Kusamehe ni mtihani, jitahidi uushinde

Kusamehe ni mtihani, jitahidi uushinde

Think Hard

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
318
Reaction score
307
NI NJEMA KWAKO ISOME

Katika maisha hakuna jambo gumu kama kusamehe na hakuna kitu chenye faida kama kusamehe. Kuna watu katika maisha wapo ili tuumie na TUJIFUNZE. Wengine wapo ili tukisha umia wao watuumize zaidi ili tukose imani kwa wengine!

Lakini katika wote, wapo ambao kazi yao ni kutufariji, wao Inawezekana walipitia magumu kama yetu hivyo wana fahamu njia ya kutokea lakini kwa sababu tuliumizwa zaidi hatutaki kuwaamini hata wao. Ukisamehe unaweza kuamini upya!

Ni kweli katika maisha bila watu kama hao hatuwezi kuitwa "imara". Umewahi KUJIULIZA kwanini mtu anaitwa MVUMILIVU?? Kipimo chake ni kipi?? Uwezo wa kusamehe na kusonga mbele bila malalamiko ndiyo UVUMILIVU HALISI.

HAUNA jambo gumu kama kusamehe maumivu ambayo yanajirudia kichwani, yana choma moyo kama panga kali...... Vuta picha mtu anakuumiza alafu vilevile anataka akumalize kabisa! Alafu baada ya kuumbuka anaomba msamaha!

Vuta picha umemfumania mkeo au mume wako alafu una ambiwa samehe! Vuta picha mtu kamuua mzazi wako au ndugu yako kisha una ambiwa samehe! Moyo unauma, akili inakataa, mwili unawaka hasira lakini bado una ambiwa samehe, jikaze tu!

Wengine walikusababisha uishi maisha ambayo unaishi kwa sasa, unatamani hata wafe! Lakini una ambiwa samehe! Msamaha ni nini hasa?? Unalia ukijipiga kifua, msamaha ni nini?? Machozi ya uchungu yanakutoka kujaribu kuosha hasira yako lakini moyo unakataa!

Utaimba nyimbo zote za kujifariji lakini moyo unasema HAPANA NIMEUMIZWA SANA. Unashindwa kula na kulala vizuri kwa sababu umeumia! Mbaya zaidi hisia zikiumia ni hatari kuliko Simba aliye katwa mguu! Na wengi wana umizwa sana kwa sababu ya kitu kimoja tu IMANI.

Wengi leo wame umizwa sana na Mama mkwe, shangazi, wazazi, ndugu, marafiki, wapenzi, majirani na kadhalika! Lakini tiba ni moja tu, KUSAMEHE. Kutokusamehe ni sawa na kumsaidia shetani kufanya kazi maana mawazo yako yatakuwa sawa na shetani anavyo waza (uharibifu).

Kusamehe ni tiba ya presha, ni tiba ya kichwa na moyo. Kusamehe ni dawa ya maisha na pia ni baraka kwako! KUSAMEHE kunamfanya MUNGU akuamini ili upande daraja la imani la kiwango kingine cha juu zaidi.

Nakumbuka katika maisha yangu, nimewahi KUUMIZWA mara nyingi tu katika mambo tofauti tofauti, lakini mara zote napata somo jipya. Pamoja na kujifunza sana lakini kuna muda ilinibidi NISAMEHE KWA MACHOZI, yaani nasamehe nikiwa natokwa machozi kwa lengo la kuuponya moyo wangu!

Ni kweli umeumia lakini Samehe sasa, samehe leo, samehe kesho, samehe siku zote! Binadamu wana umiza sana sana sana tena sana lakini jivike moyo mkuu, samehe ili maombi yako yakubaliwe na MUNGU. Kumbuka msamaha ni tiba, ni amani ni upendo ni faida.

NB: Kwa yeyote aliye wahi kuniumiza kwa namna yoyote ile NIMEMSAMEHE, kwa yeyote yule anaye ona nimemuudhi na anisamehe, kwa yeyote yule ambaye huwa anahisi sijamsamehe na afahamu sasa kwamba NIMEMSAMEHE asitazame ukubwa wa kosa au mazingira ya ugomvi, atazame utumishi na huruma ya MUNGU ndani yangu, amen.
 
