Zanika
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,316
- 752
- Thread starter
- #121
Mm ni mzaliwa wa Kilimanjaro.Wachanga wamepambana na hali zao kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwao.nchi hii haijawah kua na rais mchaga.mm sio wa huko lakini hoja yako haina mashiko.Ukilazimisha maendeleo kwa nguvu ni kazi bure.Ukipeleka uwanja wa ndege mahali angalia jamii husika.watu wa jamii husika lazma waamke.Angalia mahitaji yao.Wengine wanataka soko la pamba ww unapeleka Airport. Arusha na moshi yote ni miji ya kitalii then unataka viwanja vya ndege vijengwe Manyara ili madini unayosema yapande ndege kirahisi kwenda Ulaya?.uzalendo wako una mashaka.NI kweli shughili za mji wa Manyara ni nyingi kma utalii lakini ukifuatilia kampuni zote za utalii ziko Moshi na Arusha.Huko Manyara kwako ni kwenda kuangalia wanyama tu,dola zikiwa zimebaki Arusha na Moshi.Hahahaaaa.Hao wabaki kuonyesha watalii shughuli mbalimbali ikiwemo tamaduni za kimasai.
Nataka nikuambie ukweli usio kificho vingi ya ulivyotaja hapo juu vililetwa na Serikali zilizokuwepo si kwa sababu mnazoaminishwa kuwa jamii zetu zilikuwa zimeelimika jambo ambalo si kweli kwani bado kulikuwa na % kubwa sana ya wasio na elimu kuluko waliopata elimu. Maendeleo yaliebda kwa sababu ya vivutio vilivyokuwepo na ambavyo kwa Taifa vilikuwa ni kipaumbele kuweka miundo mbinu sambamba na huduma. Tena watendaji walikuwa ni wa kutoka jamii zingine za nchi hii na walitimiza wajibu wao pasipo kinyongo bila kujali wao sio watu wa Kaskazini.
Usilolijua ama unalolidharau ni kuwa nchi yetu ina vivutio vingi ambavyo kwa Dunia ya sasa sio lazima biashara yake ipitie baharini kama ilivyokuwa enzi za mkoloni na awamu za mwanzo baada ya Uhuru. Au utalii u-operate kutokea Mikoa ya Kaskazini pekee. Hata Musoma au Mwanza Mtalii anaweza fika akaenda Serengeti mradi atengenezewe plan nzuri na yenye tija kwa upande wake.
Haihitaji mfanya biashara wa madini wa Geita na maeneo mengine wa kanda hizo asafiri hadi Kilmanjaro,Dar,Kigali au Entebe ili aende nchi za nje and v/s. Hayo yamepitwa na wakati sasa ambapo Wafanya biashara wanataka kufika mahali haraka na kumaliza deals zao waangalie issue zingine.. Hivyo kuwa na International Airport eneo la Mikoa ya Ziwa Nyanza kwangu mimi ni fursa nzuri itakayofungua zaidi milango ya uchumi wa taifa letu.
Pili utalii nchi hii ni mpana na umeenea kila kona ya nchi kuliko unavyofikiria wewe. Kigoma inajulikana kimataufa kwa Sokwe na utalii wa eneo la Ziwa Tanganyika,jirani na hayo maeneo ya Geita,Chato Biharsmulo kuna hifadhi zipo. In short kunahitajika kufungua milango ya fursa tulizo nazo kila kona ya nchi yetu ili kuimarusha uchumi wetu. Kinachohitajika ni wananchi kujiongeza na kujichanganya kwenye fursa hizi na sio kufanya promo za ubaguzi.