali unaweza tujulisha muda wa application wa course hii, na pia gharama zake, maana nilisikia Open ada unalipia per course!

Ni kweli tunalipa kwa Course/Unit:

1. Gharama.

MPM (Masters of Project Management) ina Course 8, ambazo 6 ni Core alafu 2 ni Elective. Na kila course unit kwa mwaka 2017/18 tulilipia Tsh 220,000 lakini sasa hivi wamepunguza gharama hizo na kuwa Tsh 180,000 per unit.

Kwahiyo, gharama ya course moja yenye unit 2 ilikuwa ni Tsh 220,000 x 2 = 440,000 alafu Dissertation ilikuwa na unit 6, ambapo ni 6 x 220,000 =1,320,000. Hivyo jumla ya gharama kwa tuition fees tu ni (440,000 x course 8) + (Dissertation Unit 6 x 220,000) = 3,520,000 +1,320,000 = Total 4,840,000.

Kwa hesabu hiyo, badilisha kwenye 220,000 uweke 180,000 ambayo ndio bei ya sasa. (360,000 x 8) + (6 x 180,000)
2,880,000 + 1,080,000 = Total 3,960,000. Hivyo Tsh 3,960,000 kwa bei ya sasa ndio gharama ya Course work plus Dissertation.

Kuna michango mingine ya chuo ambayo kwa sasa sitaweza ikumbuka, lakini nashauri uende katika Website ya chuo utaikuta imeorodheshwa.

2. Muda wa Application

Mkuu nadhani kama sijakosea, Open University kwa mwaka wana enroll mara 2 (nakubali kusahihishwa) hivyo muda wa application inategemea na wewe ungependa kuapply mwezi gani, maana kuna June, then December. Nikiri kuwa katika sehem hii sina ufahamu mzuri, ila nikushauri utembelee Regional centre yako, au kupitia website yao kuna namba za help desk, unaweza wapigia watakufahamisha mengi juu ya Usajili wa wanafunzi wapya.

Karibu
 
Asante sana mkuu. Na sasa umeniondoa hofu na kunipa ujasiri mkubwa wa ku-join Open University, maana kuna watu wana mawazo negative sana kuhusu OUT.

Back
Top Bottom