Kusafirishs laptop

Kusafirishs laptop

Ze Heby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
5,906
Reaction score
6,694
Wakuu naomba mrejee kwenye kichwa cha uzi.Nina laptop nataka niitume Songea,naomba mwenye kujua watu wanaofanya hii kazi na ikiwezekana na gharama zao.Nipo dar
 
wakuu naomba mrejee kwenye kichwa cha uzi.nina laptop nataka niitume songea,naomba mwenye kujua watu wanaofanya hii kazi na ikiwezekana na gharama zao.nipo dar

nenda ubungo bus terminal uliza basi za super feo utaipata ofisi zao na mzigo utafika mpaka songea au mbinga kabisa
 
Ahsante mkuu,vipi kuhusu usalama wa mzigo?
 
ahsante mkuu,vipi kuhusu usalama wa mzigo?

mara nenda ile magari yanapofika mkabizi dreva au konda kisha mpe posho yake chukua namba,hakikisha unaenda ofisini kuomba namba ya dreva na jina lake kabla gari haijafika,ili ikifika unalinganisha namba na jina unakuwa na uwakika
 
we unataka kutoa sadaka!!:shock::shock::shock::shock: wezi wakubwa wasafirisha mizigo bora uagize kwa mtu unayemjua
 
Secret Star usimwogopeshe mwenzio bana huyo mtu unayemjua akikwambia kuwa ameibiwa kwenye basi utamdai? mbona kila siku tunasafirisha vitu vya thamani na vinafika popote tanzania kwa kutumia haohao unaowaita wezi? Ze Heby hiyo laptop usimpe dereva wala conductor, ifunge vizuri ipeleke kwenye Ofisi za Super Feo Express, Shule ya Uhuru jirani na ofisi za Kampala Couch (usipeleke ubungo, mizigo yote ni ofisi ya kkoo), ikabidhi pale na uwaambie wazi kuwa ni laptop (for extra care), utaandikiwa risiti inayoonesha umesafirisha laptop, bei ni 20,000/- (elfu ishirini) kwa laptop moja. Ondoa shaka mzigo wako utafika salama salmini, usisahau kuandika jina na namba ya unayemtumia juu ya parcel, pia hakikisha kuwa ana kitambulisho atakachowasilisha siku ya kuchukua mzigo.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom