Kusaliti vs Kusalitiwa

Kusaliti vs Kusalitiwa

muhala.jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
751
Reaction score
659
MATAABIKO YA KIMAISHA ANAYOPATA MSALITI BAADA YA USALITI!

MTENDWA wa usaliti hupata maumivu makali, wakati huohuo mwanzoni msaliti hukenua kwa kudhani ameshinda. Maisha hayapo hivyo!

Anayesalitiwa humwaga machozi kwa kilio cha mahangaiko ya moyo. Husahau kumshukuru Mungu. Hutamani kulipa kisasi. Hushindwa kutambua kuwa mzunguko wa maisha ya binadamu kama Maulana alivyoumba, tendo baya humrudia mtendaji mwenyewe wasaa unapotimu.

Laiti kila mmoja angejua mataabiko ambayo wasaliti hukutana nayo, kungekuwa na nafuu kubwa ya kimaisha. Idadi ya vitendo vya usaliti ingepungua.
Msaliti anapaswa kujua; Unapomsaliti mwenzio maana yake unakuwa sawa na kuyageuza maisha yake juu chini. Hilo siyo jambo dogo, kwani unaharibu mfumo wa maisha yake. Maumivu unayompa ni makubwa mno.

Katika uhusiano wa kimapenzi au ndoa, unapomsaliti mwenzio unakuwa umeingiza kaa la moto ndani ya moyo wa mwenzako. Aliwekeza upendo wake na imani kubwa, usaliti wako unamsababishia aende kuanza upya!

Wachumba wanaachana, ndoa zinavunjika. Urafiki Unavunjika, Yupo ambaye amewahi kutafsiri usaliti kama mfano wa mtu aliyetumia muda mrefu kujenga ghorofa lakini wewe unakuja kubomoa kwa siku moja.

Imani inajengwa na huchukua muda mtu kumwamini mwenzi wake kwa kiwango cha kutokuwa na shaka juu yake. Inapotokea anabaini kufanyiwa kitu tofauti na imani aliyokuwa nayo, kila kitu hubadilika. Imani yote huondoka na ni vigumu mno kumwamini tena.

Kabla ya kufika kwenye pointi ya kuchambua mateso kama siyo mataabiko ya wasaliti, tubaki kwenye swalu la msingi umewahi Kusalitiwa katika mapenzi ?
Je unaamini kua malipo ya usaliti ni hapa hapa duniani na kwa mungu ni mahesabu tuu? Tubadilike tuache kuwasaliti wanao tupenda jamani INAUMA SANA KUSALITIWA NA UNAE MPENDA.

#jr....#mngoni wa town!
 
Nishasaliti na kusalitiwa mara kibao wacha niwe msomaji tuu.
IMG_20180725_201721.jpg
 
Kulingana na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanakumba kizazi chetu hiki ,frankly speaking uaminifu ktk mahusiano umekuwa negligible, na hii huchangiwa na sababu mbalimbali ila hasa ni tamaa.

Lakini pia baadhi ya watu huweza kukufanya usaliti bila kupenda kutokana na kuleta chokochoko kadha wa kadha ktk mapenzi

Cha msingi tuingie kwenye mahusiano tukijua kusalitiwa kupo ili hata siku ukisalitiwa basi usiumie hadi kuhatarisha maisha yako. Jipende kwanza kabla ya kupendwa.

Mapenzi ya kweli yashaded zamani,sasa hivi n kuelewana tu bhc...tuache kupenda kindezndez bhn
 
Usaliti upo sana tu kwa sababu watu tumekuwa wabinafsi sana hatufikirii matokeo yale tunayofanya kuelekea wengine

Tunajifikira zaidi ndo maana watu wengi sana wanaona kawaida sana kusaliti wenzi wao,ila ikitokea siku moja wao pia wamesalitiwa athari yake ni kubwa sana wengine huweza kuanguka hata presha au kupata maumivu makali sana na ya muda mrefu.

