Kuseti DSTV Dish.

Infopaedia

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
1,234
Reaction score
1,503
Habari za saa hii wakuu. Natafuta mtaalamu wa kunisetia dish langu la Dstv. Ukiwa na contact ya mtaalamu pia si vibaya ukituunganisha. Nipo jijini mwanza. Ni-pm kwa mazungumzo zaidi.
 
Hilo haliwezi kuwa DSTV..
DSTV wanakupa na hadi fundi,kuwa muwazi ni TING au uchafu mwingine!
 
Hilo haliwezi kuwa DSTV..
DSTV wanakupa na hadi fundi,kuwa muwazi ni TING au uchafu mwingine!

Dah! kwanza asante sana kaka kwa ku-take trouble na kuandika. Sintokulaumu sababu naelewa. Turudi kwenye mada. Hili dish nilikuwa nalitumia Arusha. Sasa nimehamia Mwanza.............. Nasubiri msaada wako
 
kaka nipo mbali tarime ningekufungia dstv kwa bei chee.kama unaweza kunilipia usafiri am ready
 
kaka nipo mbali tarime ningekufungia dstv kwa bei chee.kama unaweza kunilipia usafiri am ready
Asante sana kaka kwa plan yako ya kunisaidia. Naomba iwe plan C. Hapa Mwanza kuna duka kubwa la vifaa vya kielektroniki linaitwa Semira (kama sijakosea). Wanauza satelite dishes. Plan A nataka niende pale nikaulizie fundi. Natumaini nitapata.
 
sawa kaka mafundi ni wengi sana,mmoja wao huyu hapa yuko mwanza 078-495-9379 atakusaidia
 
kaka ungekuwa na uelewa japo kidogo kujusu haya mambo ningekuelekeza fasta kaka
 
kaka ungekuwa na uelewa japo kidogo kujusu haya mambo ningekuelekeza fasta kaka
Huo uelewa mdogo ukoje kaka? Kama kulitundika nimeshalitundika. Kulizungusha juu chini, mashariki kusi kaskazi magharibi, sana tu. Ku-connect cable mpaka kwenye kisimbuzi naweza. Kuingia kwenye setting za kisimbuzi na kubadili frequency, transponder na mlolongo wote naweza. Zaidi ya hapo sina ujanja kaka.
 

sasa kama yote hayo unaweza unakwama wapi sasa mkuu?!!!!...umenikumbusha enzi za kuita "fundi" aje "kukufungia" computer uliyonunua!!!
 
sasa kama yote hayo unaweza unakwama wapi sasa mkuu?!!!!...umenikumbusha enzi za kuita "fundi" aje "kukufungia" computer uliyonunua!!!
Usitake nicheke mkuu. Bora hiyo ya computer, umenikumbusha moja. Kipindi kile simu ndiyo zimeingia, nilienda kwa fundi simu. Kuna jamaa akaja anataka abadilishiwe mlio wa simu (ring tone). Alibadilishiwa na akalipa pesa. Nilishangaa sana, coz by that time na mimi nilikuwa a bit full maujanja kwenye tweak za simu. BTW kinachonishinda hapo ni kutafuta nyuzi mkuu, pia jinsi ya kujuwa kama Low Noise Block (LNB) ni nzima au mbovu. Coz LNB yenyewe inakaribia mwaka sasa ilikuwa chini ya uvungu tu. Lakini nadhani kinachonikwamisha nisi-set mwenyewe ni muda pia. Sina muda wa kutosha kuhangaika nalo. Naona bora kumuita mtu amalize issue. Ila hao mafundi wakinizinguwa, napanda mwenyewe juu ya bati. Nalielekezea linakotokea jua, nali-turn kushoto to some degree then nalibetuwa kwa juu. Kama LNB itakuwa poa, lazima bar ya signal strength igonge mia faster, zaidi ya hapo basi kuna mkono wa mtu.
 

Hahahaa, kweli tumetoka mbali mkuu. btw, kama una smartphone yoyote inaweza kukusaidia kutafuta uelekeo, la sivyo we angalia jua linakochomozea halafu unakuwa unatingisha taratibu mpaka kitu kikubali! lakini kama tatizo ni mua we mwite fundi mchundo na yeye apate rizki!
 

hii kwa kutumia smartphone unafanyaje?
 
hii kwa kutumia smartphone unafanyaje?

Kama unatumia android download application inaitwa sat finder then andika code za sat unayotaka itafind wakati unazungusha simu na ikifika mahala pake itapiga alarm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…