uhurumoja
JF-Expert Member
- Mar 2, 2014
- 12,019
- 28,581
Naamini naongea na watu wa rika mbalimbali kwamba vijana na watu wazima wenye familia basi kama mada inavyojieleza niko hapa kuwaambia vijana na wazazi kuwafundisha watoto na vijana na hata watu wazima sasa kushiriki katika malezi au matunzo yao.huwa najiuliza leo hii kijana anaanza kuvuta unga je ni kweli kwamba hajui madhara ya unga?mtu anakunywa pombe na kuwa mlevi wa kupindukia je ni kweli kwamba hajui madhara yake,mwanamke au mwanaume mwenye familia anatoka nje ya ndoa na kuanzisha uhusiano ambao wakati mwingine humfanya hata asahau kabisa familia yake je hajui kwamba afanyalo ni baya,mwanafunzi wa primary na secondary anapojiingiza katika starehe mpaka kusahau kabisa au kuacha shule je hajui kwamba jambo hili ni baya.jama tunaishi katika dunia ambayo imejaa kila aina ya mifano mizuri na mibaya hauhitaji mzazi au mwenza akwambie jambo zuri au baya waweza ona hata we mwenyewe na kufanya uamuzi sahihi tusiwe sababu ya kuwafanya wengine walie just because we can do that kumbuka jambo lolote baya unalofanya leo kuna mtu linamuumiza au litamuumiza zaidi baadae.jitahidi kuwa furaha kwa wengine.