Kama tungeweza kujifunza kufikiria na kujali hisia za wengine usaliti ingekuwa ni msamiati tu.
 
Hakuna jambo linauma kama usaliti..niliwahi kusalitiwa na mtu nisiyemtarajia kama atafanya hivyo na kila nikimfikiria hadi leo najihisi kutetemeka!

Kimsingi nilichokuja kujifunza ni kutrust nobody

Kwa niliyenaye sasa nitaendelea kumpenda na kuwa mwaminifu kwake ila simuamini ile 100%
 
Usaliti haujawahi kuwa na matokeo mazuri hata siku moja

Lazima malipo yapatikane hasa kwa wale ambao wanasaliti wenzao bila kujutia wala kuona ubaya wa kufanya hivyo
Niliwahi kumsaliti mtu mwishowe nikajikuta nimenusurika ngoma, nikaishia PEP
 
Nimewahi kumsaliti mtu , japo hakujua.
Ila hadi Leo roho inanisuta kwa nini nilimfanyia vile.
SI kwasababu we Malaya au kuna maelezo mengine [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Au tumsingizie shetani
 
MATAABIKO YA KIMAISHA ANAYOPATA MSALITI BAADA YA USALITI!

MTENDWA wa usaliti hupata maumivu makali, wakati huohuo mwanzoni msaliti hukenua kwa kudhani ameshinda. Maisha hayapo hivyo!

Anayesalitiwa humwaga machozi kwa kilio cha mahangaiko ya moyo. Husahau kumshukuru Mungu. Hutamani kulipa kisasi. Hushindwa kutambua kuwa mzunguko wa maisha ya binadamu kama Maulana alivyoumba, tendo baya humrudia mtendaji mwenyewe wasaa unapotimu.

Laiti kila mmoja angejua mataabiko ambayo wasaliti hukutana nayo, kungekuwa na nafuu kubwa ya kimaisha. Idadi ya vitendo vya usaliti ingepungua.
Msaliti anapaswa kujua; Unapomsaliti mwenzio maana yake unakuwa sawa na kuyageuza maisha yake juu chini. Hilo siyo jambo dogo, kwani unaharibu mfumo wa maisha yake. Maumivu unayompa ni makubwa mno.

Katika uhusiano wa kimapenzi au ndoa, unapomsaliti mwenzio unakuwa umeingiza kaa la moto ndani ya moyo wa mwenzako. Aliwekeza upendo wake na imani kubwa, usaliti wako unamsababishia aende kuanza upya!

Wachumba wanaachana, ndoa zinavunjika. Urafiki Unavunjika, Yupo ambaye amewahi kutafsiri usaliti kama mfano wa mtu aliyetumia muda mrefu kujenga ghorofa lakini wewe unakuja kubomoa kwa siku moja.

Imani inajengwa na huchukua muda mtu kumwamini mwenzi wake kwa kiwango cha kutokuwa na shaka juu yake. Inapotokea anabaini kufanyiwa kitu tofauti na imani aliyokuwa nayo, kila kitu hubadilika. Imani yote huondoka na ni vigumu mno kumwamini tena.

Kabla ya kufika kwenye pointi ya kuchambua mateso kama siyo mataabiko ya wasaliti, tubaki kwenye swalu la msingi umewahi Kusalitiwa katika mapenzi ?
Je unaamini kua malipo ya usaliti ni hapa hapa duniani na kwa mungu ni mahesabu tuu? Tubadilike tuache kuwasaliti wanao tupenda jamani INAUMA SANA KUSALITIWA NA UNAE MPENDA.

#jr....#mngoni wa town!
Usaliti= usaa+lita

Yaan usaliti = ujenge ghorofa miezi sita kwa kutumia billions of money and then libomolewe na tetemeko la dakika moja na sekunde kadhaatu, lote chiniii=> usaa+lita[emoji21]
 
Back
Top Bottom