Kweli mwamba, nami sijasahau nilisimama kwenye treni toka DSM mpaka Mwanza. Almost 40 Hours njiani, tena kwenye corridor la katikati ya viti ambapo watu hupita kila wakati kwenda mbele wengine kwenda nyuma wakikanyaga chochote na hawasikii ukilalamika. Unamwona aliyekaa analalamika ati kachoka kukaa lakini haruhusu kukupa nafasi ukae kidogo. Niliapa nikipangiwa kufanya kazi Mwanza naacha kazi. Siku hizo kulikuwapo ndege na treni tu. Mabus hayakuwapo. Ndege labda uwe na kauhusiano na kina Rostam wa siku zile, maana hata uuze kila kitu chako hufikii hata nusu ya bei ya ticket. Unamuuliza Mungu, "Nimekukosea sana kuliko binadamu yeyote hata niteseke kiasi hiki?" Weacha tu.