Kusimamishwa uchaguzi mdogo Kilombero kwasababisha vurugu kubwa

Kingo

JF-Expert Member
May 12, 2009
855
390
Mawasiliano kati ya wilaya ya Kilosa na Kilombero yamekuwa shakani baada ya uongozi wa Wilaya ya Kilombero kusitisha uchaguzi ambao ungefanyika jana kwa madai kuwa mgombea wa CDM hana sifa ya kugombea kwani alikuwa kifungoni na akaachiwa ghafla. Hali hiyo imeleta mtafaruku na hali si nzuri sana na diwani wa eneo hilo kajiufungia ndani tangu asb.

Source: ITV Breaking News, Morogoro RPC
 
Wananchi kilombero wamepambana na polisi baada ya uchaguzi mdogo kusitishwa.mawasiliano wa kilombero na kilosa yamekatwa.source Radio one
 
Halmashaur ya wilaya ya kilombero hivi leo kumetokea mafuko ya wananchi kufunga barabara inayounganisha wilaya ya kilombero na kilosa.hali hiyo ya sintofaham imejitokeza baada ya serikali kuairisha uchaguzi wa mwenyekiti wa kitongoji na kijiji .kwa madai ya halmashaur ni kuwa mgombea wa chadema hana sifa za kuwa kiongozi kwan hivi karibun alikuwa na keSi mahakamani.
 
JK analeta mzaha sana yaani kuna siku nchi italipuka hii hatakaa aamini kinachotokea
 
Mgombea wa Cdm.. aliwekewa pingamizi na ccm , Pingamizi likatupwa .Ccm wakakata rufaa kwa mkurugenzi .. na cdm wakaendelea na kampeni kama kawaida .ccm wakagoma kufanya kampeni eti wanaogopa kufanyiwa fujo na cdm . kituko ijumamosi Ded kilosa katangaza kusitisha uchaguzi uliokuwa ufanyike ijumapili ya tar 27 june.ndio chanzo cha fujo .kwani hoja za rufaa za ccm hazina mashiko .wanaogopa uchaguzi watabwagwa na cdm .
 
Mawasiliano kati ya wilaya ya Kilosa na Kilombero yamekuwa shakani baada ya uongozi wa Wilaya ya Kilombero kusitisha uchaguzi ambao ungefanyika jana kwa madai kuwa mgombea wa CDM hana sifa ya kugombea kwani alikuwa kifungoni na akaachiwa ghafla. Hali hiyo imeleta mtafaruku na hali si nzuri sana na diwani wa eneo hilo kajiufungia ndani tangu asb.

Source: ITV Breaking News, Morogoro RPC

Tuhabarishane wakuu huu ni uchaguzi wa kumchagua nani kwa tarehe zipi?
 
Alishinda kwa rufaa. Vipi Aden Rage ,si alifungwa akatoka kwa rufaa .je ina tofauti .ccm wanaogopa uchaguzi.
 
Mawasiliano kati ya wilaya ya Kilosa na Kilombero yamekuwa shakani baada ya uongozi wa Wilaya ya Kilombero kusitisha uchaguzi ambao ungefanyika jana kwa madai kuwa mgombea wa CDM hana sifa ya kugombea kwani alikuwa kifungoni na akaachiwa ghafla. Hali hiyo imeleta mtafaruku na hali si nzuri sana na diwani wa eneo hilo kajiufungia ndani tangu asb.

Source: ITV Breaking News, Morogoro RPC
....mawasiliano gani yamekatika? yana uhusiano gani na uchaguzi?
 
Back
Top Bottom