Kuna mambo mengine yanaumiza sana sana, bila hofu ya Mungu unaweza hata kuua. Ila tunaambiwa ni vema kusamehe kwan kwa kufanya hivyo utakuwa umempalia makaa huyo mkosa, Mungu tuumbie moyo wa msamaha
 
Mungu ni mwema sana...atakupa moyo wa kusahau na ukaishi kwa amani kabisa..
 
asante Mkuu, aisee nikimkumbuka huyu aliyenitenda inauma sana sana ila ngoja nimsamehe tu
Mwombe Mungu akupe moyo wa kusamehe na kusahau ndugu....Utaishi maisha ya amani kabisa..
 
Nilitendwa!!!! niliumia ,nilijichukia nilimchukia kila aliyeitwa mwanaume.... lakini baada ya kwenda kanisani Padri akasema Msamaha ni nin ? alipotuelezea maana yake hakika nilirudi nyumbani nikaa na kutafakari nikajiona mim mjinga..nikaomba na kuachilia msamaha na kumpigia simu aliyeniumiza nikamwambia nimekusamehe kisha nikakata simu..toka siku hiyo nina amani moyoni mwangu nikiwa nimejawa na furaha maana nilikonda kipindi ambacho sijasamehe ..hakika msamaha huleta uponyaji pale palipo na maumivu ...samehe kila aliyekukosea au kukukwaza katika maisha yako..Hakika msamaha ni tiba
 
Neno kusamehe ni gumu sana kwa mawazo na akili za kibinadamu........lakini ndio njia pekee ya kuweza kuishi kwa amani....dawa chungu lakini inaponya.........kuna machungu unafanyiwa na binadamu unashindwa kuelewa aliwaza nini hadi kufikia kufanya hayo.....mwisho wa siku msamaha ni silaha ya ushindi
 
Daahh!!!hapana simsamehi kwanza!!

looh!kwa makwazo yalee!!!

bado bado!
 
Mimi ni mgumu sana kusamehe jamani hapa naumizwa yaani nina mtu alinikwaza mwaka jana October kama hii had leo sipokei simu yake wala sitaki hata kumuona. Kifupi moyo wangu mgumu sana kusamehe nahitaji maombi yenu wanajukwaa ili niwe huru kama anavyotushauri Think Hard.
 
Yaani hapa ni sawa na tambwe kufunga goli la mkono halaf uwaabie wale wasamehe… .ni ngumu sana
 
Huwa nasamehe baada ya kushindwa revenge.
 
Nilitendwa!!!! niliumia ,nilijichukia nilimchukia kila aliyeitwa mwanaume.... lakini baada ya kwenda kanisani Padri akasema Msamaha ni nin ? alipotuelezea maana yake hakika nilirudi nyumbani nikaa na kutafakari nikajiona mim mjinga..nikaomba na kuachilia msamaha na kumpigia simu aliyeniumiza nikamwambia nimekusamehe kisha nikakata simu..toka siku hiyo nina amani moyoni mwangu nikiwa nimejawa na furaha maana nilikonda kipindi ambacho sijasamehe ..hakika msamaha huleta uponyaji pale palipo na maumivu ...samehe kila aliyekukosea au kukukwaza katika maisha yako..Hakika msamaha ni tiba
Hongera sana Binti wa kirombo.....Nafurahi umetoa ushuhuda ya kuwaponya wengine...Ubarikiwe sana coz natamani sana kila aliyekosewa asamehe na asahau..
 
Mimi ni mgumu sana kusamehe jamani hapa naumizwa yaani nina mtu alinikwaza mwaka jana October kama hii had leo sipokei simu yake wala sitaki hata kumuona. Kifupi moyo wangu mgumu sana kusamehe nahitaji maombi yenu wanajukwaa ili niwe huru kama anavyotushauri Think Hard.
Pole sana Gololi One..Kiukweli natambua ni vigumu sana sana kusamehe kwa akili ya kibinadamu..Lakini naamini kabisa ukiwa serious na dhamira ya dhati wa kusamehe nakuhakikishia inawezekana.. Kukubwa mshirikishe Mungu na ufikirie kwa undani zaidi mateso unayoendelea kupata pindi tu unapomkumbuka aliyekutenda...Amua tu na jivike ujasiri then Msamehe... Nakuhakikishia slowly but surely utasahau na hata ukikumbuka utakua na amani...
Nakutakia kila la kheri na Naomba Mungu akupe moyo wa kusamehe..
Kumbuka: Msamaha Pekee ndio jibu la amani na ushindi wako..
 
