Heri ya mwaka mpya wana MMU, naombeni ushauri, Mimi ni mdada wa miaka 28 nimeolewa.
Ila sikubahatika kusoma, lakini mwenzangu yeye amebahatika kusoma na ana kazi nzuri tu, mwakajana alinishauri nijiunge na elimu ya watu wazima yaani secondary kwa miaka miwili, lengo likiwa nitakapo maliza kidato cha nne nikasome uwalimu, kweli mwaka jana nilisoma na mtihani nikafanya wa Qt vizuri tu ambapo mwaka huu ndo natakiwa nimalizie kidato cha nne kwa kufanya mtihani wa Pc.
Lakini kinachonipa wakati mgumu ni huu utawala wa awamu ya tano ambapo ajira imekua mtihani, hata ajira za waalimu kazi ambayo ilikuwa na uwakika wa ajira pindi tu mtu atokapo chuoni na kupangiwa kituo cha kazi, lakini sasaivi imekuwa tofauti.
Naombeni ushauri je niendelee na masomo na kama nitaendelea na masomo je nitakapo maliza nitasoma kozi gani ya muda mfupi ambayo hata kupata ajira ni rahisi, au niachane na kusoma nifanye biashara, maana naona kama napoteza muda na umri nao unasonga.
Naombeni mnishauri ndugu zangu