Leo nimewatoa madogo kwenda kuangalia movie waliokuwa wanaisubiria kwa hamu sana ya Minecraft
Aisee, sikujua kumbe leo ndio ilikuwa onyesho la kwanza nchi nzima
Huo Mzuka nilioukuta humo ndani kwa vijana wa mashabiki wa video game ya Minecraft sio mchezo.
Ilikuwa ni miruzi na makofi na kushangilia kwa sana, kila ikitokea sehemu inawakosha , kama I am Steveeee.................... Chicken Jerky......
Zamani wakati tunapelekwa kungalia movie na wazazi huko Empire, New Chox na Odeon cinema, kuangalia movie za kihindi na za Bruce Lee, ilikuwa ni shangwe na makofi mengi ndani ya movie kutoka kwa watazamaji, pale starring anapotembeza mkono.
Nilivyokua kijana nikiwa nikienda mwenyewe na kukutana na hizi kelele na vigelegele ndani ya movie nilikuwa naona ni ushamba sana,
Ila leo nimejiona mimi ni mshamba, sababu madogo na wenyewe kumbe wanacheza sana hiyo game ya Minecraft na wenyewe walikuwa mstari wa mbele kupiga makelele na makofi ndani ya movie , mwanzoni nilikuwa nawakaripia watulie kumbe wananiona dingi mnoko hata kwenye movie, ila baadae hata mimi nilijikuta naanza kushangilia nao na makofi mengi ndani movie.
Kweli uzee ni ushamba....