NI NJEMA KWAKO ISOME

Katika maisha hakuna jambo gumu kama kusamehe na hakuna kitu chenye faida kama kusamehe. Kuna watu katika maisha wapo ili tuumie na TUJIFUNZE. Wengine wapo ili tukisha umia wao watuumize zaidi ili tukose imani kwa wengine!

Lakini katika wote, wapo ambao kazi yao ni kutufariji, wao Inawezekana walipitia magumu kama yetu hivyo wana fahamu njia ya kutokea lakini kwa sababu tuliumizwa zaidi hatutaki kuwaamini hata wao. Ukisamehe unaweza kuamini upya!

Ni kweli katika maisha bila watu kama hao hatuwezi kuitwa "imara". Umewahi KUJIULIZA kwanini mtu anaitwa MVUMILIVU?? Kipimo chake ni kipi?? Uwezo wa kusamehe na kusonga mbele bila malalamiko ndiyo UVUMILIVU HALISI.

HAUNA jambo gumu kama kusamehe maumivu ambayo yanajirudia kichwani, yana choma moyo kama panga kali...... Vuta picha mtu anakuumiza alafu vilevile anataka akumalize kabisa! Alafu baada ya kuumbuka anaomba msamaha!

Vuta picha umemfumania mkeo au mume wako alafu una ambiwa samehe! Vuta picha mtu kamuua mzazi wako au ndugu yako kisha una ambiwa samehe! Moyo unauma, akili inakataa, mwili unawaka hasira lakini bado una ambiwa samehe, jikaze tu!

Wengine walikusababisha uishi maisha ambayo unaishi kwa sasa, unatamani hata wafe! Lakini una ambiwa samehe! Msamaha ni nini hasa?? Unalia ukijipiga kifua, msamaha ni nini?? Machozi ya uchungu yanakutoka kujaribu kuosha hasira yako lakini moyo unakataa!

Utaimba nyimbo zote za kujifariji lakini moyo unasema HAPANA NIMEUMIZWA SANA. Unashindwa kula na kulala vizuri kwa sababu umeumia! Mbaya zaidi hisia zikiumia ni hatari kuliko Simba aliye katwa mguu! Na wengi wana umizwa sana kwa sababu ya kitu kimoja tu IMANI.

Wengi leo wame umizwa sana na Mama mkwe, shangazi, wazazi, ndugu, marafiki, wapenzi, majirani na kadhalika! Lakini tiba ni moja tu, KUSAMEHE. Kutokusamehe ni sawa na kumsaidia shetani kufanya kazi maana mawazo yako yatakuwa sawa na shetani anavyo waza (uharibifu).

Kusamehe ni tiba ya presha, ni tiba ya kichwa na moyo. Kusamehe ni dawa ya maisha na pia ni baraka kwako! KUSAMEHE kunamfanya MUNGU akuamini ili upande daraja la imani la kiwango kingine cha juu zaidi.

Nakumbuka katika maisha yangu, nimewahi KUUMIZWA mara nyingi tu katika mambo tofauti tofauti, lakini mara zote napata somo jipya. Pamoja na kujifunza sana lakini kuna muda ilinibidi NISAMEHE KWA MACHOZI, yaani nasamehe nikiwa natokwa machozi kwa lengo la kuuponya moyo wangu!

Ni kweli umeumia lakini Samehe sasa, samehe leo, samehe kesho, samehe siku zote! Binadamu wana umiza sana sana sana tena sana lakini jivike moyo mkuu, samehe ili maombi yako yakubaliwe na MUNGU. Kumbuka msamaha ni tiba, ni amani ni upendo ni faida.

NB: Kwa yeyote aliye wahi kuniumiza kwa namna yoyote ile NIMEMSAMEHE, kwa yeyote yule anaye ona nimemuudhi na anisamehe, kwa yeyote yule ambaye huwa anahisi sijamsamehe na afahamu sasa kwamba NIMEMSAMEHE asitazame ukubwa wa kosa au mazingira ya ugomvi, atazame utumishi na huruma ya MUNGU ndani yangu, amen.
Asante sana , nimejifunza kitu. Ila changamoto kumsamehe mtu ambaye upo nae kila siku kwa mfano mpenzi. Ninaweza kusamehe, lkn siwezi kuvumilia kuendelea kumuona aliyenikosea,kwangu ni kama ananitonesha kidonda.
 
Back
Top Bottom