Kushuka kwa viwango vya elimu.

h.imani

Senior Member
Oct 2, 2011
189
94
WALIMU.

Enzi zile wanafunzi walikuwa wanapelekwa kusoma aliefaulu tena kwa kuchaguliwa moja kwa moja na sio kuandika barua za maombi. Kwahiyo walimu wote waliokwenda vyuoni walikuwa wamechaguliwa kwa ufaulu wa juu sana kiasi kwamba walikuwa wabunifu wa hali ya huu sana katika ufundishaji na juhidi za ufundishaji haukuwa ni wito kama tunavoelewa, isipokuwa mambo haya yalipelekea walimu hawa kuwa bora sana katika ufundishaji;

1. Walimu walichaguliwa kwaufaulu mzuri usiopingika.
2. Walimu walisoma bure katika vyuo/shule walivyopangiwa.
3. Walimu walisafirishwa kwa gharama ya serikali mpaka vituo vyao vya kazi.
4. Walimu walipewa posho ya kujikimu wakati akianza kazi bila mizengwe.

Mambo haya yalipelekea walimu hawa kutokuwa bora katika ufundishaji;

1.
Walimu wanaomba vyuo vya ualimu na kupata nafasi hizo sio kwa kiwango cha ufaulu kama inavotakiwa.
2. Walimu hupewa nafasi za kusoma kwa rushwa na sio kuzingatiwa kwa sheria na taratibu
3. Walimu walisoma kwa pesa zao mwanzo hadi mwisho na hio hupelekea kazi kufanya kama maslahi yapo.
4. Walimu hupewa posho zao na mishahara yao kwa mizengwe na ikiwa wamegharamia kila kitu mpaka kufikia kuitwa mwalimu.

Kwa upeo na uelewa wangu ni kuwa; ili elimu uwe safi na nzuri zaidi ya tuliyonayo sasahivi, inatakiwa ELIMU KWA NGAZI ZOTE ITOLEWE BURE, ili ikija suala na kufundisha kwa tena ikibidi kwa kujitolea mwalimu hawezi kusita na ataonesha juhudi ya hali yajuu tena kwa mshahara wakawaida sana, na kama kunakuwa na malalamiko ya maslahi kusolve kwake itakuwa ni rahisi ukilinganisha na sasa.

Huu ni mfano tu wa idara/secta ya elimu, pia hata secta ya afya pia.

Naomba mnisahihishe kama kunamahali nimebugi.

See you.
 
Hii ishu ya Big Results Now kwangu naona haitofanikiwa kurejesha maana ya elimu kwasababu;
1. Ni sera kama zilizowahi kuwepo na zikafa ambazo huanza juu i.e top kuja chini i.e down kisiasa
2.Katika vipaumbele 9 vya BRN kile cha motisha kwa waalimu kinataja vyeti,Tv n.k kwamba watazawadiwa waalimu kitu ambacho sidhani kama waalimu wanahitaji hayo kweli ama wanahitaji mishahara bora
3.Shule za kata bado hazina waalimu wa kutosha kila somo kwa mikondo yote
4.Waalimu hawajaguswa kwa kuwalipa mishahara bora
 
siasa pia imechangia kushuka kwa elimu mfano nenda staff zao story zao ni siasa mwanzo mwisho ccm iko vile cdm wapo hivi kipindi cha dk 40 wengi huwa wanatenga dk 10 za siasa hakuna muda wanajadili taaluma kisa kupuuzwa kwa madai ya walimu mzee wa kaya ctaki kura zenu kwani mko wangapi
 
Back
Top Bottom